Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya Corona: Kwa nini tunapaswa kujifunza kuishi na corona, sio kupigana nayo
Hivi karibuni serikali ya Uingereza ilisema kwamba inapania kuudhibiti ugonjwa wa COVID-19, kama mafua.
Mawaziri na washauri wake wa kisayansi kuhusu chanjo na tiba mpya walisema hatua hiyo itapunguza idadi ya vifo na kuwawezesha watu kuish na virusi hivyo badala ya kukabiliana navyo.
Lakini je hili linawezekana?
Lengo lisiloweza kufikiwa
Kuangamiza kabisa corona duniani itakuwa ufanisi mkubwa, hasa ikizingatiwa maafa na uharibifu unaosababishwa na ugonjwa huo.
Tatizo ni kwamba kirusi kimoja pekee kilichoangamizwa : Tetemaji (smallpox), mwaka 1980.
Ilichukua miongo kadhaa kufikia hatua hiyo, na wanasayansi na serikali zilifanikiwa kufikia lengo hilo kutokana na msururu wa mazingira ya kipekee.
Kwanza chanjo yake ilikuwa imara kiasi cha kuwa haikuhitaji kuhifadhiwa kwenye jokofu, na ilipotolewa matokeo yake ilikuwa moja kwa moja ima imefanya kazi au la.
Pia ilikuwa wazi kutambua mtu ameambukizwa. Haikuwa lazima kufanya uchunguzi wa maabara, hali ambayo ilisaidia sana kudhibiti mlipuko wa ugonjwa.
Corona kama sote tunavyojua, ni tofauti kabisa na tetemaji.
Mkakati wa "covid zero"
Licha ya kwamba lazima mtu afanyiwe vipimo vya maabara kubaini kama ameambukizwa virusi vya corona, wataalamu wamekuwa wakitumia mkakati unaofahamika kama "zero covid" unaolenga kuangamiza virusi hivyo.
Hii inamaanisha kupunguza idadi ya maambukizi katika eneo lililoathirika kwa hadi karibu sufuri na kuendelea kudhibiti hali ya maambukizi kwa kiwango hicho.
Mmoja wa wataalamu wanaounga mkono pendekezo la kuudhibiti ugonjwa wa COVID-19, kama surua ni Profesa Devi Sridhar,mtaalamu wa afya ya uma katika Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Scotland.
Sridhar anaamini tunastahili kutibu COVID-19 kama surua au ukambi, ugonjwa ambao umeangamizwa katika baadhi ya mataifa tajiri.
Profesa anasema kuwa juhudi kuweka vizuizi vya mara kwa mara na kupunguza idadi ya visa vya maambukizi pamoja na mfumo mzuri zaidi wa ufuatiliaji na upimaji na chanjo zaidi, itaruhusu virusi vyenyewe virusi kuzoea "maisha ya kawaida", ili kuwezesha mikahawa, baa pamoja na hafla za michezo na muziki.
Lakini athari ya hatua hiyo, anasema itakuwa kudhibitiwa kwa usafiri wa kimataifa na kuweka vizuwizi vya mpakani, ikiwa ni pamoja na " watu kukaa karantini kwa siku kadhaa au muda mrefu" visa vya maambukizi vikipanda.
Je! Inawezekana kupata COVID-19 na kueneza kwa wengine baada ya kupata chanjo?
"Maisha yanaweza kurejea walau kataika hali ya kawaida.Tunaweza kufungua njia ya usafiri kati ya nchi moja hadi nyingine ambayo imefuatilia mfumo huo wa kudhibiti maambukizi," anasema.
Tatizo la njia ya ukambi
Huenda ingekuwa njia nzuri lakini ile ambayo wengi wanaamini haiwezi kutekelezeka kwani inahitaji vizuizi ambavyo vitakuwa na athari kwa kijamii na kiuchumi.
"Mkakati wa Covid Zero haiendani na haki na uhuru wa mtu binafsi ambao huonyesha demokrasia ya baada ya vita ," anasema Profesa Francois Balloux, Mkurugenzi wa Taasisi ya Genetics katika Chuo Kikuu cha London.
Nchi kama New Zealand, Taiwan na Australia wamefanikiwa kufikia hilo kwasababu waliweza kuzuia virusi kushamiri, na kila kitu kinaashiria endapo watu watapewa chanjo, wataanza kuondoa vikwazo vya mpakani.
Changamoto baada ya hapo itakuwa "kupiga hatua mbele ya virusi," anaeleza. Lakini hili sio jambo gumu kama inavyotazamiwa.
Virusi vya Corona vinaweza kudhibitiwa kama vile vinavyosababisha mafua, anasema, kumaanisha chanjo inatarajiwa kufanya kazi kwa kiwango kikubwa.