Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jessica Krug amekiri kuwa mweupe, mwenye asili ya Kiyahudi
Profesa mmoja Marekani ambaye kazi yake inaangazia Afrika na Waafrika wanaoishi ughaibuni amesema alidanganya kwamba yeye ni mweusi.
Jessica Krug, profesa mshiriki wa Chuo Kikuu cha George Washington, amekubali kwamba yeye ni mweupe mwanamke wa Wakiyahudi kutoka mji wa Kansas.
"Nimejijengea maisha ya uongo kwamba mimi ni mtu mweusi, na kudanganya katika kila hatua ya maisha yangu," aliandika.
Kesi yake inafanana sana na Rachel Dolezal, mwanaharakati mzungu aliyedai kwamba yeye ni mweusi.
Bi. Dolezal kwanza aligonga vichwa vya habari mwaka 2015 wakati wazazi wake walipomkana kwamba yeye sio mzungu.
Mwanamke huyo aliyekuwa mwanaharakati wa haki za kiraia na mhadhiri wa masomo ya Afrika alidanganya kwamba ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika kwa miaka mingi, lakini anasema "alijitambua kama mweusi".
Kulingana na makala iliyochapishwa Alhamisi, Jessica Krug alisema aliamini visivyo kuhusu utambulisho, " kwamba sikuwa na haki ya kudai: Ni mwafrika wa kwanza kutoka Afrika Kaskazini, ni mtu mweusi mwenye asili ya Marekani, kisha mwenye asili ya Carribean kutoka Bronx".
Anaelezea tabia hii kama iliyosawa na vurugu, wizi na ulaghai wa namna mbalimbali zinazotumiwa na wazungu kuendelea kutumia na kunyanyasa utambulisho wa mtu mweusi na utamaduni", na kuongeza kwamba aliendelea kudanganya hata katika uhusiano wake wa binafsi.
Alilaumu kudanganya kwake kwa misingi ya matatizo ya akili na mfadhaiko aliopitia miaka ya awali, ingawa alisema hiyo haikuwa kisingizio cha matendo yake.
Makala ya Bi. Krug haikutoa sababu ya uamuzi wake wa kukiri uongo wake, na pia kwanini ameamua kusema ukweli sasa.
Hatahivyo, mwandishi Hari Ziyad alisema uamuzi huo umewadia kwasababu amejulikana".
"Jess Krug... ni mtu nimemuita rafiki hadi asubuhi hii aliponipigia simu na kukubali kila kitu kilichoandikwa kwenye makala. Hakuchukua hatua hiyo ili kuonekana mzuri," aliandika kwenye mtandao wa Twitter.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, Bi. Krug pia alitumia jina Jessica La Bombalera kama mwanaharakati.
Katika moja ya video aliyoitoa mapema mwaka huu, alikosoa Wazungu wa New York kwa kushindwa kutumia muda wao vizuri na wenyeji weusi na wengineo wasio wazungu kutoka New York.
Chuo Kikuu cha George Washington, ambapo Bi. Krug anafundisha masomo ya Afrika, Caribbean na historia ya wanaoishi ughaibuni, kimesema kinajua kuhusu makala ya Bi. Krug lakini hakiwezi kuzungumza lolote kuhusiana na hilo.