Virusi vya corona: 'Sasa iweje?' Jinsi rais wa Brazil anavyopuuza janga la Covid-19

Iliyochapishwa

Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19 nchini Brazili vinaendelea kuongezeka huku mamia ya watul wakifariki kila siku nchini humo, lakini rais Jair Bolsonaro amekuwa akitumia maneno mawili kuelezea hali hiyo: "Sasa iweje?"

Rais huyo kwa mara nyingine amewaomba raia wa Brazil warejee kazini, alipokutana na kuwasalimia kwa mikono na hata kupiga seilfie na wafuasi wake katika mkutano wa hadhara mjini Brasilia siku ya Jumapili (3).

Lakini anakabiliwa na ukosowaji mkubwa kwa kupuuza ugonjwa huo mara kwa mara.

Idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa virisi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 nchini humo imepita 100,000, huku zaidi ya wa 7,000 wakifariki - idadi ambayo ni yajuu zaidi Amerika Kusini. 

Lakini alipoulizwa na mwandishi wa habari kuhusu idadi ya vifo, ambayo ilikuwa imepita 5,000 siku ya Jumanne (Aprili 28), rais alisema:

"Sasa iweje? Samahani, mwataka nifanye nini? Siweezi kufanya miujiza."

'Mafua kidogo tu'

Bw. Bolsonaro aliwahi kupuuza ugonjwa wa Covid-19 na kuutaja kama "homa kidogo tu" na kulaumu vyombo vya habari kwa kueneza taarifa ghushi ili kuzua taharuki katika jamii.

Huku hayo yakijiri, katika mitandao ya kijamii, kundi linalomuunga mkono rais lilichapisha picha za majeneza feki ambazo linasema ilizikwa bila kuwa na maiti ili kuongeza idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo.

Karibu wanahabari watatu walishambuliwa katika mukutano huo wa siku ya Jumapili ambao ulihudhuriwa na mamia ya waandamanaji waliokuwa wakishinikiza Bungea la Congress na mahakama ya juu zaidi kufungwa.

Shirika la habari la Reuterslilishuhudia mmoja wa wapiga picha wa gazeti la O Estado de S. Paulo akiburuzwa chini na kupigwa mateke mara kadhaa.

Bw. Bolsonaro pia aliwahi kusema kuwa "watu walio na historia ya uanariadha kama yeye" hawatahisi chochote wakipatwa na virusi - ikizidi sana, watahisi kupatwa na mafua kidogo tu, alidai.

Lakini kiongozi huyo wa mrengo wa kulia anakabiliwa na shinikizo kubwa la kumtaka abainishe ikiwa ameambukizwa ugonjwa huo, baada ya maafisa 20 katika msafara wake uliokuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Marekani mwezi Machi kugunduliwa kuwa na maradhi ya Covid-19.

Mnamo April 19, Bw. Bolsonaro aliungana na waandamanaji wengine waliokuwa wakishinikiza kuondolewa kwa marufuku ya kutotoka nje nje ya mji mkuu wa Brasilia. Wakati wa akitoa hotuba yake alionekana akikohoa.

Lakini kauli yake ya hivi punde ya kusema "Sasa iweje?" imewaghadhabisha hata baadhi ya wafuasi wake

'Kutojali'

Guilherme Rolim,daktari wa meno mwenye umri wa miaka 36,anasema alimpigia kura Bw. Bolsonaro mwaka 2018 kwasababu alitaka "mabadiliko".

Bw. Rolim aliiambia BBC Brasil kuwa anachukulia chaguo lake kama "mabaya ya lazima" lakini, baada ya kumpoteza baba yake kutokana na Covid-19, ameilaumu serikali kwa jinsi inavyoshughulikia suala janga hilo.

"Bolsonaro ni jamaa asiyejali. mastamshi yake ayanaashiria utepetevu wa hali ya juu katika jukumu lake kama kiongozi. Rais anafanya mzaha na kitu hatari sana," alisema.

"Kama kijana aliyempoteza baba yake kutokana na ugonjwa wa corona, Nahofia kauli zinazotolewa na rais. Pengine anasema maneno hayo kwa sababu hajapoteza jamaa wa karibu, hajapata machungu yanayotokana na kumpoteza mtu anayempenda."

Katika majimbo kama ya Sao Paulo na Rio de Janeiro, hatua za watu kuwekwa karantini zimekuwa zikirefushwa, na magavana katika majimbo hayo wamekuwa wakimkosoa Bw. Bolsonaro.

