Moja kwa moja, Lissu: “Ni ushahidi wako kwamba mimi ni mhaini?”Shahidi: “Sijasema hivyo”
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, Jumanne Agosti 11, 2026, ameendelea kumuhoji shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka kuhusu uhaini, uchaguzi na Katiba.
Kesi yahahirishwa mpaka kesho Alhamisi Agosti 12, 2026
Upande wa Jamuhuri wameomba ahirisho la kesi kwa sababu hawakujiandaa na shahidi mwingine
Lissu: Ninaomba ile amri ya Mahakama ya kuwa wanapaswa kuja na mashahidi wawili, tumechelewa sana na sio kwa sababu zangu ni kwa sababu zao, mimi naendelea kukaa gerezani na sina hatia. Kuanzia kesho waje na mashahidi wa kutosha
Jaji: Shauri lina ahirishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi...
Shahidi wa 16 wa Jamhuri amaliza kutoa ushahidi wake
Upande wa Serikali, Katuga, unamuuliza Shahidi, Mahamba
Katuga: Naomba ufafanuzi waambie majaji yale maneno yaliyoko kwenye hati ya mashitaka tutakinukisha, kuna neno serikali wafafanunulie majaji ulimaanisha nini
Shahidi: Nilipotamka neno serikali lipo nilimaanisha serikali ndio nyenye mamlaka ya kutekeleza na kusimamia sheria za nchi kwa hiyo kutamka maneno kama hayo kwamba utauzia uchaguzi au utavuruga uchaguzi ni kuitishia serikali kwani ndio ina wajibu wa kulinda amani ya nchi
Katuga: Tuendelee kujikita hapo hapo uliulizwa ni nani aliyechapisha mtandaoni ukamkomalia ukamwambia ni wewe na akaenda mbele akuuliza je akina P na P1 walifanya nini ukasema wao walisambaza na yeye ndio alichapisha ifafanulie Mahakama ulimaanisha nini?
Shahidi: Nilimaanisha kwamba mshitakiwa alikuwa akiongea mbele ya waandishi wa habari ambao walikuwa wakirusha yale matangazo tunaamuni kwamba hiyo ilikuwa ni nia yake na kama alikuwa hataki asingewaruhusu
Katuga: Ndio maana ukakomaa ni wewe ni wewe?
Shahdi: Ndio
Katuga: Uliulizwa haya maneno kunzia uchaguzi, kukinukisha je yamo kwenye kifungu cha 39/2 B
Shahdi: Yale maneno aliyotamka mshitakiwa tafsiri yangu ni kwamba kulikuwa na hiyo nia ya kuitishia serikali
Katuga: Umeulizwa sana hapa mambo ya Katiba na ukaulizwa kudai Katiba ifafanulie mahakama haya madai na kosa hili la uhaini au nini majibu yako kwenye hili la katiba na uhaini
Shahidi: Havihusiani
Katuga: Kuna maswali mengi uliulizwa juu ya mambo ya Oktoba 2025 mkaambiwa wewe na polisi mlifanya vurugu ulimaanisha nini
Shahidi: Sio kweli kwamba Polisi ilihusika kwenye vurugu ni wazi kwamba baada uchunguzi tuliofanya ulibaini kwamba kulikuwa na maandalizi ya awali
Lissu anaingilia:...Mimi sikuuliza hilo swali na kwakuwa shahidi anajibu kitu kipya nitaomba ni rudie kufanya dodoso
Katuga: Umeulizwa na mshitakiwa ushahidi uliosoma Mahakamani na ule uliandika polisi leo ukaulizwa je unataka ushahidi wako Mahakamani usiaminiwe ukasema ndio na uliandika Polisi ukasema ndio ukasema huajelezea sababu ya utofauti wa ushahidi wako wa kuandika na kuongea fafanua ulimaanisha nini uliposema sijaeleza
Shahidi: Kweli sijaeleza sababu ya hiyo tofauti ila majibu ya hapa mahakamani yalitokana na maswali niliyokuwa ninaulizwa na mawakili hapa mahakamani
Katuga: Waheshimiwa majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu .
Jaji Nduguru: Shahidi umemaliza kutoa ushahidi wako unaweza kwenda...
Lissu amuuliza shahidi: “Ni ushahidi wako kwamba mimi ni mhaini?”Ajibu: “Sijasema hivyo”
Lissu hiyo taarifa ipo Mahakamani najua kuna taarifa ilikataliwa sababu haikuandaliwa na mtaalamu ilikataliwa
Shahidi: Tuendelee
Lissu Mpaka sasa wewe ni shahidi wa 16 nyie wote hakuna aliyewasilisha ushahidi wa video na hakuna kidhibiti hata kimoja zaidi ya stori
Shahidi: Ni sahihi
Lissu: Twende kwenye mkutano wangu uliyosababisha yote haya juu ya msimamo wangu na chama changu juu ya uchaguzi na katiba
Shahidi: Sina hakika kama ulizungumzia katiba
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu madai ya mfumo wa uchaguzi na katiba ni madai ya siku nyingi
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama una fahamu mwaka 1992, Tume ya Nyalali ilipendekeza itungwe katiba mpya itakapofikia Septemba 1993
Shahidi: Sijawahi kusikia
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu mapendekezo hayo ya Jaji Nyalali yalikataliwa na CCM chini ya serikali ya Rais Mwinyi
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Rais Mkapa marehemu aliunda tume ya Jaji Robert Kisanga mwaka 1998, walipendekeza kuwe na Katiba mpya na Rais Mkapa akasema hakuwatuma waangalie hayo ya katiba
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Rais Mkapa akaunda Tume nyingine ya Jaji Mark Bomani nayo ikapendekeza katiba mpya na Mkapa na CCM yake wakakataaa
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Warioba na wakaanda rasimu ya Katiba mpya na mapendekezo ya mabadiliko kwenye mfumo wetu wa uchaguzi, Rais Kikwete naye akataaaa waeleze majaji
Shahidi: Sijawahi kusikia
Lissu: Waleze majaji kuwa tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano
Shahdi: Ni sahihi
Lissu: Tangu 1995 watazamaji wa uchaguzi huo kutoka nje kimataifa na kikanda kila kwenye uchaguzi mkuu wamependeza kwa serikali itungwe katiba mpya na mabadiliko kwenye mfumo wetu wa uchaguzi
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji mwaka 2015 ilani ya CCM ilikua na ahadi kuwa watakamilisha mchakato wa katiba mpya
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji hata mwaka 2020, CCM ya Magufuli iliahidi mchakato wa katiba mpya utakamilika
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Hata alipokuja Samia naye alikataaa
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Kila uchaguzi mkuu lazima kuwe na mauaji ya raia
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Baada ya hotuba yangu ya tarehe tatu wewe na Jeshi mlichukua hatua ya kunitafuta na kuniuliza nilimaanisha nini
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Kwa yote haya katika historia yetu ya miaka 35, No Reforms No Election ilikuwa sahihi kwenye mazingira haya
Shahidi: Hapana
Lissu: Jaji Chande anasema hivi ghasia za baada ya uchaguzi mkuu zilitokana na matatizo ambayo yamekueko kwa muda mrefu ikiwemo madai ya katiba mpya, mfumo wa uchaguzi. Maelfu ya watu wameuawa sababu ya kutotatuliwa kwa muda mrefu, je nakosea
Shahidi: Unakosea
Lissu: Kwa hiyo hata Jaji Chande na tume yake wamekosea?
