Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Obama ampigia simu Trump kumpongeza

Mgombea wa Republican Donald Trump amemshinda Hillary Clinton wa Democratic katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Moja kwa moja

  1. Trump ndiye mshindi Florida

    ABC News wametangaza kwamba makadirio yao yanaonyesha Trump ameshinda jimbo muhimu la Florida.Sasa Trump ana kura 222 za wajumbe na Clinton 197 za wajumbe. Mshindi anahitaji kura 270.

    Jimbo hilo huwa muhimu sana kwa mgombea yeyote.

    Jimbo hilo lilimpigia Obama mwaka 2008 na 2012 (Democratic), lakini George W Bush (Republican) alishinda uchaguzi uliotangulia 2000 na 2004. Jambo la kushangaza ni kuwa alikuwa mbele na kura 537 pekee mwaka 2000.

    Hata hivyo, ilichukua siku 36 kwake kuthibitishwa kuwa mshindi, kwa hivyo iwapo wagombea watakaribiana sana usitarajie matokeo yatangazwe haraka.  

  2. Habari za hivi punde, Donald Trump mshindi Utah

    ABC News wanakadiria kwamba Trump ameshinda jimbo la Utah, ambalo lina wajumbe 6.

  3. Trump atashinda Florida - Vyombo vya habari Marekani

    Vyombo vya habari Marekani vinakadiria kwamba Donald Trump atashinda katika jimbo muhimu la Florida. Jimbo hilo lina kura 29 za wajumbe. Bado tunasubiri makadirio ya ABC News.

    Jimbo hilo huwa muhimu sana kwa mgombea yeyote.

    Jimbo hilo lilimpigia Obama mwaka 2008 na 2012 (Democratic), lakini George W Bush (Republican) alishinda uchaguzi uliotangulia 2000 na 2004. Jambo la kushangaza ni kuwa alikuwa mbele na kura 537 pekee mwaka 2000.

    Hata hivyo, ilichukua siku 36 kwake kuthibitishwa kuwa mshindi, kwa hivyo iwapo wagombea watakaribiana sana usitarajie matokeo yatangazwe haraka.  

  4. Clinton: Nashukuru kwa yote

    Hillary Clinton ameandika kwenye Twitter kwamba anashukuru kwa yote yanayofanyika, bila kujali matokeo yatakayotolewa usiku wa leo (Marekani bado ni usiku).

  5. Habari za hivi punde, Clinton mshindi jimbo la Oregon

    ABC News wanakadiria kwamba Hillary Clinton ndiye mshindi jimbo la Oregon. Jimbo hilo lina kura 7 za wajumbe. Sasa Clinton ana kura 197 za wajumbe na Trump 187 za wajumbe. Mshindi anahitaji kura 270.

  6. Trump ashinda North Carolina

    Donald Trump ameshinda jimbo la North Carolina, kwa mujibu wa makadirio ya ABC News.

      Clinton kwa sasa ana jumla ya kura 190 za wajumbe na Trump 187. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.  

  7. Habari za hivi punde, Clinton ashinda California na Hawaii, Trump Idaho

    Hillary Clinton ameshinda majimbo ya California na Hawaii naye Donald Trump akashinda Idaho.

    California ina kura 55 za wajumbe na Hawaii 4. Idaho ina kura 4 za wajimbo.

    Ushindi California umumuwezesha Clinton kumpita Trump kufikia sasa, akiwa na kura 190 za wajumbe naye Trump kura 172. Mshindi anahitaji jumla ya kura 270.

  8. Habari za hivi punde, Clinton ashinda Colorado

    ABC News wanakadiria kwamba Clinton ndiye mshindi Colorado, jimbo jingine lililokuwa linashindaniwa. Jimbo hilo lina kura 9 za wajumbe. Clinton kwa sasa ana jumla ya kura 131 za wajumbe na Trump 168. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.

  9. Habari za hivi punde, Clinton kushinda Virginia

    ABC News wamekadiria kwamba Hillary Clinton ndiye mshindi jimbo la Virginia, moja ya majimbo yaliyokuwa yanashindaniwa. Jimbo hilo lina kura 13 za wajumbe.

  10. Habari za hivi punde, Trump ndiye mshindi Ohio

    ABC News wamekadiria kwamba Donald Trump atashinda jimbo muhimu la Ohio. Jimbo hilo lina kura 18 za wajumbe.

    Sasa Clinton ana kura 109 za wajumbe na Trump 168. Mshindi anahitaji kura 270.

    Ohio ni jimbo ambalo matokeo yake yalisubiriwa zaidi. Jimbo hilo limeunga mkono mgombea aliyeshinda urais kila uchaguzi wa urais isipokuwa wakati mmoja pekee tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.  

