Virusi vya corona: Je ni kwanini inakua vigumu kulinganisha viwango vya corona kimataifa?

Iliyochapishwa

Kila mtu anataka kujua iwapo nchi yake nchi yake inashughulikia vyema virusi vya corona, ikilinganishwa na nchi nyingine.Lakini lazima uhakikishe kwamba unalinganisha mambo yanayofanana.

Marekani kwa mfano, ina vifo vingi zaidi vya Covid-19 kuliko nchi nyingine kwani kufikia tarehe 20 Aprili, ilikua na jumla ya vifo 40,000.

Lakini idadi ya watu wa Marekani ni milioni 330.

Iwapo utachukua nchi kubwa zaidi za Ulaya magharibi -Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na uhispania -kwa pamoja zina idadi ya watu takriban milioni 320.

Na jumla ya vifo vilivyorekodiwa kutoka na virusi vya corona katika nchi hizo tano , kufikia Aprili 20 vilikua ni zaidi ya watu 85,000-mara mbili zaidi ya vile vya Marekani.

Kwahivyo,takwimu za kila nchi hazielezei hadithi kamili.

Ili kulinganisha kwako kuwe kwa maana, anasema Rowland Kao, profesa wa data za kisayansi katika Chuo kiku cha Edinburgh,kuna mambo makubwa mawili ya kuzingatiwa.

"Je taarifa ulizonazo zinamaanisha kitu kimoja? Na inamaana kulinganisha namba mbili iwapo ugonjwa (sababu zote zinazosababisha kusambaa kwa ugonjwa) ni tofauti.?

Kuhesabu vifo

Ngoja tutizame baadhi ya namba kwanza. Kuna tofauti katika jinsi nchi zinavyorekodi vifo vinavyotokana na Covid-19.

Ufaransa kwamfano, hujumuisha vifo vinavyotokea katika nyumba za wazee katika idadi ya vifo inavyovitangaza kila siku , lakini idadi kuu ya kila siku ya vifo Uingereza hujumuisha vifo vinavyotokea hospitalini.

Hakuna kiwango kilichokubalika cha kimataifa juu ya jinsi unavyohesabu vifo, au sababu zake.

Je mtu anahitaji kuwa amepimwa virusi vya corona ndio ahesabiwe katika takwimu,au kushukiwa na daktari pekee inatosha? Je virusi vinahitaji kuwa ndio chanzo cha kifo, au kutajwa kwa katika cheti cha kifo kuna maana?

Je unalinganisha mambo yanayofanana?

Viwango vya vifo

Viwango vya vofo vinalengwa sana, lakini kuna njia tofauti za kuvipima pia.

Moja wa uwiano wa matukio ya vifo -ya watu wote waliopatikana na virusi vya corona , ni wangapi waliougua hadi?.

Lakini nchi tofauti zinapima virusi hivyo kwa njia tofauti sana. Uingereza inawapima zaidi watu ambao wanaugua vya kutosha kiwango cha kulazwa hospitalini.Hiyo inaweza kufanya kiwango cha vifo kuonekana kuwa ni cha juu zaidi katika nchi ambayo ina mpango mpana zaidi wa kuwapima watu,

Kadri nchi inavyowapima zaidi watu, ndivyo inavyowapata watu wenye virusi vya corona wenye dalili ndogo, au labda wasio na dalili kabisa.

Kwahiyo, kiwango cha vifo katika visa vilivyothibitishwa sio sawa na kiwango cha jumla cha vifo.

Kipimo kingine ni vifo vingapi vilivyotokea ikilinganishwa na ukubwa wa idadi ya watu wa -idadi ya vifo kwa watu milioni, kwa mfano.

Lakini hilo linategemea kwa sehemu na kiwango gani cha kilichofikiwa cha mlipuko katika nchi husika. Kama kisa cha kwanza kilitokea mwanzoni katika mlipuko wa dunia, halafu ikachukua muda mrefu kwa idadi ya vifo kuongezeka.

