Habari za hivi punde, Trump: Asanteni sana
Trump amepanda jukwaani Manhattan, New York. Amewashukuru wafuasi wake na kusema amepigiwa simu na Hillary Clinton "kuwapongeza".
Aidha, amesema mwenyewe amempongeza Bi Clinton.
"Hillary amefanya kazi kwa bidii sana na kwa muda mrefu sana na twafaa kumshukuru kwa alivyoitumikia nchi yetu," Bw Trump amesema.
"Sasa ni wakati wa Marekani kuponya vidonda vya mgawanyiko."