  11. Hali ilivyo kambi ya Donald Trump

    Bintiye Donald Trump, Ivanka amepakia kwenye Twitter picha ya hali ilivyo Trump na watu wake wa karibu wakifuatilia matokeo.

    Tazama:

  12. Trump akifuatilia matokeo

    Donald Trump amepakia kwenye Twitter picha yake na mgombea mwenza wake, mkewe Melania, miongoni mwa wengine, wakifuatilia matokeo ya urais Marekani.

    Tazama:

  13. Habari za hivi punde, Trump ashinda Missouri, Clinton New Mexico

    Donald Trump ameshinda jimbo la Missouri naye Hillary Clinton akashinda New Mexico kwa mujibu wa makadirio ya ABC News.

    Missouri kuna kura 10 za wajumbe na New Mexico kura 5 za wajumbe.

    Sasa Clinton ana kura 109 na Trump 150. Mshindi anahitajika kupata kura 270 za wajumbe.

  14. Habari za hivi punde, Trump ashinda jimbo la Montana

    Mgombea wa Republican Donald Trump ameshinda jimbo la Montana. Jimbo hilo lina kura 3 za wajumbe. Clinton sasa ana jumla ya kura 104 za wajumbe na Trump 140.

  15. Hakuna dalili za ushindi wa mapema kwa Clinton

    Baadhi ya wachanganuzi walikuwa wamedokeza kwamba huenda Hillary Clinton akashinda mapema iwapo angeshinda katika jimbo muhimu kama vile Florida. 

    Lakini ikizingatiwa kwamba Trump kwa sasa yuko mbele kidogo Florida na majimbo mengine muhimu kama vile Georgia hakujatangazwa anayekadiria kushinda, inaonekana huenda mshindi asifahamike karibuni.

  16. Trump 'ana nafasi nzuri' - New York Times

    Gazeti la New York Times, ambalo limekuwa likiunga mkono Hillary Clinton, linasema mfumo wake wa kompyuta kwa sasa unabashiri uwezekano wa Trump kushinda kuwa 53%.

  17. Trump 'ana nafasi ya kushinda urais'

    Nate Silver, anayeandika blogu ya FiveThirtyEight (538 ni idadi ya kura za wajumbe) anasema Clinton anaonekana kuwa na uwezekano wa kushinda wingi wa kura kwa  3% hadi  4%, kama zilivyoonyesha kura za maoni kitaifa.

    Hata hivyo, ameongeza, anaweza tu kushinda kura 290 za wajumbe, ushindi mwembamba, ambao una maana kwamba kuna uwezekano wa Donald Trump kushinda urais.

    Hilo huenda liakafanyika kwa sababu wafuasi wa Clinton hawapo kwa wingi majimbo yanayoshindaniwa.

    Silver anafahamika kwa kuweza kutabiri matokeo katika majimbo yote 50 mwaka  2012.

  18. Habari za hivi punde, Louisiana kwenda kwa Trump

    ABC News wanakadiria kwamba Donald Trump atashinda jimbo la Louisiana.

    Jimbo hilo limepigia kura mgombea wa Republican katika chaguzi nne mtawalia lakini waliunga mkono  Bill Clinton mwaka 1992 na 1996.

    Jimbo hilo huwa halichukuliwi kama ngome ya Republican kama yalivyo majimbo mengine jirani.Jimbo hilo lina kura nane za wajumbe.

  19. Aliyepigana vita Iraq ashinda useneta Illinois

    Tammy Duckworth ameshinda kiti cha useneta Illinois. 

    Alikuwa rubani wa helikopta katika jeshi na alipoteza miguu yake miwili akipigana vita Iraq.

    Duckworth amekuwa akihudumu kama mbunge katika Bunge la Wawakilishi.

    Amemshinda seneta Mark Kirk, ambaye amekosolewa baada yake kutofanya vyema kwenye mdahalo.

    Mamake  Duckworth anatoka Thailand lakini babake ni Mmarekani.

    Ushindi huo ni muhimu kwa Democratic wanaojaribu kutwaa tena udhibiti wa Bunge la Seneti. Ili kufanya hivyo, wanahitaji kushinda viti vitatu vya usenera. Viti vinane vinachukuliwa kuwa na ushindani mkubwa, na tayari wameshindwa Indiana na Ohio.

  20. Habari za hivi punde, Clinton mshindi Connecticut, kwa mujibu wa ABC

      Hillary Clinton ameshinda jimbo la Connecticut, ngome ya chama cha Democratic ambapo amejishindia kura saba za wajumbe, kwa mujibu wa ABC News. Clinton sasa ana kura za wajumbe 104 na Trump 129.