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Hayo unayosema ni makosa yangu waeleze majaji kama unafahamu kikosi kazi cha kamati ya haki za binadamu umoja wa mataifa kimetoa taarifa baada ya uchunguzi wa miezi tisa imesema kukamatwa kwangu ni kinyume cha sheria na nilipwe fidia
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu tarehe 10 Juai, Kamati ya Mawaziri wanaowakilisha Jumuiya ya Madola imetoa taarifa inayoitaka serikali ya Tanzania kuniachilia huru ndani ya mwezi mmoja na wasipofanya hivyo kwenye kikao cha Septemba, watachuku hatua stahiki dhidi ya serikali ya Tanzania
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Swali langu la mwisho bwana askari kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola wote wanasema niachiliwe na ni ushahidi wako kwamba mtu huyu anayepiganiwa na Taasisi zote hizi ni mtu mbaya mhaini na anayestahili kunyongwa
Shahidi: Sijasema hivyo
Lissu amemaliza kumuhoji shahidi wa 16, Mahamba
Lissu ahoji mahakamani kuhusu mauaji ya Oktoba 29
Lissu aendelea kumuhoji shahidi wa 16 wa upande wa Mashtaka, ACP Amin Mahamba.
Lissu: Waeleze Majaji kama ulidhamiria maelezo yako ya kizimbani ya juzi yaaminiwe na mahakama kama ushahidi wa kweli
Shahidi: Nilidhamiria yatumike
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama maelezo yako uliyoandika polisi ulidhamiria yatumike mahakamani kama ushahidi wa kweli
Shahidi: Nilidhamiria yatumike
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna mahali popote umeelezea sababu ya hizo tofauti kati ya ulichoandika na ulichosema mahakamani
Shahidi: Hakuna mahali nilipoelezea
Lissu: Ushahdii wako kuhusiana na wale mashahidi waliofichwa mliowatoa mikoani unakumbuka ulisema kwamba hao mashahidi waliofichwa ni watu ambao walikamatwa na Polisi kweli si kweli
Shahidi: Kweli
Lissu: Na walikamatwa kwa kupanga njama za kufanya vurugu kwenye uchaguzi Mkuu
Shahidi: Walihamasisha
Lissu: Na walipokamatwa walikiri
Shahidi: Ndio
Lissu: Na waliandika maelezo yanayosema hivyo
Shahidi: Sahihi
Lissu: Hiyo mipango waliyokuwa wanaipanga ilikuwa makosa ya jinai
Shahidi: Kweli
Lissu: Wakakiri kwa maandishi, mkawaleta mahakamani wakakiri mahakamani au sio?
Shahidi: Ndio
Lissu: Waeleze Majaji hizo tuhuma za kijinai mlizowakamata nazo ziliishia wapi?
Shahidi: Nikirejea maelezo yangu baada ya kuwakamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa RCO tuliitisha jalada tukalisoma tukalipitia tulibaini wote walikua wamechochewa na wewe
Lissu: Ni kweli au si kweli mliwafutia kesi wote
Shahidi:.....
Lissu: Katika hao mashahidi walikuwepo waliotokea Dar es Salaam. Waeleze Majaji kama ni kweli au si kweli Dar es Salaam kulitokea vurugu zilizoua watu 182
Shahidi: Mimi sio Msemaji wa Jeshi la Polisi
Lissu: Kwa mujibu wa Tume ya Jaji Chande watu 182 waliiawa Dar es Salaam kweli si kweli
Shahidi: Si kweli
Lissu: Mliwashtaki kwa makosa mliyowakamata
Shahidi: ....
Lissu: Siku ya uchaguzi tarehe 29 kwa mujibu wa Jaji Chande waliuawa watu 23 na watu ambao mlikuwa mnajua wameandika walikuja mahakamani wakasema tutaleta fujo mmewaachia
Shahidi:Si kweli
Lissu: Umesema ulikuwa mpelelezi wa matukio ya Okt 29 Shahidi: Ndio
Lissu: Kuna watu mliwakanata Mbeya mkawaandika maelezo mkawaleta mahakamani halafu mkawaachia
Shahidi: Kweli
Lissu: Kwenye Mji wa Mbeya kwa mujibu wa ripoti ya Jaji Chande waliuawa watu 80
Shahidi:...
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama hiyo mikoa mitatu Dar es Salaam Arusha Mbeya, jumla ya watu walioawa ni watu 315 kama kuna RPC, ZPC, RCO, OCD, OCCID au Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya aliyechukiliwa hatua kwa uzembe
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Waeleze majaji kama wale waliosema wataenda kufanya vurugu na wakafanya kama kuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua mpaka sasa
Shahidi: Ni matukio mawili tofauti
Lissu: Kuma mikoa mingine nane Mkoa wa Mwanza hawakukuletea taarifa kwamba kuna shida inapangwa kwenye uchaguzi
Shahidi: Sikupata
Lissu: Mwanza Okt 29 kwa mujibu ws Ripoti ya Jaji Chande waliuawa watu 90 waeleze majaji Mwanza mna RPC
Shahidi: Ndio
Lissu: Kuna RCO, Mtu wa usalama wa taifa au mapolisi wote kama kuna aliyechukuliwa hatua kwa kutoona janga kubwa lililoukuta mkoa wa Mwanza
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Kwa Mikoa minne wameuawa watu 405 kwa mujibu wa Ripoti ya chande Songwe, Geita Mara, Shinyanga, Geita, Ruvuma katika mikoa hiyo ni Ruvuma pekee mlipewa taarifa kwamba watu wanapanga kufanya vurugu mkawakamata wakaandika maelezo ya mashtaka mkawaleta mahakamani mkawaachi ni kwel isi kweli?
Shahidi: Si kweli
Lissu: Kwa hiyo wa Songea mliwaleta mahakamani mkawashtaki
Shahidi: Waliachiwa kwa mujibu wa sheria
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama wote hawa vyombo vya ulinzi na usalama wamechukuliwa hatua yoyote
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Niambie kama nipo sahihi au nakosea kwamba katika hsitoria yetu yote kama nchi ilianza wakati wa Wajerumani mara ya mwisho katika nchi hii watu waliuawa kwa kiasi kikubwa hivyo ilikuwa 1907 wakati Wajerumani wanazima vita vya maji maji kuanzia hapo Wajerumani hawakuua watu kama ilivyokuwa mwaka jana Waingereza walikaa kwa miaka 40 hawakuua, Nyerere miaka 21, miaka 10 ya Mwinyi hayakuwepo, miaka 10 ya Mkapa hayakuwepo, miaka 10 ya Kikwete hayakuwepo, miaka sita ya Magufuli yalikuwepo kidogo sana lakini ndani ya wiki moja ya utawala wa Samia wameuawa watu 500 kuliko miaka yote
Shahidi: Sio sahihi
Lissu: Je, video mliyoangalia ikiwa mtandaoni au iliyokuwa kwenye Memory card iliyopokelewa Dodoma au kwenye flash Disc iliyoandikwa Aldepo
Shahidi: Iliyokuwa mtandaoni
Lissu: Kwa hiyo kwa jibu hilo ntakua sahihi hamkuangalia video ikiyokuwa kwenye Memory card na iliyokuwa kwenye Flash Disc
Shahidi: Hatukuangalia
Lissu: Nitakuwa sahihi au nitakosea nikisema kwamba pengine kwenye hiyo flash disc Aldeepo hakuna video yoyote
Shahidi: Sio sahihi
Lissu: Unajuaje wakati hukuangalia
Shahidi: Si kuna taarifa
Lissu: Unafahamu kama hata mahakamani hazikuletwa?
Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu inaendelea, Mahakama inasikiliza ushahidi
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, inaendela sasa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Lissu ameendelea na maswali ya dodoso ya shahidi wa Jamhuri, ACP Amin Mahamba.
Katika maswali ya leo, Lissu amemuuliza Mahamba kuhusu watu waliokamatwa kabla ya uchaguzi kwa tuhuma za kupanga vurugu na baadaye kuachiwa baada ya majalada yao kupitia upya.
Mahamba amethibitisha kuwa baadhi ya watu hao walikamatwa wakiwa wanatuhumiwa kupanga njama na vurugu, na kwamba baadaye mashtaka yao yalifutwa.
Lissu pia amemuuliza kuhusu matukio ya vifo Dar es Salaam, Arusha na Mbeya, akirejea takwimu za Tume ya Jaji Chande zinazodai watu 315 waliuawa katika maeneo hayo.
Alipoulizwa kama kuna makamanda wa polisi au viongozi wa serikali waliochukuliwa hatua kutokana na vifo hivyo, ACP Mahamba amesema hana hakika kama kuna aliyechukuliwa hatua.
Lissu amesema hana maswali mengi leo na anataka kumaliza “loose ends” katika ushahidi wa shahidi huyo.
Yaliyojiri jana Lissu akiendelea kumuhoji shahidi wa 16 katika kesi ya uhaini
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anaendelea kumuhoji Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Lissu alianza kumuhoji shahidi huyo jana, baada ya Mahamba kumaliza kutoa ushahidi wake wa msingi. Katika hatua ya maswali ya dodoso, Lissu ameuliza karibu maswali 300 akichunguza upelelezi wa kesi hiyo na tofauti kati ya ushahidi wa shahidi mahakamani na maelezo yake ya awali.
Kesi ya Lissu ilifikia wapi?
Julai 30, 2026, Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali ombi la Jamhuri la kutaka kuwasilisha ushahidi wa nyongeza katika kesi hiyo.
Mahakama hiyo ilikubaliana na hoja za Lissu kwamba kifungu cha sheria kilichotumiwa na upande wa mashtaka hakikuruhusu ushahidi huo kuwasilishwa katika hatua hiyo ya kesi.
Kesi hiyo imeanza tena baada ya kusimama tangu Februari 24, 2026, na imepangwa kusikilizwa kwa mfululizo hadi Septemba 7, 2026.
Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Upande wa mashtaka unahusisha shtaka hilo na kauli alizotoa kuhusu kusudio la kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kilichojiri mahakamani jana
Katika maswali yake, Lissu amekuwa akimuuliza shahidi kuhusu namna upelelezi wa kesi hiyo ulivyofanywa, akilenga pia tofauti kati ya maelezo yake ya awali na ushahidi alioutoa mahakamani.
Katika sehemu kadhaa, shahidi amekiri kwamba mambo aliyoyataja jana katika ushahidi wake hayakuwepo kwenye maelezo yake yaliyoandikwa. Hayo ni pamoja na baadhi ya maelezo kuhusu uchunguzi wa video ya hotuba ya Lissu, hatua za upelelezi na mawasiliano na baadhi ya taasisi.
Lissu pia amemuuliza shahidi kuhusu video ya hotuba yake iliyochapishwa na Jambo TV. Alitaka kujua kama polisi walikuwa na ushahidi kwamba yeye ndiye aliyechapisha video hiyo. Shahidi amesema Lissu ndiye aliyechapisha, lakini alipoulizwa kama anajua iwapo Lissu alikuwa mfanyakazi au mpiga picha wa Jambo TV, au alikuwa na nywila za akaunti hiyo, amesema “sina hakika.”
Lissu amemuuliza pia shahidi kuhusu madai ya vitisho dhidi ya mashahidi wa upande wa mashtaka. Amehoji iwapo majina ya watu waliodaiwa kutishiwa, aina ya vitisho, tarehe na maeneo yalitajwa katika hati ya kiapo ya shahidi.
Katika sehemu nyingine ya maswali, Lissu amemuuliza shahidi kuhusu watu waliokamatwa au kushtakiwa kwa makosa yanayohusishwa na matukio ya baada ya uchaguzi. Shahidi amesema “sikumbuki” alipoulizwa kuhusu baadhi ya kesi hizo.
Lissu pia amezungumzia historia yake ya kukamatwa na kufunguliwa kesi mbalimbali na polisi, akisema: “Kwa karibu robo karne naonewa.” Shahidi amesema hafahamu kuhusu matukio kadhaa aliyoyataja, huku akikiri kufahamu tukio la mwaka 2017 ambapo Lissu alipigwa risasi.
Aidha, Lissu amemuuliza shahidi kama katika upelelezi wake alizingatia haki za kikatiba za kutoa maoni na kukutana, pamoja na iwapo alishirikisha taasisi nyingine za usalama katika upelelezi huo.
Kesi inaendelea leo, Agosti 12, 2026, Lissu akitarajiwa kuendelea kumuhoji shahidi huyo wa 16 wa upande wa mashtaka.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anaendelea leo kumuhoji Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Lissu amekuwa akimuhoji shahidi huyo tangu Jumatatu, Agosti 10, huku jana akiendelea na maswali ya dodoso (cross-examination) kwa mfululizo wa maswali kuhusu upelelezi wa kesi hiyo, ushahidi wake mahakamani na tofauti kati ya ushahidi huo na maelezo yake ya awali.
Kwa siku mbili za mahojiano, Lissu amemuuliza shahidi huyo karibu maswali 300, huku sehemu kubwa ya maswali ikijikita katika upelelezi wa polisi na ushahidi unaohusishwa na video ya hotuba yake iliyochapishwa na Jambo TV.
Kesi hiyo inaendelea leo katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. BBC inaendelea kufuatilia kinachojiri mahakamani.
KARIBU TENA SIKU YA 3 YA USIKILIZWAJI WA KESI YA UHAINI YA LISSU BAADA YA KUANZA TENA
Yaliyojiri leo katika kesi ya uhaini ya Lissu, ikihairishwa hadi kesho, Kwa ufupi kilichojiri leo
Chanzo cha picha, Getty Images
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ameendelea leo kumuhoji Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Katika maswali ya dodoso (cross-examination), Lissu amekuwa akimhoji shahidi kuhusu upelelezi wa kesi hiyo, akilenga hasa tofauti kati ya ushahidi alioutoa mahakamani na maelezo yake ya awali. Shahidi amekuwa akijibu mara kwa mara kuwa baadhi ya mambo aliyoyataja kwenye ushahidi wake wa jana Mahakamani hayapo katika maelezo yake yaliyoandikwa.
