Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Man City iko tayari kumsajili Fernandez wa Chelsea

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wako tayari kufikia bei inayotakiwa na Chelsea kwa ajili ya Enzo Fernandez, huku Blues wakitaka pauni milioni 120 kwa kiungo huyo wa kati raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)
Liverpool na Brighton zimefanya mazungumzo mapya siku ya Jumapili kuhusu winga raia wa Gambia, Yankuba Minth, 22, huku Reds wakifikiria kutoa ofa ya tatu. (TeamTalk)
Beki wa kushoto wa Barcelona na Uhispania, Alejandro Balde, 22, amempa ruhusa wakala wake Jorge Mendes kujadili uhamisho wake kwenda Manchester United. (Sport)
Aston Villa wamewasiliana na klabu ya Ubelgiji, Club Brugge kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa kati raia wa Ecuador, Joel Ordonez, 22. (David Ornstein)

Chanzo cha picha, Getty Images
Brentford wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 37 kwa ajili ya beki wa West Ham United na Senegal, El Hadji Malick Diouf, 21. (Football Insider)
Manchester United haitamuuza mshambuliaji wake raia wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, 25, chini ya pauni milioni 40 huku Juventus, Napoli na Aston Villa zikionyesha nia ya kumsajili. (Sun)
Kocha mkuu wa Juventus, Luciano Spalletti anasisitiza kwamba mshambuliaji raia wa Uturuki, Kenan Yildiz, 21, hatauzwa kwenda Arsenal. (Metro)
Barcelona wanapuuza ripoti zinazowahusisha kumtaka beki wa kati wa Sporting na Ureno, Goncalo Inacio, 24, wakisema hakuna makubaliano au mkataba wowote. (Fabrizio Romano)
Kocha mkuu wa Sporting, Rui Borges, hajaondoa uwezekano wa uhamisho wa Inacio kwenda Barcelona au AC Milan baada ya kumwacha nje ya kikosi chake cha kwanza katika ushindi wao dhidi ya Alverca siku ya Jumamosi. (Goal)
RB Leipzig wamefikia makubaliano ya mdomo na AC Milan kumsajili tena mshambuliaji raia wa Ufaransa, Christopher Nkunku, 28, kwa mkopo wa msimu mzima na chaguo la kumnunua. (Sky Sports Germany)