Coronavirus pia iliingizwa siasa baada ya rais Bw. Bolsonaro kumfuta kazi waziri maarufu wa afya, Luiz Henrique Mandetta, mwezi uliopita baada ya kutofautiana naye kuhusu jinsi ya kukabiliana na coronavirus.

Alimteua Nelson Teich ambaye ni mtaalamu wa oncolojia katika kliniki ya kibinafsi kuchukua nafasi ya Bw. Mandetta.

Mwenendo wa rais kuhusu coronavirus umeungwa mkono na baadhi ya sekta katika jamii, hususan sekta za kiuchumi ambazo zimeathiriwa na amri ya kutotoka nje.

'Brazil haiwezi kusimama'

Kura ya maoni iliyochapishwa na Datafolha Aprili 29 inaashiria kuwa asilimia 52 ya raia wa Brazil wanaamini kuwa watu wanastahili kukaa nyumbani, ikilinganishwa na asilimia 60 mwanzoni mwa mwezi.

Miongoni mwa watu matajiri, wanaounga mkono karantini ni 39%.

Junior Durski, milionea mmiliki wa migahawa ya Madero, alizua gumzo baada ya kusemamwezi Machi kuwa: "Sasa watu 5,000 watafariki kutokana na virusi vya corona na hatuwezi kuepuka hilo. Hatuwezi kufunga kila kitu, na kujificha adui na tusifanye kazi."

Lakini baada alisema kauli yake hiyo ilieleweka vibaya.

Wafanyabiashara wengine wengi wamekubaliana ka kauli hoyo, akiwemo bilionea Luciano Hang, mmiliki wa maduka ya Havan na "muinjilisti wa biashara huru", kwa mujibu wa shirika la habari la Bloomberg.

Bw.Hang amekosoa "uwoga unaozingira" ugonjwa wa Covid-19 na kusema kuwa hana hofu kuhusu biashara yake kuhusiana na hali ilivyo bali, bali anahofia uchumi wa Brazil. Yeye binafsi anaweza kuwafuta kazi wafanyakazi wake 22,000 na "kuenda kujivinjari ufukweni".

Kutengwa Kimataifa

Lakini dunia inapoendelea kuwa na wasiwasi kuhusu athari zinazosababishwa na janga la virusi vya corona, msimamo wa Bw. Bolsonaro unaoneka kumfanya atengwe.

Tom Phillips, mwandishi wa gazeti la Guardian mjini Rio,aliandika kwenye Twitter: "Najaribu (na kushindwa) kutafakari kiongozi mwingine duniani anayeulizwa kuhusu maelfu ya vifo katika nchi zao na jibu lao ni : 'Sasa iweje?'"

Hata Donald Trump,ambaye Bw. Bolsonaroamejivunia kufananishwa nae, anaunga mkono hatua za kukabiliana na maambukizi kama vile kutokaribiana licha ya athari zake za kiuchumi.

Wakati wa akihutubia wanahabari katika ikulu ya White House siku Alhamisi (28), aligusia hali ya Brazil.

"Nachukia kusema, lakini Brazil iko juu sana, jedwali lao liko juu, liko juu sana. Huko juu, karibia mwisho wa jedwali,"alisema Trump. "Rais wa Brazil ni raifiki wangu mzuri, lakini wanaishi katika nyakati ngumu sana."

Gavona wa jimbo la Florida nchini Marekani, Ron de Santis, amesema kuwa wanafuatilia ''kwa karibu'' hali nchini na kuongeza kuwa huenda wakabuni hatua za udhibiti hususana kwa raia wa Brazil.

Wataalamu wanasema viwango vya rasmi vya maambukizo ya Covid-19 huenda zisitoe hali halisi ya mambo

Kwa mujibu wa Imperial College London, viwango vya maambukizo nchini Brazil imefikia 2.8 na ni ya juu zaidi ikilinganishwa na mataifa mengine 48.

Mataifa yanayokadiria viwango vya maambukizi yako chini 1- kumaanisha kila mtu anayepata ugonjwa huo anaambukiza pengine mtu mmoja yameanza kulegeza masharti ya kutotoka nje.

Hii ni kwasababu ni watu wachache wanaoambukizwa hadi maambukizo yatakapokomeshwa kabisa.