Lissu pia amemuuliza shahidi kuhusu namna video ya hotuba yake iliyochapishwa na Jambo TV ilivyopatikana na kuchunguzwa, ulinzi wa mashahidi, mawasiliano na Ofisi ya DPP pamoja na maafisa wengine wa usalama. Amehoji pia madai ya polisi kuhusu vitisho kwa mashahidi na kama ushahidi huo uliainishwa katika maelezo ya shahidi.
Katika sehemu nyingine ya maswali, Lissu ameuliza kuhusu historia yake ya kukamatwa na kufunguliwa kesi mbalimbali na polisi, akisema amekuwa akionea na jeshi hilo kwa karibu robo karne. Shahidi amesema “sifahamu” alipoulizwa kuhusu matukio mengi ya nyuma, huku akikiri kufahamu kuwa Lissu alipigwa risasi mwaka 2017.
Lissu pia amehoji kama polisi walikuwa na ushahidi kwamba yeye ndiye aliyechapisha video hiyo kwenye YouTube ya Jambo TV. Shahidi amesema “ndio”, lakini alipoulizwa kama anafahamu kama Lissu alikuwa mfanyakazi, mpiga picha au alikuwa na nywila za Jambo TV, amejibu mara kadhaa “sina hakika.”
Kesi imeahirishwa hadi kesho, Agosti 12, 2026, ambapo Lissu anatarajiwa kuendelea na maswali ya dodoso ya shahidi huyo.
Lissu anaendelea, nikweli au si kweli ulichaguliwa kuwa mpelelezi wa matukio ya baada ya uchaguzi
kama mpelelezi mkuu wa matukio hayo
Shahidi: Sikua mpelelezi wa matukio hayo nilikua kwenye team lakini sikua mpelelezi wa matukio hayo.
Lissu: Kutokana na upelelezi wa timu yako kuna watu walishitakiwa kwa uhaini kama mimi?
Shahidi: Sikumbuki.
Lissu: Kesi ya Paulina Palyango na wenzake 75 ya kula njama.
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Pia Niffer na wenzake shtaka la kwanza kula njama la pili uhaini
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Omar Pandu Salum na wenzake 33 na hili unalikumbuka?
Shahidi: Sikumbuki.
Lissu: Waeleze majaji hukumbuki kuna watu wengi sana walikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini jumla ya watu 673 nchi nzima kwa upelelezi wako na wenzako.
Shahdii: Sikumbuki na mimi sio msemaji wa Jeshi.
Lissu: Waeleze majaji kwamba kesi zote hizi zilifutwa
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Nakurejesha kwenye mikutano ya hadhara, waeleze majaji kama sheria inazuia hii mikutano wakati wa uchaguzi tu.
Shahidi: Sina jibu.
Lissu: Pamoja na waandishi wa jambo unafahamu kulikuwa na waandishi wa Azam, ITV, Arusha one digital, Clouds media , walikuwepo waandishi wa Chanzo TV
Shahidi: Ndio ninafahamu
Lissu: Waeleze majaji kuwa hawa waandishi wengine walirusha mkutano kwenye vyombo vyao.
Shahidi: Walirusha kutokea kwa Jambo
Lissu: Waandishi wa habari wote hawa walifahamu hayo maneno na kuyarusha?
Shahidi: Kufahamu sijui ila waliyarusha.
Lissu: Mtu anayepata taarifa za uhaini anapaswa azitolee taarifa polisi ni iweli sio kweli?
Shahidi: Ndio
Lissu: Na huyu mtu asipotolea taarifa polisi anakuwa amefanya kosa la kuficha uhaini?
Shahidi: Sifahamu sina hakika nayo.
Lissu: Kuna hata mmoja kati ya waandishi hawa aliyetoa taarifa
Shahidi: Hakuna.
Lissu: Mtu ambaye amechapisha maneno hayo si anakua amefanya kusambaza?
Shahidi: Hawakufanya kosa
Lissu: Kwenye huo mkutano kulikua na watu zaidi ya 300 waeleze majaji kama hata mmoja alileta taarifa
Shahidi: Hakuna.
Lissu: Kuna hata mmoja kati yao ukiacha mimi alituhumiwa.
Shahidi: Hapana.
Lissu: Ulikuwa mkuu wa upelelezi waeleze majaji kama ndio ulitoa amri nikamatwe.
Shahidi: Hapana.
Lissu: Je ni kweli au sio kweli aliyetoa maelekezo nikamatwe ni Ramadhani Kingai
Shahidi: Ulikuwa umekamatwa kupitia boss wangu Ramadhani Nganzi
Lissu: Ni kweli si kweli DCI Kingai aliwapa maelekezo kuwa mtawasiliana naye kupitia Ramadhani nganzi
Shahidi: Ndio ni kweli.
Lissu: Je ni sahihi kusema kwamba DCI kingai alitoa taarifa kwa nganzi awape taarifa kwamba Lissu amekamatwa analetwa Dar es salaam.
Shahidi: Ndio
Lissu: Nani kati yako na msaidizi wako George Padem nani alitoa amri lifunguliwe jalada la uhaini?
Shahidi: Wakati nateuliwa nilikuta tayari wameshafungua file
Lissu: Waeleze majaji kama umesoma maelezo ya Geogre Padem amekuzungumzia wewe kwa sentensi mbili tu
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Ulikuta kazi yote imefanyika na hukufanya la maana ndio maana umetajwa kwa mistari miwili tu
Shahidi: Sina hakika.
Lissu: Nataka nizungumzie la kwangu na mgogiro wangu wa muda mrefu wa Jeshi, waeleze majaji kama unafahamu kwamba kwa karibu robo karne jeshi la Polisi limenionea sana kwa kunikamata na kunifungulia kesi za uongo
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu 2002 nilikamatwa na kufungiwa central
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu ilipofika mwaka 2008 wakaifuta
2011 nilikamatwa na jeshi la polisi nikachaniwa nguo na kufungwa machakani na kesho yake nikafunguliwa shauri la ilegal trace passing
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu mwaka 2012 nilikamatwa kwa kusimama na wananchi wa Arusha ambao ndugu zao waliuawa na kesi ilifutwa.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji mwaka 2013 pia nilikamatwa kusimama na wananchi wa Arusha na kesi ikafutwa.
Shahidi: Sifahamu
Lissu: 2016 nilisema iwapo uchaguzi utarudiwa Zanzibar uliofutwa na Jecha kungetokea maaafa na Kingai na Hamduni walikuja kutoa ushahidi nikawakaanga kama wewe na aliyetoa amri nikamatwe ni Camilius Wambura leo ni IGP.
