Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Marekani yaishambulia Iran baada ya vikosi vyake kushambulia meli ya mizigo

Kamandi Kuu ya Marekani au Centcom ilishambulia vituo vya kuhifadhia makombora na ndege zisizo na rubani siku ya Ijumaa.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Mama afariki akimuokoa binti yake mchanga katika matetemeko la ardhi Venezuela

    Mama mmoja raia wa Venezuela amefariki alipokuwa akimwokoa bintiye wakati wa tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo, kwa mujibu wa mwanasoka Héctor Bello na vyombo vya habari nchini humo.

    Bello aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram kwamba "upendo wake wa thamani", uliotajwa na vyombo vya habari vya Venezuela kama mke wake Andrea, uliokoa maisha ya mtoto wao mchanga wakati wa tetemeko kubwa la ardhi.

    "Nitasimulia hadithi ya jinsi ulivyomuokoa, mpenzi wangu - jinsi ulivyohatarisha maisha yako mwenyewe kwa ajili ya binti yetu, jinsi ulivyokuwa mwanamke shujaa ambaye hakuwahi kumuacha, hata ulipovuta pumzi zako za mwisho," Bello aliandika katika chapisho lake.

    Waokoaji wanaendelea kupekua vifusi kuwatafuta manusura baada ya matetemeko mawili ya ardhi kukumba mji mkuu Caracas kusababisha vifo vya takriban watu 920 na kujeruhi zaidi ya 3,000.

    Maelezo zaidi:

  2. Kombe la Dunia 2026: Ubelgiji yafuzu raundi ya pili baada ya kuilaza New zealand

    Leandro Trossard alifunga mara mbili Ubelgiji ikijikatia tiketi ya kutinga hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia kwa ushindi mkubwa dhidi ya New Zealand.

    Trossard alianza kufunga dakika ya 28 huku New Zealand ikiruhusu kona iliyopigwa na Kevin de Bruyne, na kumruhusu fowadi huyo wa Arsenal kumalizia kutoka eneo la karibu baada ya mpira kutoka nyuma ya beki Tim Payne.

    Kikosi cha Rudi Garcia huenda hakingeonekana hadi kipindi cha mapumziko lakini karibui dakika tano baada ya mapumziko walipata lao la pili.

    De Bruyne alimpigia Trossard, japo mkwaju wa kwanza lilizuiwa lakini akafuatisha kwa ustadi kwenye lango la karibu.

    Matokeo hayo yalitiwa shaka katika dakika ya 66 pale De Bruyne alipochomoa shuti kali la mguu wa kushoto kutoka umbali wa yadi 20.

    New Zealand walipata bao baada ya Elijah Just kupachika wavuni bao lake la tatu katika michuano hiyo lakini Ubelgiji walirejea kileleni muda mfupi baada ya Romelu Lukaku kuifunga bao lengine kwa kichwa ndani ya sekunde 56 tu baada ya kuingia uwanjani.

    Alexis Saelemaekers, naye aliongeza idadi ya magoli alipofunga bao la tano katika dakika za majeruhi.

    Maelezo zaidi:

  3. Maandamano yalipuka kusini mwa Beirut baada ya Lebanon-Israel kukubaliana

    Video iliyorekodiwa karibu usiku wa manane Jumamosi kusini mwa Beirut inawaonyesha waandamanaji na waendesha pikipiki wakikusanyika barabarani, wakipeperusha bendera, baada ya Lebanon na Israel kutia saini makubaliano ya kumaliza mapigano kati ya Israel na Hezbollah. Moshi mkubwa mweusi unaonekana nyuma.

    Shirika la habari la Reuters lilitaja eneo video hiyo iliporekodiwa kuwa viungani mwa kusini mwa Beirut kwa kuchunguza ishara, nguzo za umeme, na umbo la mitaa, na kuilinganisha na satelaiti na picha za kumbukumbu.

    Hata hivyo, muda halisi ambao video ilirekodiwa haujathibitishwa kikamilifu.

    Reuters iliripoti kuhusu maandamano hayo Ijumaa usiku, na toleo la zamani la video hiyo halijapatikana mtandaoni tangu Juni 26.

    Lebanon na Israel wameyataja makubaliano hayo kama hatua ya kwanza, ambapo Hezbollah lazima ipokonye silaha na majeshi ya Israel lazima yaondoke Lebanon.

    Bado haijabainika jinsi makubaliano hayo yatakavyotekelezwa. Hezbollah imesema haitazingatia.

    Soma pia:

  4. Marekani na Iran: Mashambulizi yatajibiwa kwa mashambulizi- JD Vance

    Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance almeonya Iran kwamba itakabiliwa na "vikali" ikiendelea kufanya mashambulizi zaidi.

