Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je wanawake wajawazito watapokea chanjo ya Covid-19 ? Inategemea
Huku chanjo dhidi ya virusi vya iliyosubiriwa kwa muda mrefu ikianza kutolewa ni wazi kwamba sio kila mtu anayeweza kuipata. Kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha , upatikanaji huu unategemea na ni wapo wanapoishi.
Majaribio ya kimatibabu kwa ajili ya chanjo ya Pfizer BioNTech hayakujumuisha wanawake wajawazito wala wanaonyonyesha, na kampuni hiyo inasema data zilizopo kwa sasa "hazitoshi" kubaini hatari zozote zinazoweza kusababishwa na chanjo hiyo kwa mimba.
Nchini Uingereza ukosefu huu wa data uliwafanya wadhibiti wa chanjo kuwaondoa wanawake wajawzito na wanaonyonyesha katika mipango ya chanjo. nchini marekani, uamuzi umeachwa kwa wanawake wenyewe kuamua iwapo watachnjwa au la.
Hizi ndio sababu zilizozigawanya nchi hizo, kile inachomaanisha kwa wanawake wajawazito.
Data zinasemaje?
Hadi sasa, hazielezei mengi
" Hapakuwa na data , hilo ndio kweli ," anasema Dkt Ruth Faden, mtaalamu wa maadili ya kibaiolojia katika chuo kikuu cha Johns Hopkins University, ambaye anahusika na haki na afya za wanawake wajawazito. Hakuna taarifa kuwa hususa juu ya hatari kwa wanawake wenye mimba na wanawakewanaonyonyesha, hakuna bado taarifa za kutosha kusema ukweli.
Pfizer imesema kuwa ilifuata muongozo wa Taasisi ya utoaji wa Cahakula na dawa katika kuwaondoa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha katika majaribioya kimatibabu. Wanawake hawa hawatajumuishwa katika majariobio ya tiba hadi kampuni itakapokamilisha kile kinachoitwa stadi za Dart (ukuaji na sumu ya uzazi ), ambazo mara nyingi hufanyika katika wanyama.
Wataalamu wanasema hili ni jambo la kawaida.
"Katika nyakati ambazo sio za janga, kama unazungumzia kuhusu nembo mpya ya chanjo, watu wanaofikiria vyema wanaojitolea kuendeleza maslahi ya wanawake wajawazito na vizazi vyao wangependa bado kuhusisha wanawake wajawazito "katika majaribio ya awali ya matibab, anasema Dkt Faden . "Huwezi kuwakweka kuanzia mwanzo ".
Katika maadili ya kibaiolojia , wanawake walielezewa kama "watu wagumu", Dkt Faden alisema. " Hakuna mahali ambapo unakuwa na vyombo viwili kwa wakati mmoja, vyote ambavyo ni vifaa vya hofu ya kimaadili ."
" Na kwa ukubwa, hakuna mtu anayejali zadi juu ya hali ya kizazi kuliko mwanamke mjamzito. Swali la kwanza ambalo kwa kawaida unalipata ni 'je hii itakuwa salama kwa mtoto wangu mchanga?'" alisema.
lakini uamuzi wa kuwaacha nje ya majaribio ya tiba katika kliniki wanawake wajawazito ni gumu zaidi wakati wa janga.
"Tuko mahala pagumu," alisema Dkt Emily Stinnett Miller, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika Chuo Kikuu cha Northwestern ambaye pia ni mjumbe wa Kikosi kazi cha Covid-19 cha tiba ya wanawake wajawazito na vijusi . " Wanatakiwa kuchukua uamuzi muhimu na wa haraka na kuna faida na hasara za kuwajumuisha na kuwatenga ." wanawake wajawazito.
Hasara kubwa -ukosefu wa data-ni dhahiri sasa. "Hatuna data kusema kwelikuweza kuchukua maamuzi ya kimatibabu ambayo tunahitaji kufanya ," alisema.
Ni kwanini Uingereza na Marekani wanatofautiana ?
Wakikabiliwa na tatizo linalofanana la ukosefu wa data, Marekani na Uingereza wamegawanyika katika sera yao ya kushughulikia suala hilo.
" Wakati unapokuwa hauna data ambazo zinaelezea hasa kuhusu swali, basi swali linalofuata na kutulia na kusema 'SAWA, ni nini kitu kingine tunachokifahamu,?'" Dkt Faden alisema.
Uingereza imechukua mkono makini zaidi . Katika wavuti wake , Wizara ya afya ya umma ya nchi hiyo ilisema wakati ushahidi "hauoneshi wasi wasi kwa usalama wa mimba ", shirika "linataka kuona data nyingine zisizo za kimatibabu " kabla ya kukamilisha ushauri wake kwa wanawake wajawazito.
" Kama majaribio ya kipekee ya chanjo za Covid-19 miongoni mwa wanawake hayajafanyika, hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwashauri wanawake wajawazito na wanaonyonyesha kupata chanjo za Covid-19 ," alisema Dkt Edward Morris, rais wamadaktari bingwa wa wanawake katika Royal College (RCOG), katika taarifa.
Wataalamu nchini US walichukua mkondo mwingine, wakaacha uamuzi wa chanjo kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.
"Wataalamu walifikia makubaliano ya pamoja ya mtazamo kuwa hapakuwa na ushahidi wa kisayansi wa madhara ," Dkt Faden alisema. Lakini akatahadharisha, "kwamba hii haimaanishi kuwa hakuna madhara kabisa".
Majaribio ya chanjo ya Covid huenda yalifanyika kwa kasi kubwa, lakini hayakuvuka hatua yoyote , wasimamizi wa viwango wa Marekani na Uingereza alisema, na uidhinishaji hutolewa tu wakati chanjo inapokuwa salama na yenye ufanisi.
Hii inawaacha wapi wanawake ?
Katika nchi zote, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha watatakiwa kusubiri taarifa zaidi kabla ya kupata ushahidi zaidi kuhusu chanjo.
Matokeo ya awali kutoka katika kampuni ya Pfizer kuhusiana na tafiti za sumu za ukuaji zinatarajiwa mwishoni mwa mwaka huu . Pale tafiti zitakapokamilika, kampuni hiyo inaweza kupanua majaribio yake ya tiba kujumuisha wanawake wajawazito . Pia kuna wanawake wachache ambao walipata ujauzito huku wakifanyiwa majaribio ambao wataendelea kuchunguzwa katika kipindi chao cha ujauzito.
Joanna Sullivan, 35, ambaye anaishi kusini magharibi mwa Ohio, anatarajia mtoto wake wa kwanza mwezi Juni. Hapangi kupata chanjo hadi pale atakapojifungua.
"Sijui ni matatizo ya aina gani unayoweza kuyapata, na kwakuwa ni mtoto wangu wa kwanza, kwa kuwa nina umri mkubwa, kuna uwezekano wa hatari ya hali ya juu ," alisema. Na ingawa inaweza kuwa "usaidizi " anaona ni heri aone jinsi wanawake wengine wajawazito watakavyokuwa watakapopewa dawa hiyo , Bibi Sullivan alisema anaweza kusubiri.