Kuna tofauti gani kati ya Freemason na Illuminati?

Chanzo cha picha, Alamy
- Author, Dave Roos
- Nafasi, history.com
- Iliyochapishwa
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Kwa karne nyingi, Freemasons na Illuminati wamehusishwa na nadharia za njama (conspiracy theory), kwamba ni watu wanaoongoza matukio ya dunia. Kwa kweli, makundi yote mawili yalianzishwa katika karne ya 18 (Enlightenment Era) kwa misingi wa udugu, usawa na utafutaji wa maarifa.
Illuminati ilianza kama "kundi la wasomaji" la siri la wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopinga mafundisho ya kidini na waliojitolea katika ugunduzi wa kisayansi.
Kadiri ilivyokuwa ikikua, waliongeza wanachama wengi kutoka Freemasonry, kundi maarufu la kidugu ambalo tayari lilikuwepo kwa karne moja nyuma. Baada ya muda, Illuminati walijumuisha baadhi ya mila na alama za Freemason ili kuongeza mvuto wa kundi lao la siri.
Kwa hivyo, kuna mwingiliano fulani kati ya Freemasonry na Illuminati. Makundi yote mawili yaliwahudumia watu mashuhuri wenye mawazo huru, lakini yalidumisha viwango tofauti vya usiri.
Freemason na Illuminati

Chanzo cha picha, Getty Images
Freemason walikuwa mafundi stadi waliosaidia kujenga makanisa makubwa ya Gothic ya Uingereza na Ulaya katika Enzi za Kati. Freemason walitengeneza mabango na manenosiri ili kuthibitisha uanachama wao walipokuwa wakisafiri kutoka nchi hadi nchi. Wakati fulani, vikundi vya Freemason vilianza kukubali "wanachama wa heshima" ambao hawakuwa mafundi ili kuongeza idadi yao.
Katika karne ya 17, Freemason walibadilika kutoka kundi la mafundi stadi hadi jamii ya kindugu kwa ajili ya maendeleo na ujamaa. Baraza la kwanza linalojulikana Grand Lodge liliundwa London 1717, ambalo linazingatiwa kama siku ya kuzaliwa kwa Freemason ya kisasa.
Baraza la Illuminati halikuundwa hadi mwaka 1776. Lilikuwa wazo la profesa wa chuo kikuu cha Ujerumani, Adam Weishaupt, ambaye aliwaingiza wanafunzi katika kitivo cha School of Humanity, kitivo cha siri. Jina la kwanza la Weishaupt kwa kundi hilo lilikuwa "Wanaopenda Ukamilifu."
"Jina hilo lilionyesha imani ya Weishaupt katika uwezekano wa kuunda ukamilifu wa jamii ya wanadamu," anasema Reinhard Markner, mwanahistoria ambaye ni mtaalamu wa jamii za siri za kisasa.
Weishaupt alibadilisha jina la kikundi hicho kuwa "Illuminati" mwaka 1778 katika juhudi za kuendeleza dhamira yake ya kupingana na nguvu za "giza," haswa Makanisa ya Kikristo na mtu mwingine yeyote anayepinga uhuru na uhuru wa mawazo.
Illuminati Ilikuwa jamii ya siri
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika karne ya 18, kuwa Freemason haikuwa kitu cha kuficha, anasema Olaf Simons, sehemu ya Kundi la Utafiti la Illuminati katika Chuo Kikuu cha Erfurt nchini Ujerumani.
"Ukiwa ni Freemason ni jambo ambalo lilivutia," anasema Simons. "Kile ambacho hutakiwi kukizungumza na watu wa nje, ni kile unachofanya wakati wa ibada na sherehe za Freemason.”
Freemason hupitia viwango vitatu tofauti au "digrii" wanapoingizwa kwenye klabu: mwanafunzi aliyeingia (entered apprentice), mfanyakazi mwenza (fellowcraft) na mtaalamu wa uashi (master mason). Kila moja ya safu hizi ina ibada yake ya utangulizi iliyojaa siri, mavazi ya sherehe na ishara. Maelezo ya sherehe hizo ndiyo ambayo Freemason huapa kuyaweka siri.
Kwa upande mwingine, Illuminati waliweka kila kitu siri. Mara nyingi waliwasiliana kwa kutumia alama za siri na kutajana kwa majina ya siri. Illuminati waliita vikundi vyao vya ndani "Makanisa ya Minerval" na wakawaingiza wanachama kimya kimya kutoka vyuo vikuu na nyumba za kulala wageni za Freemason.
Alama za Freemasonry na Illuminati

