Habari za hivi punde, Trump mshindi jimbo la Arkansas
Trump anakadiriwa kushinda jimbo la Arkansas kwa mujibu wa ABC News. Jimbo hilo lina kura sita za wajumbe.
Kwa kura za wajumbe, sasa Trump ana 129 na Clinton 97.
Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mgombea wa Republican Donald Trump amemshinda Hillary Clinton wa Democratic katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.
Trump anakadiriwa kushinda jimbo la Arkansas kwa mujibu wa ABC News. Jimbo hilo lina kura sita za wajumbe.
Kwa kura za wajumbe, sasa Trump ana 129 na Clinton 97.
ABC News wamekadiria kwamba Clinton atashinda kwenye jimbo lake la New York, lakini Trump anashinda Texas, Kansas, North Dakota, South Dakota na Wyoming.
Trump ameshinda pia Nebraska, na kupata kura 4 kati ya 5 za wajumbe katika jimbo hilo. Majimbo hayo hata hivyo hayatazamwi kama majimbo yanayoshindaniwa.
Donald Trump anaonekana kuwa mbele kidogo kwa sasa jimbo muhimu la Florida.
Hata hivyo, maeneo mengi matokeo hayajajulikana, baadhi yakiwa ngome za chama cha Democratic.
Jimbo hilo lina kura 29 za wajumbe na ni muhimu sana kwa mgombea yeyote.
Jimbo hilo lilimpigia Obama mwaka 2008 na 2012 (Democratic), lakini George W Bush (Republican) alishinda uchaguzi uliotangulia 2000 na 2004. Jambo la kushangaza ni kuwa alikuwa mbele na kura 537 pekee mwaka 2000. Hata hivyo, ilichukua siku 36 kwake kuthibitishwa kuwa mshindi, kwa hivyo iwapo wagombea watakaribiana sana usitarajie matokeo yatangazwe haraka.
Iwapo Trump atashindwa Florida na Ohio, matumaini yake ya kushinda urais yatakuwa finyu.
Marco Rubio ,mgombea ambaye wakati mmoja alitarajiwa kushinda tiketi ya urais ya chama cha Republican ameshinda wadhfa wa Useneta huko Florida.
Rubio mwenye umri wa miaka 45 alitarajiwa kujiunga na sekta ya kibinafsi baada ya kupoteza uteuzi huo kwa Donald Trump lakini akabadili uamuzi wake na sasa atakuwa seneta wa jimbo hilo.
Maafisa wa polisi katika mji wa Azusa jimbo la California wanasema kuwa kuna hali ya 'mshikemshike' katika nyumba moja karibu na kituo cha kupiga kura inayohusisha mwanamke aliyejihami na bunduki.
Polisi wamepelekwa katika eneo hilo na kushambuliwa na mtu huyo huku wakijaribu kubaini iwapo kuna mtu mwengine ambaya hajakamatwa.
Mtu mmoja ameuawa huku wengine watatu wakijeruhiwa.
Polisi wanasema kuwa ni mapema mno kubani lengo la mtu aliyefyatua risasi,lakini wanaamini kwamba tukio hilo linaaminika kuwa katika eneo hilo jirani mashariki mwa Los Angeles.
Maeneo mengi Marekani yatasubiri vituo vifungwe- sana kati ya 19:00 EST (24:00 GMT - Saa tisa usiku Afrika Mashariki) na 20:00 EST (01:00 GMT - Saa kumi usiku Afrika Mashariki) - kuanza kupokea matokeo na makadirio ya matokeo katika majimbo mbalimbali.
Vituo vya kura vitafungwa katika jimbo lenye umuhimu mkubwa uchaguzini kutokana na wingi wa wajumbe, California (55), ambayo ni ngome ya Democratic, pamoja na Oregon (7), Washington (12), Idaho (4) na Hawaii (4).
Kwa kutegemea hali itakavyokuwa, mshindi anatarajiwa kutangazwa wakati huu.
Kwa kufuata desturi, atakayeshindwa anatarajiwa kutoa hotuba ya kukubali kushindwa muda mfupi baadaye.
Soma zaidi hapa: Mwongozo wa matukio makuu uchaguzi Marekani
ABC News wanakadiria kwamba Trump ameshinda jimbo la Alabama. Hilo linamuongezea kura 9 za wajumbe.
Makadirio ya ABC News yanaonesha Trump atashinda Tennessee (kura 11) na South Carolina (kura 9 za wajumbe).
Kwa jumla sasa Clinton ana kura 68 za wajumbe na Trump kura 57.
Kufikia sasa, makadirio yanaonesha Clinton ana kura 68 za wajumbe na Trump kura 37.
ABC News wanakadiria Clinton atashinda majimbo ya New Jersey, District of Columbia, Massachusetts, Maryland, Delaware, Illinois na Rhode Island.
Trump anakadiriwa kushinda Mississippi na Oklahoma.
Jimbo linalogombaniwa na wagombea wawili wa urais nchini Marekani la Carolina kaskazini limeongeza muda wa kupiga kura katika kaunti nane za Durham kufuatia matatizo ya mfumo wake wa kupigia kura mapema Jumanne.
Kaunti hiyo ni ngome ya chama cha Democrat kutokana na idadi kubwa ya Wamarekani weusi ambao wameunga mkono chama hicho.
Mapema ,chama cha Republican katika jimbo hilo kilisema katika taarifa kwamba hakuna ushahidi wa kuongeza muda wa kupiga kura kufuatia tatizo hilo.
West Virginia ABC News wanakadiria kwamba Donald Trump atashinda Virginia Magharibi.