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Hujajua kwamba hiyo kesi ilikuja kufutwa nikiwa Ubelgiji nikiwa napigania uhai wangu 2021.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji 2017 kama unafahamu nilikamatwa jimboni kwangu na kushtakiwa kwa kosa la uchochezi Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Mwigulu Nchemba akawaambia huyo mbunge mnamsafirisha usiku akigongwa na malori.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Nilikamatwa nikiwa bungeni 2017 nje baada ya kumwita Magufuli dikteta uchwara na kushtakiwa kwa uchochezi.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kati ya Juni 2016 na Julai 20217 nilikamatwa mara nane na kufunguliwa kesi mara sita na zote zilifutwa mwaka 2021
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kwamba sijawahi kutiwa hatiani hata mara moja sina criminal record.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kama baada ya majaribio hayo ya kuninyamazisha nililetewa watu wasiojulikana nikapigwa risasi
Shahidi: Nafahamu
Lissu: Hata watu kuniombea polisi waliwapiga marufuku, hata watu kunitolea damu walikatazwa, wakenya ndio walinitolea damu
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Kwa karibu robo karne naonewa kama ilivyo kwenye kesi hii.
Kesi imeahirishwa mpaka kesho.
"Mnanitesea nini kama mna ushahidi dhidi ya mnaosema wana makosa"
Chanzo cha picha, AFP
Lissu: Shahidi ni kweli au si kweli mmoja wa maafisa wa polisi walioshughulika na upelelezi wa kesi hii ni 'Assistant Andrew Chulu ndiye aliyechukua ile memory card kwa mashahidi P na P1 akavileta Dar es Salaaam.
Shahidi: Ndio
Lissu: Waeleze majaji kama ulisoma maelezo ya inspekta Andrew Chulu
Shahidi: Nimesoma
Lissu: Na umesema ulisoma maelezo ya P
Shahidi: Sijayasoma
Lissu: Waeleze majaji mnanitesea mimi nini kama mna ushahdi wa hao mnaosema wamefanya makosa
Shahidi: Huteswi
Lissu: Ninakurudisha kwenye PGO 1/25 crimes are acts defined by the law upelelezi wa polisi lazima ufuate masharti ya sheria kwa mujibu wa PGO tendo la kuvuruga uchaguzi ni uhaini.
Lissu: Kila askari polisi ana wajibu wa kuheshimu haki na uhuru wa raia na kufanya tofauti haikubaliki.
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Waeleze majaji kwenye maelezo yako polisi mwaka jana wameonesha kuzingatia uhuru wangu
Lissu:Kwenye maelezo yako kuna eneo ulilozingatia uhuru wangu kwa mujibu wa katiba?
Shahidi: Kimya
Lissu: Kimya maana yake hakuna, ibara ya 19/1 kwenye katiba kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra
20/1 kila mtu anao uhuru wa kukutana wengine na kuchangamana na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani.
Lissu: Chama changu kiliitisha uchaguzi wakaalika waandishi wa habari mwenyekiti wa chama akatoa maoni yake hadharani ulizingatia uhuru wangu?
Shahidi: Maneno yalikua ya vitisho
Lissu: Nilimtisha nani, Serikali?
Lissu: Nina haki ya kufaidi haki zote kwenye katiba waeleze majaji kama umezingatia haki zangu na umeandika kwenye maelezo yako
Shahidi: Hakuna
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba kwenye mkutano huo nilishambulia sana mfumo wa uchaguzi na nilisema mfumo umekua ukiipemdelea CCM na watumishi wote wa serikali wamekua wakiipendelea CCM na nilisema Tume ya uchaguzi wamekuwa na Tabia ya kuengua wagombea wa upinzani, mfano uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji ni kweli sio kweli?
Lissu: Waeleze majaji kama ulishirikisha Ikulu, Ofisi ya Waziri Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.
Shahidi: Sikuwashirikisha
Lissu: Je, uliwajulisha Ofisi ya DPP?
Shahidi: Ndio niliwajulisha
Lissu: Ulimshirikisha nani?
Shahidi: Mheshimiwa Mayenga
Lissu: Waeleze majaji kama iko kwenye maelezo yako D15
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kuratibu upelelezi wa makosa ya Jinai ni DPP kupitia mawakili wake, sasa waeleze majaji ni DPP yupi au mwanasheria yupi toka kwa DPP aliyeratibu upelelezi wako
Shahidi: Ni ofisi ya DPP ndio yule niliyekwambia jana sikumbuki jina ana jina gumu la kibantu
Lissu: Tutapeleka kwa DPP Mwakitalu atupe hilo jina
Lissu: Umesema wewe ni shahidi mbobevu wa miaka mingi waeleze majaji kama umewahi kusimamia upelelezi kesi yoyote ya kisiasa.
Shahidi: Hapana sijawahi.
Lissu: Hii ni ya kwanza?
Shahidi: Ndio
Lissu: Umewahi kushiriki kusimamia upelelezi au kisimamia kesi ya mwanasiasa kama Tundu Lissu?
Shahidi: Hapana
Lissu: Umesema kwenye kitengo x unachofanyia kazi kinashughulikia pia makosa ya mtandao na iwapo ushasimamia kesi ya makosa ya kimtandao
Shahidi: Nimeshawahi
Lissu: Ni kesi gani hiyo?
Shahidi: Ni ya yule aliyekutangulia Mheshimiwa Mbowe na Dokta Slaa
Lissu: Waeleze majaji hiyo kesi iliishia wapi
Shahidi: Iliisha
Lissu: Ilishia wapi?
Shahidi: Mh. DPP hakuwa na nia ya kuendelea na kesi.
Lissu: Kwanini?
Shahidi: Ushahidi haukutosha
Lissu: Nitakuwa sahihi nikisema kwa miaka yako 26 ni kesi moja tu ya masuala ya kimtandao ambayo umesimamia na ukashindwa
Shahidi: Hapana ziko nyingi nimetaja moja tu
Lissu: Nauliza hivyo kwasababu nataka kujua uelewa wako jana ulisema mimi ndio nilichapisha hiyo video kwenye mtandao wa youtube wa jambo tv
Shahidi: Ndio ni wewe
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu maana ya neno chapisha yaani publish. Waeleze majaji kama mimi ndio niyechapisha hiyo video kwenye jambo tv huko youtube
Shahidi: Ni wewe
Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mfanyakazi wa Jambo TV
Shahidi: Sina hakika
Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mpiga picha wa Jambo TV
Shahidi: Sina hakika
Lissu: Waeleze majaji kama nina nywila za mtandao wa Jambo TV
Shahidi: Sina hakika
Lissu: Na wewe ndio mpelelezi uliyepeleleza na huna hakika na yote
Shahidi kabaki kimya
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba hiyo video ilichukuliwa na shahidi anayeitwa na P1 mfanyakazi wa Jambo TV
Shahidi: Si kweli
Lissu: Waeleze kama umesoma maelezo ya P1
Shahidi: Sijasoma
Lissu ni kweli au si kweli kwamba P1 aliandika maelezo haya “tulikua na kamera tatu siku hiyo na tulikuwa tunarusha kwenye chaneli yetu ya Jambo Tv je hayo sio maelezo ya P1?
Shahidi: Ndio
Lissu: Je ni kweli au si kweli aliekezwa P1 kutoa memorikadi, Je ni kweli kwamba kwenye maelezo P alisema alikuwa na wenzake watatu ndio walikua wana fanya hiyo kazi na kurisha mkutano wa mtuhumiwa?