    Onyo hilo lilitolewa baada ya jeshi la Marekani kutangaza kuwa limeshambulia Iran kujibu shambulizi lake dhidi ya meli ya mizigo katika mlango wa bahari wa Hormuz.

    Vance aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: "Iran ilitia saini makubaliano ya kusitisha mapigano na tumezingatia. Ikiwa wana maswali kuhusu utekelezaji wa makubaliano hayo, wanaweza kuwasiliana nasi. Lakini mashambulizi ya vurugu yatakabiliwa kwa vurugu."

    Amesisitiza kuwa lengo la mkataba wa makubaliano ulitiwa saini kati ya Marekani na Iran ni kumaliza karibu miezi minne ya vita.

  5. Idadi ya waliofariki katika tetemeko la ardhi Venezuela yafikia 920

    Zaidi ya watu 900 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine 3,360 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi la Venezuela, kulingana na serikali, huku waokoaji wakiendelea kuwatafuta manusura wa mkasa huo.

    Waliojeruhiwa wanatibiwa katika vituo vya matibabu vya muda baada ya makumi ya majengo kaskazini mwa nchi hiyo kuharibiwa na matetemeko hayo mawili, ukiwemo mji mkuu Caracas.

    Afisa mkuu wa serikali alisema mamia ya waokoaji wa kimataifa wamewasili nchini, na wengine zaidi wako njiani.

    Matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliitikisa Venezuela ndani ya sekunde moja baada ya nyingine Jumatano. Tetemeko la pili lililokuwa na ukubwa wa 7.5. lilikuwa mojawapo ya mitetemeko makubwa zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo katika karne moja.

    Eneo la La Guaira, kaskazini mwa mji mkuu wa Caracas limeathirika zaidi, maafisa wanasema.

    Watu wengi hawajulikani walipo huku maafisa wakihofia huenda idadi ya vifo ikaongezeka ingawa juhudi za uokoaji bado ziendelea.

    Maelezo zaidi:

  6. Marekani yaishambulia Iran baada ya vikosi vyake kushambulia meli ya mizigo

    Jeshi la Marekani limefanya mashambulizi katika maeneo maalum nchini Iran baada ya Rais Donald Trump kuishutumu Iran kwa "ukiukaji wa kijinga" wa makubaliano yake ya kusitisha mapigano kufuatia shambulio dhidi ya meli ya mizigo katika Mlango wa bahari wa Hormuz.

    Kamandi Kuu ya Marekani au Centcom ilisema ilishambulia vituo vya kuhifadhia makombora na ndege zisizo na rubani na sehemu za rada za pwani siku ya Ijumaa.

    Ilisema hatua hiyo ilikuwa kujibu shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya meli ya mizigo siku ya Alhamisi, tukio ambalo lilisimamisha mpango wa kuwahamisha maelfu ya mabaharia waliokwama katika eneo hilo.

    Tehran ilisema meli hiyo ya mizigo ilishambuliwa kwa sababu ilikuwa ikitumia njia ambayo ahaijaidhinishwa kupita kwenye maji ya Ghuba.

    Centcom - ilielezea mashambulio hayo kama "jibu kubwa" la kulipiza kisasi shambulio la ndege zisizo na rubani za Iran.

    "Uchokozi usio na msingi dhidi ya meli za kibiashara uliofanywa na vikosi vya Iran ulikiuka wazi makubaliano ya usitishaji mapigano," ilisema katika taarifa.

    Centcom inasema jeshi la Marekani "litaendelea kutoa uratibu wa njia salama na usaidizi kwa meli za kibiashara zinazopita kwenye mlango wa bahari wa Hormuz".

    Hata hivyo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) lililaumu "serikali ya Marekani kwa kukiuka mkataba".

    Katika taarifa yake IRGC ilisemaMarekani ilifanya mashambulizi ya anga katika ufuo wa Iran "kwa visingizio mbalimbali vya meli inayokiuka utaratibu wa usafiri katika Mlango wa bahari wa Hormuz".

    IRGC ilisema jeshi lake la majini lililipiza kisasi kwa kushambulia ngome kadhaa za kijeshi za Marekani katika eneo hilo, bila kutoa maelezo zaidi. BBC imewasiliana na Pentagon kuthibitisha hilo.

    "Wakiendelea kufanya uchokozi majibu yetu yatakuwa makubwa zaidi kuliko haya," IRGC iliongeza.

    Tehran ilifunga mkondo huo baada ya mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran kuanza mwishoni mwa mwezi Februari.

    Soma zaidi:

  7. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja