Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Obama ampigia simu Trump kumpongeza

Mgombea wa Republican Donald Trump amemshinda Hillary Clinton wa Democratic katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Moja kwa moja

  1. Tim Kaine ahimiza Wamarekani wajitokeze kwa wingi

    Mgombea mwenza wa chama cha Democratic Tim Kaine amepiga kura yake jimbo la Virginia na akawahimiza Wamarekani pia wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Amesema: "Jitokezeni tu na mshiriki."

    Hillary Clinton ametoa ujumbe sawa kupitia Twitter:

  2. Mgombea mwenza wa Clinton kituoni kupiga kura

     Mgombea mwenza wa Bi Clinton, Tim Kaine, amefika katika kituo cha kupigia kura Virginia kupiga kura yake kwa mujibu wa mwandishi huyu wa Fox News:  

  3. Tunafahamu nini kutokana na kura za mapema?

    Upigaji wa kura mapema ulifanyika katika majimbo mengi nchini Marekani na kufikia sasa inakadiriwa kwamba Wamarekani 46 milioni tayari wamepiga kura.

    Ingawa kura hizi zitahesabiwa baada ya vituo kufungwa Jumanne, baadhi ya majimbo huta takwimu na maelezo kuhusu waliopiga kura kwa mfano kuhusu idadi ya waliopiga kura na iwapo wamejiandikisha kuwa wa chama cha Republican au Democratic.

    Jimbo la Nevada, kwa mfano, tunajua kwamba karibu watu 800,000 walipiga kura kabla ya kufungwa kwa upigaji wa kura za mapema tarehe 4 Novemba.

    Asilimia 42 walikuwa wanachama wa Democratic na 36% wanachama wa Republican. Takwimu hizo hazina tofauti kubwa na hali 2012, ambapo Barack Obama aliongoza kwa 6.7%.

  4. Mambo muhimu kuhusu uchaguzi mkuu Marekani

    Siku ya uchaguzi, mshindi si lazima awe yule anayepata kura nyingi kwa jumla. Kuna majimbo 50 na Washington D.C. Kila jimbo huwa na 'Kura za Wajumbe' kwa kutegemea sana wingi wa watu. Tazama video hii kupata mambo muhimu kuhusu uchaguzi wa urais Marekani. 

  5. Kampeni za dakika za mwisho

    Hillary Clinton na Donald Trump wamefanya mikutano ya dakika za mwisho mwisho kuwahimiza raia wa Marekani wawapigie kura zikiwa zimesalia saa chache kabla ya uchaguzi kufanyika.  

    Huu hapa ni muhtasari wa matukio makuu ya siku ya mwisho ya kampeni.

    • Donald Trump na Hillary Clinton walifanya mikutano ya kampeni ya mwisho majimbo yanayoshindaniwa
    • Clinton amewahimiza wapiga kura kuunga mkono Marekani “inayowajumuisha wote”
    • Bw Trump naye amewaambia wafuasi wake kwamba wana "fursa nzuri ya kuvunja mfumo mbovu na usio na maadili".
    • Utathmini wa kura za maoni wa BBC unaonesha Clinton yupo mbele kwa alama nne: Clinton ana 48% na Trump ana 44%
    • Takriban Wamarekani 44.9 milioni walipiga kura mapema. Hii huenda ikawa 40% ya kura zote
    • Kuna dalili kwamba wapiga kura wa asili ya Hispania (Kilatino/Mexico) wamejitokeza kwa wingi, habari njema kwa Clinton
    • Mkuu wa kampeni wa Trump Kellyanne Conway ameondolea mbali wasiwasi wa jamii ya kimataifa kumhusu Trump, akihojiwa na BBC.
  6. Hujambo!

    Karibu kwa taarifa maalum za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu nchini Marekani. Wagombea wawili wakuu ni Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democratic.