Virusi vya corona: Chanjo ya Oxford ilivyowezesha mfumo wa kinga mwilini kukabiliana na virusi

Iliyochapishwa

Chanjo ya virusi vya corona iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza imeonekana kuwa ni salama na inachochea mfumo wa kinga ya mwili kukabiliana na virusi.

Majaribio ya chanjo hiyo yaliyowahusishwa watu 1,077 yameonyesha kuwa sindano ya chanjo hiyo waliyopigwa iliwezesha kutengeneza seli za protini za kinga ya mwili pamoja na seli nyeupe za damu zinazoratibu mfumo wa kinga ya mwili zenye uwezo wa kupambana na virusi vya corona, zinazofahamika kama T-cells.

Matokeo yanatia matumaini makubwa, lakini bado ni mapema sana kufahamu kama nana hii inatosha kuulinda mwili na majaribio makubwa yanaendelea.

Uingereza tayari imeagiza dozi milioni 100 za chanjo.

Je chanjo hii inafanya kazi vipi?

Chanjo -inayofahamika kama ChAdOx1 nCoV-19 - inatengenezwa kwa kasi ambayo haikutarajiwa.

Inatengenezwa kutoka kwa virusi vilivyobuniwa ambavyo kwa kawaida husababisha homa ya kawaida ya mafua kwa sokwe.

Vilifanyiwa mabadiliko makubwa , kwanza ili viweze kusababisha maambukizi kwa binadamu na pia kuvifanya "vionekane " zaidi kama virusi vya corona

Wanasayansi walifanyikiwa kufanya hivyo kwa kuhamisha taarifa za jeni kwa ''protini ya virusi vya corona inayochipuka " - ambayo kutumiwa na virusi hivyo kuvamia seli zetu - kwa chanjo waliyokuwa wakiitengeneza.

Hii inamaanisha kwamba chanjo inafanana na virusi vya corona na mfumo wa kinga ya mwilina inaweza kujifunza kushambulia kirusi.

Je antibodies na T-cells ni nini?

Katika kukabiliana na virusi vya corona lengo kuu limekuwa ni kuhusu antibodies, (seli za protini za kinga ya mwili) lakini hii ni sehemu moja tu ya kinga ya ulinzi wa mwili wetu.

Antibodies ni seli ndogo za protini ambazo hutengenezwa na mfumo wa kinga ambazo huganda kwenye virusi.

T-cells, ni aina ya seli nyeupe, husaidia kuratibu mfumo wa kinga ya mwili na zina uwezo wa kubaini ni seli zipi za mwili zina maambukizi na kuziangamiza.

Karibu chanjo zote zenye ufanisi huwa zina antibodies na T-cell kwa pamoja.

Viwango vya T-cells viliongezeka siku 14 baada ya chanjo na viwango vya seli za protini zikaongezeka baada ya siku 28. Utafiti haujaendeshwa kwa muda mrefu wa kutosha kuelewa ni kwa muda gani chanjo hiyo inaweza kudumu, utafiti katika jarida la Lancet ulionyesha.

Profesa Andrew Pollard, kutika kikundi cha utafiti cha Oxford aliiambia BBC kwamba: "Tumefurahishwa kwa kweli na matokeo yaliyochapishwa walikua wakishuhudia kudhoofishwa kwa antibodies na T-cells kwa pamoja.

"Matokeo yalikuwa yanatia matumaini makubwa na tunaamini matokeo yatakayopatikana yatakuwa ni ya kinga.

"Lakini swali muhimu ambalo kila mtu anataka kujua ni je chanjo inafanya kazi, je inatoa kinga…na tunasubiri ."

Utafiti unaonyesha kwamba 90ya watu hutengeneza kinga ya mwili baada ya kupata dozi ya kwanza. Ni watu kumi pekee waliopewa dozi mbili na wote walitengeneza kinga ya mwili

"Hatufahamu ni kiwango kipi kinahitajika kwa ajili ya kinga, lakini tunaweza kuwa na uhakika kwa kutoa dozi ya pili ," Prof Pollard taliiambia BBC.

Je ni salama?

Hapakuwa na athari za hatari kutokana na chanjo, hata hivyo 70% ya watu waliofanyiwa majaribio walipata homa au maumivu ya kichwa.

Watafiti wanasema athari hizi zinaweza kutibiwa kwa tembe za paracetamol.

Profesa Sarah Gilbert, kutoka Chuo kikuu cha Oxford, nchini Uingereza anasema : " Bado kuna kazi kubwa ya kuhfanya kabla ya kuthibitisha kuwa chanjo yetu itasaidia kutibu janga la Covid-19 , lakini matokeo haya ya awali yanaleta matumani ."

Ni hatua gani zinazofuata katika jaribio la chanjo hii ?

Matokeo hadi sasa ni ya matumaini, lakini lengo lao kuu ni kuhakikisha chanjo ni salama vya kutosha kuwapatia watu.

Utafiti hauwezi kuoneshwa iwapo chanjo inaweza kuwazuia watu kuugua au kupunguza dalili zao za Covid-19.

Zaidi ya watu 10,000 watashiriki katika awamu ijayo za tmajaribio nchini Uingereza.

Hatahivyo, jaribio hili pia limepanuliwa katika nchi nyingine kwasababu viwango vya virusi vya corona viko chini nchini Uingereza, na hivyo kuwa vigumu kufahamu iwapo chanjo ina ufanisi.

Kutakuwa na jarijbio kubwa la chanjo litakalowashirikishwa 30,000 nchini Marekani pamoja na watu 2,000 nchini Afrika Kusini na 5,000 kutoka Brazil.

Pia kuna miito ya "kutathmini chanjo " ambapo watu waliochanjwa wanadungwa tena makusudi virusi vya corona. Hatahivyo, kuna hofu ya kimaadili kutokana na ukosefu wa tiba.

Nitapata lini chanjo ?

Inawezekana chanjo ya virusi vya corona itathibitishwa kuwa yenye ufanisi kabla ya mwisho wa mwaka huu, hatahivyo, haitapatikana miongoni mwa watu wengi.

Wahudumu wa afya watapewa kipaumbele kama watu wanaokabiliwa na hatari ya kupata maambukizi ya Covid-19 kutokana na umri wao au hali yao ya kimatibabu.

Hatahivyo, huenda dawa hiyo ikasambazwa, kuanzia mwanzoni mwa mwaka ujao kama kila kitu kitakwennda kama kilivyopangwa.

Je ni maendeleo gani yaliyopatika kuhusu chanjo nyingine?

Chanjo ya Oxford sio ya kwanza kufikia kiwango hijki, kwani kuna makundi ya watafiti kutoka Uchina na Marekani ambayo pia yanachapisha matokeo sawa ya utafiti wao wa chanjo.

Kampuni ya Marekani ya Moderna ilikuwa ya kwanza kutangaza matokeo yake na chanjo yake inaweza kkuharibu antibodies. Wanachoma sindano ya virusi vya corona s RNA (alama yake ya jeni), ambayo hatimae inaanza kutengeneza protini za virusi ili kuchochea uwezo wa kinga ya mwili.

Kampuni za BioNte na Pfizer pia zina matokeo chanya ya matumizi ya chanjo yao ya RNA.