Shahidi: Ndio
Lissu: Waeleze majaji kama ulisoma maelezo ya shahidi namba moja George Banem na alisema hiyo video ilirekodiwa na kurushwa na wafanyakazi wa Jambo TV
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Waleze majaji Mkurgenzi wa Jambo Tv, John alipata mwaliko toka kwa Ofisi habari na sio mimi Tundu Lissu
Lissu: Waeleze majaji kama huo ndio utendaji wa Jeshi la polisi Tanzania
Shahidi: Hapana
Lissu: Waeleze majaji kama ni ushahidi wako kwamba mwenyekiti anawajibika kijinai kwa makosa ya wanachama wake.
Lissu: Kesi ya uhaini sio rahisi haijawahi kuwa rahisi, ni kiapo chako kweli si kweli
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Kuna mahali popote umesema shahidi alitishiwa kupigwa
Shahidi: Ipo
Lissu: Isome tafadhali.
Shahidi: Naona hii hapa “body harm”
Lissu: Body harm inaweza kuwa na namna nyingi, je, kwenye kiapo chako kuna mtu alipigwa aliambiwa tutakuua tutachoma nyumba tutashambulia familia yako?
Shahidi: hiyo haipo
Lissu: Sasa shahidi kuhusiana na hii habari ya mashahidi kutishiwa, waliletwa mashahidi niliwauliza swali je ulitishiwa kupigwa, ndugu zako au kudhuriwa wote walisema hapana sasa wewe unadai walitishiwa Je mahakama ifuate ushahidi wa nani?
Shahidi: Wakwangu
Lissu: Shahdi angalia hicho kielelezo chako mwanzo kabisa... Makazi Goba njia Nne kata ya Matosa waeleze majaji kama kweli si kweli Goba iko halmashauri ya manispaa ya Ubungo.
Shahidi: Sijui
Lissu: Hujui, Goba iko manisapaa ya Ubungo?..nataka nimsomee shahidi aelewe maeneo.
Anamsomea maneo yote ya ubungo.
Lissu: Waeleze majaji wewe umeandika kata gani
Shahidi: Kata ya matosa.
Lissu: Shahidi twende kwenye kielezo D15 waeleze majaji nani ameandika hayo maelezo.
Shahidi: Nimeandika mwenyewe.
Lissu: Hayo ni maelezo waeleze majaji kama shahidi ana uwezo wa kujiandikia maelezo yake mwenyewe kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai.
Shahidi: Shahidi yeyote maelezo yake yanachukuliwa na afisa wa polisi.
Lissu: Kwenye hayo maelezo aliyekupa onyo kama shahidi ni nani?
Shahidi: Nimetoa tamko
Lissu: Hilo tamko umelitoa mbele ya nani mbele ya afisa gani wa polisi?
Shahidi anajieleza
Lissu: Wewe si umesema ni polisi mimi mwanasheria
Lissu: Hilo tamko umetoa mbele ya nani?
Shahidi: Nimeandika mwenyewe
Lissu: Kuna sehemu ya saini ya mtoa maelezo hapo amesaini nani?
Shahidi: Mwenyewe
Lissu: Na hapo chini sehemu ya afisa aliyeandika maelezo
Shahidi: Nimesaini mwenyewe.
Lissu: Kwenye maelezo yako D15 umesema majukumu yako ni kulinda raia na mali zao.
Shahidi: Ndio
Lissu: Na ulisema uko kwenye kitengo x
Shahidi: Ndio
Lissu: Waleze majaji kama kazi za kitengo X ni pamoja na kulinda raia na mali zao
Shahidi: Ndio
Lissu: Unafahamu PGO
Shahidi: Ndio
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi apewe nakala yangu ya PGO sidhani kama wanayo.
Shahidi anapokea..
Lissu: Waeleze majaji kama hayo yaliyotajwa ni sehemu ya majukumu ya kitengo X kwenye kulinda raia na mali zao. Nimekuwekea alama order 6/8
Shahidi: Swali ni nini?
Lissu: Je, kitengo X kina wajibu wa kulinda raia na mali zao?
Shahidi: Ni sehemu ya majukumu yetu.
Lissu: Soma yote yako manne
Shahidi anasoma
Lissu: Waeleze majaji kama polisi kuna kitengo Y
Shahidi: Ndio kipo.
Lissu: Waeleze majaji kazi zake ni nini
Shahidi: Vyote vinalinda raia na mali zao kama jukumu letu polisi.
Lissu: Waeleze majaji kama umewahi kuwa RCO Singida.
ShahIdi: Sijawahi kufanya kazi Singida.
Lissu: Hujawahi, waeleze majaji katika Jeshi la Polisi kipindi ambacho umekuwa RCO maafisa wa polisi wanaoitwa Amini Mahamba ni wangapi kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2009, mtu anayeitwa Super intendent of Police, Amini Mahamba
Shahidi:Alikuwepo afisa kama huyo lakini alikua anaitwa Amini Said Mahamba
Lissu: Waheshimiwa majaji hii ni muhimu iko kwenye kesi ya mahakama ya rufani mwaka 2007 anaidanganya mahakama chini ya kiapo
Lissu anamsomea hukumu ya kesi anayoitumia kama rejea.
Shahidi anakataa sio yeye anasema Amini huyo anayetajwa ni mtu mwingine.
Lissu: Tuendelee.. unasema kama kazi ya kitengo X ni kushughulikia usalama wa nchi, waeleze majaji kama ulimshirikisha Regional Security Officer
Shahidi: Hapana
Lissu: Waeleze majaji kama uliwashirikisha TIS.
Shahidi: Sikuwashirikisha
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kitu kinaitwa Kamati ya Ulinzi na Usalama na. kama uliijulisha kamati hiyo ya mkoa wa Dar es salaam....
Lissu amuhoji shahidi kama alipewa jina la mwanachadema yeyote aliyekua hatarini kwa vitisho
Lissu: Waeleze majaji kama uliwasilisha hiyo barua
Shahidi: Ipo
Lissu: Ipo Mahakamani
Jajji: Shahdi embu jibu kama umeleta au hujaleta mawakili wa serikali watakuuliza baadae pia
Lissu: Kwa hiyo jibu ni lipi
Shahidi: Sijaleta
Lissu: Nataka maswali yangu yajibiwe kwemye ushahidi wako, jana ulisema hivi baada ya kaungalia hiyo video uliona kwamba mtuhumiwa alidhihirisha nia yake kwa kuchapisha kwa umma, kwa kuchapisha kwemye Jambo TV. Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yako
Shahidi: Hayapo
Lissu: Shahidi kwenye ushahidi wako kuhusu tuhuma ulisema, uchaguzi mkuu uko kwa mujibu wa Katiba na mlinzi mkuu wa Katiba ni serikali. Umewahi kusoma Katiba?
Shahidi: Kipindi cha nyuma
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimsomee Katiba, Ibara ya 26 - "Kila mtu ana wajibu wa kulinda na kuzifuata na sheria za nchi hii, wewe umesema ni serikali
Shahidi:.......