Chanzo cha picha, Getty Images
Enzi ya Mwangaza haikupinga tu mamlaka ya kanisa, bali pia ilitikisa makundi ya viongozi wenye nguvu katika jamii. Markner anasema kwamba moja ya vivutio vikubwa vya Freemasonry ni kwamba ilitoa nafasi mpya ya kijamii ambapo watu wenye nguvu za utawala wangeweza kuchanganyika na watu mabwanyenye.
"Kulikuwa na vipengele vya uhuru' pia," Markner anasema. "Ndani ya mipaka ya makao makuu ya Masonic, ungeweza kuzungumza kwa uhuru na wenzako."
Kufikia 1783, "kikundi cha wasomaji" cha Weishaupt kilikuwa kimekua na kuwa jamii ya siri yenye mamia ya wanachama kote Ujerumani.
Freemasons na Illuminati wanahusishwa na aina fulani ya alama, hasa "Jicho la Mungu" ama “Eye of Providence” linaloonekana nyuma ya noti ya dola 1.
Kulingana na Markner na Simons, jicho maarufu ndani ya pembetatu halina uhusiano wowote na Freemasonry au Illuminati. Ilikuwa ishara maarufu ya Kikatoliki ya Utatu Mtakatifu inayoonyeshwa katika makanisa ya Jesuit kote Ulaya.
Hata hivyo, Makumbusho ya Kitaifa ya Masonic ya George Washington yanadai kwamba "jicho linaloona yote" lilitajwa katika maandishi ya Masonic ambayo hayajachapishwa kutoka karne ya 18.
Piramidi alama nyingine katika noti ya dola pia huhusishwa Freemason na Illuminati. Ingawa ni kweli kwamba nembo za Wamisri zilijumuishwa katika sherehe za Freemason na Illuminati, ikiwa ni pamoja na piramidi inayowakilisha kazi, piramidi haikuwa alama kuu kwa kundi lolote. Kwa Freemason, Markner anasema Hekalu la Sulemani lilikuwa na umuhimu mkubwa zaidi wa ibada kuliko piramidi.
Alama maarufu zaidi katika Freemasonry ni dira na mraba, vifaa vya uchongaji wa mawe vinavyoonekana nje ya nyumba za kulala wageni za Masonic na kwenye mavazi ya sherehe, mara nyingi zikiwa na herufi kubwa "G"." "Hiyo inawakilisha uhusiano kati ya Freemasonry na uchongaji wa mawe na usanifu," Markner anasema.
"Alama pekee ya Illuminati ni bundi na kitabu," anasema Simons. Weishaupt alipoanzisha Illuminati, alichagua picha ya bundi aliyeketi kwenye kitabu kilicho wazi ili kuwakilisha Minerva au Pallas Athena. "Athena, binti wa Zeus, ndiye mungu wa hekima na mwanga," anaelezea Simons, "na Illuminati wanatakiwa kuleta mwanga duniani."
Kilichowapata Illuminati na Freemasons

Chanzo cha picha, getty image
Serikali ya Bavaria ilinyakua vifaa vya Illuminati na kuviweka hadharani mwaka 1787. Kwa mila zao na mawasiliano yao binafsi kufichuliwa kwa ulimwengu, ikawa chanzo cha mvuto, hofu na kejeli.
"Mara tu Wabavaria walipoweka hadharani nyenzo za Illuminati, kundi hilo liliporomoka," anasema Simons. "Ukawa mwisho wa kundi hilo, kwa sababu halina siri zozote za kuwapa wanachama wapya. Siri hiyo imefichuliwa." Kiongozi wa Bavaria alipiga marufuku Illuminati, na Weishaupt akaenda uhamishoni.
Baada ya Illuminati kufichuliwa, haikuchukua muda mrefu kwa nadharia za kwanza za njama kuanza kusambaa. Baada ya Mapinduzi ya Ufaransa, watu walijaribu kuwatenga wanamapinduzi kwa kudai kwamba jambo zima lilipangwa na Illuminati, ambayo ilikuwa imekufa kwa miaka mingi na haikuwahi kufanya kazi nchini Ufaransa, anasema Simons.
Kwa upande mwingine, Freemason haikupotea kamwe. Ilipoteza mvuto wake, lakini bado kuna matawi mengi ya Freemason, ikiwa ni pamoja na Shriners International, shirika la hisani la kindugu.