Virginia Magharibi imempigia kura mgombea wa Republican tangu 2000. Mwaka 2012 chama hicho kiliongeza uungwaji mkono wake katika jimbo hilo.
Kentucky Trump atashinda. Jimbo hilo ambalo limekuwa ngome ya Republican lilimpigia kura mgombea wa Democratic mgombea alipotoka majimbo ya kusini pekee, mfano Jimmy Carter mwaka 1976 na Bill Clinton in 1992.
Vermont Clinton atashinda. Obama alipata 66% katika jimbo hilo la New England mwaka 2012.
Indiana ni Trump. Jimbo hilo ni ngome ya Republican ingawa Barack Obama alipata ushindi mwembamba 2008.
Mpwa wa George W Bush, George P Bush, alizua mjadala siku chache zilizopita alipodokeza kwamba mjomba wake, George W Bush angempigia Hillary Clinton.
Msemaji wa rais huyo wa zamani Freddy Ford hata hivyo amefafanua na kusema hakumpigia Clinton wala Trump.
Hata hivyo, kwenye viti vingine amewapigia kura wagombea wa Republican.
Kituo kimoja cha kupiga kura huko Azusa ,katika jimbo la Carlifornia kimewekwa chini ya ulinzi mkali baada ya risasi kufyatuliwa karibu na eneo hilo.
Mtu mmoja amedaiwa kufariki kulingana na polisi huku maafisa walioshiriki katika kutuliza tukio hilo wakidaiwa kuwa salama.
Ufyatulianaji huo wa risasi uliripotiwa kutokea katika kituo cha kupiga kura lakini hakuna habari kwamba unahusishwa na siasa.
Awali shirika la habari limeripoti kwamba watu wawili wamejeruhiwa.
Ufyatulianaji huo wa risasi ulifanyika katika nyumba moja iliopo jirani kulingana na Jerry Willson afisa wa kituo cha polisi cha Azusa.
ABC News wanakadiria kwamba Donald Trump atashinda Virginia Magharibi.
Virginia Magharibi imempigia kura mgombea wa Republican tangu 2000. Mwaka 2012 chama hicho kiliongeza uungwaji mkono wake katika jimbo hilo.
Kwa sasa, vituo vya kupigia kura vimefungwa Ohio na maeneo mengi Carolina Kaskazini.
Maafisa Carolina Kaskazini wameamua kuacha wazi vituo vinane karibu na mji wa Durham.
Jaji wa jimbo la Nevada amepinga mashtaka yaliowasilishwa na Donald Trump ambaye anataka masanduku ya kupiga kura katika vituo vilivyofunguliwa licha ya muda wa kupiga kura kukamilika kutengwa katika maeneo hayo.
Upande wa Trump umelalama kwamba maafisa wa eneo hilo walivifungua vituo hivyo vya kupigia kura licha ya muda wa kupiga kura kukamilika ili kuwaruhusu wapiga kura wa Hispanic.
Timu ya kampeni ya Trump ilitaka kujua majina ya wafanyikazi hao wa tume ya uchaguzi walioruhusu vituo hivyo kuwa wazi ,wakisema kuwa makarani wa vituo hivyo walitekeleza vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.
Idadi kubwa ya wapiga kura imedaiwa kujitokeza katika vituo vya kupiga kura nchini Marekani huku raia wakipiga kura kumchagua kiongozi wao.
Wachanganuzi wanatarajia kwamba idadi kubwa ya wapiga kura ndio itakayobaini ni nani kati ya Donald Trump na Hillary Clinton atakayeshinda ikulu ya white house.
Yeyote atakayeshinda,uchaguzi huo utatambuliwa kuwa wa kihistoria.
Hakuna mwanamke aliyewahi kuwa rais wa Marekani na kwamba wadhfa huo wa urais haujawahi kuwa na mtu ambaye hajawahi kuhudumia serikali ama kuhudumu katika jeshi.
Awali tulikuwa tumeripoti matatizo katika mfumo wa kupiga kura wa kielektroniki katika jimbo la Carolina Kaskazini .
Kaunti ya Durham imekuwa na matatizo na programu yake ya upigaji kura ambayo kulingana na vyombo vya habari inasababisha mlolongo mrefu na watu kusubiri kwa muda mrefu.
Maafisa wa uchaguzi wa Durham walipiga kura ya kuongeza muda wa kupiga kura kwa saa mbili jioni ya leo.
Lakini ili kufanya hivyo ,itahitaji kuungwa mkono na bodi ya uchaguzi ya Carolina Kaskazini ambapo tayari bodi hiyo imechapisha ujumbe wa Twitter ikisema kuwa wanachama wake watano watafanya mkutano katika kipindi cha saa moja lijalo ili kujadiliana kuhusu ombi hilo.
Inadaiwa kuwa huenda rais wa zamani wa Marekani George W. Bush na mkewe Laura Bush wamempigia kura Hillary Clinton kulingana na Rush Limbaugh, mtangazaji wa radio ya wahafidhina.
Tangu Jeb Bush ashindwe katika kinyanganyiro cha kuwa mgombea wa chama cha Republican mnamo mwezi Februari ,familia yake imejiondoa katika siasa za uchaguzi huu.
Wagombea wote wawili Trump na Clinton watafanya mikutano yao ya kusheherekea ushindi katika mji wa New York.
Mwandishi wa BBC Nada Tawfik yuko katika kituo cha Javits katikati mwa mji wa Manhattan ambapo amezungumza na meneja wa kampeni za bi Clinton.
Mkutano wa Trump utafanyika yapata maili mbili pekee kutoka mkutano wa Clinton huko Midtown na walioalikwa ni marafiki na mashabiki wa kampeni ya Trump na mgombea mwenza Pence.