Lissu: Ulisema kulikuwa na mipango ya kuvuruga uchaguzi kwa kutumia mbinu mbalimbali, ikiwemo kupiga watu mawe na mengineyo, waeleze majaji kama hayo maneno yako kwenye maelezo yako
Shahidi: Hayapo
Lissu: Jana ulisema hivi, hiyo video mliyoiangalia iliwekwa kwenye 'memori kadi' ikafikishwa kwenye maabara ya uchunguzi wa kisayansi ili kuithibitisha, sasa waeleze majaji kama hayo yapo kwemye maelezo yako
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kwa kuwa wewe ni shahidi wa 16 na wengine 15 waliopita hawakuwasilisha video Mahakamani naomba waeleze majaji kama umewasilisha hiyo video
Shahidi: Hapana
Lissu: Kwakuwa wewe ni shahidi wa 16 na hakuna aliyewasilisha ripoti ya kubaini uhalisia wa hizo video, waeleze majaji kama umewasilisha hiyo ripoti ya uchunguzi
Shahidi: Hapana
Lissu: Unasema ulimuelekeza Inspekta Michael kuchukua vielelezo pamoja na ripoti ya uchunguzi na kukabidhiwa kwa mtunza nyaraka. Je, hayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Baada ya kufanya yote ambayo mlikua mmeshafanya uliwasiliana na Ma RCO nchi nzima, hiyo ipo sitakuuliza, sasa kwenye maelezo yako jana umetaja majalada ya uchunguzi toka mikoa mbalimbali; Ruvuma, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam. Mimi nakuuliza juu ya jalada la Dar es Salaam, toka ofisi ya ZCO ambalo namba zake ni….. waeleze majaji kama lipo kwenye maelezo yako.
Shahdii: Hayapo
Lissu: Jana ulisema mtuhumiwa alikamatwa Mbinga na kusafirishwa usiku huo huo mpaka Dar es Salaam, Kituo Kikuu cha Kati na kufikishwa ofisi ya Deputy ZCO. Waeleze majaji kama hapo maelezo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Ulieleza pia jinsi ulivyopeleka jalada ofisi ya DPP na baadae jalada kurejeshwa kwenu kuendelea na upelelezi, waeleze majaji kama hicho kipande kipo
Shahidi: Hakipo
Lissu: Unasema mlipata taarifa mashahidi kutishiwa, je kwemye maelezo yapo?
Shahdi: Hayapo
Lissu: Unasema mliwasiliana na ofisi ya DPP ili kuweza kuwapatia ulinzi mashahidi, Je yapo?
Shahdi: Yapo
Lissu: Unasema mliomba kwa barua sema kama yapo
Shahidi: hayapo
Lissu: Unasema ulikula kiapo ili kuwaombea ushahidi, Je yapo?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Hayo ni kutoka kwenye ushahidi wako jana sasa twende kwingine, umewaeleza majaji kwamba umesoma hiyo hati ya kiapo?
Shahidi: Ndio
Lissu: Waeleze majaji kwenye hati hii uliyosaini kama ulitaja jina la shahidi yeyote
Shahdi: Hapana
Lissu: Waleze majaji kama ulipewa jina la mwanachadema yeoyote aliyekua hatarini kwa vitisho
Shahidi: Hapana
Lissu: Waleze majaji kama ulitaja mwanachama yeyote alikua akitoa vitisho hivyo
Shahidi: Hapana
Lissu: Waleze majaji kama ulitaja siku au mahali
Shahidi: Hapana
Lissu: Waeleze majaji kama ulitaja aina ya vitisho
Shahidi: Ndio nilitaja
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimuoneshe shahidi kiapo chake
Inaendelea..............
Lissu: Unataka na Mawakili wakae hapo na wao niwakaange?
Lissu: Umeeleza kwamba ulipofika
kwa Deputy ZCO, George Pademi baada ya kutambulishwa timu, uliwapangia majukumu
na ulikuwa na timu tatu. Waeleze majaji
hawa watu uliowataja jana kama wako kwenye maelezo yako uliyoandika mwaka jana
Shahidi: Hayapo
Lissu: Nyongeza nyongeza.
Pia ulieleza ulikuwa na timu ya
watu uliowataja jana pia kama wako kwemye maelezo yako
Shahidi: Hayapo
Lissu: Pia ulieleza ulikuwa na
timu ya tatu ya Legal and Advisory, unataka kuonyesha mlifuata sheria, unasema
ulikuwa na mtu ambaye jina lake hukumbuki alikuwa na jina la kibantu alitoka
ofisi ya DPP Dodoma, je waeleze majaji kama hayo maelezo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Tubaki hapo nilimuuliza shahidi
wa kwanza George Bajemu alisema hakukuwa na mwanasheria kwenye timu yenu, je
tumuamini nani
Shahidi: Kulikua na mwanasheria
Lissu: Basi tukuamini wewe George
ni liongo
Lissu: Unasema mkiwa ofisini kwa
kutumia kompyuta mlitazama hiyo video Jambo TV kwa saa mbili na usheee mkiwa
timu nzima waambie majaji kama yapo hayo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Hapo hapo, Shahidi wa
kwanza, George Bajemu aliambia Mahakama alioneshwa vipande vipande na Kaaya
wewe unasema mlitazama mkiwa na timu nzima tumuamini nani
Shahidi: …. Kabla hajajibu….
Wakili wa serikali anakatisha
kidogo na kuomba kwamba Ushahidi wa Bajemi ulikua wa tarehe nne na huyu
anaongelea ushahidi wa kuanzia tarehe 8 naomba wafuate rekodi sawa sawa
Lissu: Waheshimiwa majaji hawa
mawakili wa serikali si wana haki ya re-examination watauliza kwa wakati wao,
wako nane wanaanzaje kunifundisha mimi kufanya dodoso wasubiri zamu yao
Kimya kidogo Majaji wanaongea……
Jaji anatoa ufafanuzi waendeleee ila kwa kufuata taratibu
Lissu: Narudia swali langu George Bajem anasema mliona video vipande vipande wewe unasema mlitamza yote Majaji wa amini kipi
Shahidi: George yeye na Kaaya walitazama vipande vipande na mimi baadae baada ya kuteuliwa ndio tulikaa tukatazama kama timu kwemye kompyuta maalumu
Lissu: Waheshimiwa majaji maelezo ya George Bajem yako kwenye 'information' na niliyafanyia dodoso kwa kina na hayakuwa 'tendered' ila yako kwenye rekodi za Mahakama na nina haki ya kumuuliza shahidi kwa kutumia maelezo haya
Shahidi: Hayo sio maelezo yangu hiyo ni rekodi ya Mahakama siyajui
Lissu: Haya ndio maelezo mliyokusanya ninyi Jeshi la polisi na mkayaleta unasema hujui
Shahidi: Maelezo ya George ni ya tarehe 4 na yangu ni tarehe nane
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi asome maelezo yake yote kuanzia mwanzo
Shahidi: Anasoma maelezo yake…….
Lissu: Mpaka hapo kuna mahali mmeangalia video?
Shahidi: Hapana
Lissu: Tuendeleee, kwenye maelezo yako ya jana umesema ulipotazama hiyo video ulimuona mtuhumiwa Lissu na nyuma kulikuwa na bendera ya taifa na Chadema waeleze majaji kama hayo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kwenye maelezo yako ulisema Lissu alikua akihutubia umma wa watanzania waambie majaji kama hayo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kwenye ushahidi wako ulisema kwamba mliwasiliana na Idara ya Uhamiaji ambayo iliwathibitishia Lissu ni Raia wa Tanzania je hayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Waeleze majaji kama umewasilisha Mahakamani barua kama uliwasiliana Idara ya uhamiaji
Shahidi: Barua zipo
Lissu: Umewasilisha Mahakamani?
Shahidi: Kimya.....
Lissu: Unataka na mawakili wakae hapo na wao ni wakaange?
Itaendelea…..
"Je una akili timamu bwana afande?" - Lissu
Lissu anaendelea kumdodosa Shahidi wa 16 wa Jamhuri, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Amin Mahamba aliyeanza naye jana:
Lissu: -Shahidi habari yako
ulilala vizuri?
Shahiri: Salama Ahsante
Lissu: Sasa jana nilikua nakupitisha
kwenye maelezo yako uliyotoa kizimbani naomba leo ukijibu utoe sauti kikakamavu
kama askari anayeweza kuendesha gwaride.
Lissu: Waeleze majaji kama mwaka
2014 uliteuliwa kuwa OCCID Kyela waeleze majaji kama ipo?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Waelezema majaji kama (maelezo
ya) ulifanya kazi Kyela kama OCCID kwa miaka miwili na baadae ukahamishiwa
Ruvuma
Shahidi: Hayapo
Lissu: Na ulikuwa RCO wa mkoa wa
ruvuma kwa miaka mitano
Shahidi - Hayapo
Lissu: January 2023 ulihamishiwa
Dar kama Naibu ZCO kanda maalumu waeleze majaji kama hayo maelezo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Ukiwa Deputy ZCO ulikua unasinamia
wapelelezi wote wa Kanda maalumu
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kama RCO Kinondoni ulikuwa
mkuu wa wapelelezi wote wa mkoa wa kipolisi Kinondoni waambie majaji kama hayo maelezo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Mwezi Mei 2024 ukahamishwa
na kupelekwa kwenye kitengo X ambapo upo mpaka leo waeleze majaji kama ipo
kwenye maelezo yako
Shahidi - Hayapo
Lissu: Sasa shahidi kwenye
ushahidi wako wa jana ulisema hivi tarehe 8/04/2025 nikiwa ofisini kwangu masaa
ya mchana nilipigiwa simu na mkuu wangu wa kazi DCP Nganzi kwenye ofisi za ZCO
Dar es Salaam, ili kwenda kuratibu na kusimamia upelelezi dhidi ya mtuhumiwa
Tundu Lissu, waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yako kilelezo
namba D15
Shahidi: Yapo
Lissu: Waeleze majaji kama kuna
sehemu inamhusu mtuhumiwa Tundu lissu
Shahidi: Yapo
Lissu: Isome tena , Lissu
anamsomea tena
Na anamuuliza: Je kwenye maneno
uliyasema jana kuna majina Tundu Lissu
Shahidi: Yapo
Lissu: Je una akili timamu bwana
afande? kuna jina Tundu Lissu
Shahidi: Yapo
Lissu: Ndio maana nasema
unajifanya mjanja huna lolote afande mpelelezi mbobevu
Lissu: Ulisema jana ulipofika
ulipoitwa uliona jalada mezani ambalo lilimtaja mtuhumiwa Tundu Lissu
Shahidi: Yapo
Lissu: Kwenye karatasi yapo
Shahidi: Hayapo
INAENDELEA...........
Picha kutoka Mahakamani
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Lissu awasili Mahakama Kuu
Chanzo cha picha, Getty Images
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amewasili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili.
Lissu anatarajiwa kuendelea kumuhoji shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka, Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, katika hatua ya 'cross-examination'.
Jana, Mahamba alimaliza kutoa ushahidi wake wa msingi baada ya kueleza kuhusu upelelezi wa kesi hiyo, ikiwemo video ya hotuba ya Lissu na madai ya polisi kuhusu kauli zake za kuzuia uchaguzi. Lissu alianza kumuhoji shahidi huyo jana na leo punde anatarajiwa kuendelea na maswali yake.
Lissu alivyoanza kumuhoji shahidi
Baada ya Mahamba kumaliza ushahidi wake wa msingi, Lissu alianza kumuhoji katika hatua ya cross-examination.
Lissu alimuuliza kama anajiona kuwa afisa mpelelezi mwenye uzoefu mkubwa.
Shahidi: "Ni kweli."
Lissu kisha akamuuliza kama alipanda cheo kwa kutungia watu kesi za uongo, kutesa watuhumiwa au kukosa uadilifu.
Shahidi: "Sio kweli."
Lissu pia alidai kuwa shahidi na timu yake walishirikiana na wahalifu waliofanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka jana.
Shahidi: "Sio kweli."
Lissu aibua tofauti kati ya ushahidi na maelezo ya shahidi
Lissu alimwomba shahidi kueleza kama baadhi ya taarifa alizozitoa mahakamani zilikuwepo kwenye maelezo yake ya awali.
Katika maswali kadhaa, shahidi alijibu:
"Hayapo."
Miongoni mwa mambo hayo ni maelezo kuhusu mafunzo yake ya polisi, kituo chake cha kwanza cha kazi, mafunzo maalumu aliyodai kuyapata mwaka 2006, kuwa mkufunzi na baadhi ya majukumu aliyowahi kufanya.
Maelezo ya shahidi yapokelewa kama kielelezo D15
Baada ya mabishano mafupi kati ya Lissu na upande wa mashtaka kuhusu utaratibu wa kutumia maelezo hayo, mahakama iliruhusu yaendelee kutumika.
Maelezo hayo yalipokelewa na mahakama kama kielelezo D15.
Baadaye Jaji Dunstan Ndunguru aliahirisha kesi hadi leo saa tatu asubuhi.
Kesi inaendelea leo na Lissu anatarajiwa kuendelea kumuhoji shahidi katika hatua ya kumuuliza maswali shahidi kupima uamini na kuonyesha migongano (cross-examination)
Shahidi: "Baadhi ya watu walihamasika na kauli za Lissu"
Mahamba pia alieleza kuwa katika upelelezi wao walipokea majalada kutoka mikoa mbalimbali, yakiwemo Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Ruvuma.
Alisema baada ya kuyasoma, walibaini baadhi ya watu waliokuwa kwenye majalada hayo walikuwa wamehamasika na kauli za Lissu, na akaelekeza watafutwe na waandikwe maelezo kama mashahidi katika kesi hiyo.
Shahidi azungumzia pia kukamatwa kwa Lissu
Mahamba alisema Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025, akiwa Mbinga mkoani Ruvuma, na kusafirishwa hadi Dar es Salaam siku hiyo hiyo.
Alisema Lissu alifika Dar es Salaam Aprili 10 na kufikishwa kituo cha polisi, ambako alisomewa tuhuma lakini hakutoa maelezo, akisema atayatoa mahakamani.
Baadaye, alisema, Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka.
Shahidi azungumzia pia vitisho kwa mashahidi
Mahamba pia alidai kuwa wakati upelelezi ukiendelea, baadhi ya mashahidi waliripoti kutishiwa iwapo wangetoa ushahidi dhidi ya Lissu.
Alisema polisi walichunguza ujumbe na maoni kwenye mitandao ya Facebook, TikTok, Instagram na X, na baadaye kuwasiliana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuhusu usalama wa mashahidi hao.
Alisema hatua zilichukuliwa ili baadhi ya mashahidi hao walindwe.