Serikali ya Uingereza inalinganisha jinsi kila nchi ilichofanya tangu kurekodi kifo cha 50,lakin hata hilo linaleta baadhi ya matatizo.

Nchi ambayo imefikia kiwango cha kuwa na vifo 50 baadae inapaswa kuwa na muda zaidi wa kujiandaa kwa ajili ya virusi na hatimae kupunguza idadi ya vifo.

Wakati unapochunguza uhusiano huu, ni muhimu pia kukumbuka kwamba idadi kubwa ya watu wanaopata maambukizi ya corona watakua wamepona

Ushawishi wa kisiasa

Ni vigumu zaidi kuamini data zinazotoka katika nchi zenye mifumo wa siasa inayodhibitiwa.

Je idadi ya vifo vilivyorekodiwa hadi sasa katika nchi kama Uchina au Iran ni sahihi ? Kusema ukweli hatujui.

Kulingana na mahesabu kwa idadi ya watu wake, idali ya watu wa Uchina waliokufa ni ndogo sana, hata baada kutangaza idadi mpya ya juu ya kiwango cha vifo katika Wuhan kuwa ni 50%.

Je tunaweza kweli kuamini data?

Idadi ya watu

Kuna tofauti halisi katika idadi ya watu katika nchi tofauti. Eneo linalokaliwa na watu hasa ni muhimu -mambo hayo kama wastani wa umri, au mahali wanapoishi watu.

Uingereza imekua ikilinganishwa na Jamuhuri ya Ireland, lakini kuna matatizo. Ireland ina sehemu ndogo inayokaliwa na watu,na kiwango kikubwa cha asilimia ya watu wake wanaishi maeneo ya vijijini.

Inaleta maana zaidi kulinganisha Jiji la Dublin City na Counti yenye eneo la mji nchini Uingereza lenye ukubwa sawa na jiji hilo (kama Merseyside) kuliko kujaribu kulinganisha nchi mbili nzima.

Pia unahitaji kuhakikisha unalinganisha mambo yanayofanana kwa mfano muundo wa umri.

Kulinganisha viwango vya vifo kati ya mataifa ya Ulaya na Afrika huenda isiwezekane , kwasababu nchi katika mara nyingi huwa na idadi kubwa ya vijana.

Tunafahamu kuwa wazee wana uwezekano mkubwa wa kufa kutokana Covid-19.

Huduma tofauti za afya

.wa upande mwingine, nchi za Ulaya zina mifumo ya afya inayodhaminiwa vyema kuliko ile ya nchi nyingi za Afrika.

Na hilo pia limeathiri juu kiwango gani cha namna nchi inavyoathiriwa vibaya na virusi vya corona, na vile vile namna tamaduni tofauti zinavyozingatia agizo la watu kutokaribiana katika jamii.

Mifumo ya afya bila shaka inafursa muhimu katika kujaribu kudhibiti janga,lakini haiko sawa yote.

"Je watu wanatafuta matibabu ya mara kwa mara sawa, je ni rahis kwa kiasi gani kufika hospitalini, je unahitaji kulipia garama ndio utibiwe vizuri? Mambo yote haya yanatofautiana kila mahali," anasema Profesa Andy Tatem, wa Chuo kikuu cha Southampton.

Kigezo kingine ni kiwango cha maradhi ya kudumu-hii ina maana kuwa idadi ya magonjwa mengine,kama vile kisukari,magonjwa ya moyo na shinikizo la damu-ambayo watu wanaweza kuwa nayo tayari wanapopatwa na maambukizi.

Kupima

Nchi ambazo zimewapima sana watu katika mwanzo wa mlipuko, na kuwafuatilia kwa kutafuta watu waliokutana na waliopatwa na maambukizi ya mwanzo, zimeonekana kuwa na mafanikio zaidi katika kupunguza kasi ya kusambaa kwa ugonjwa hadi sasa.

Ujerumani na Korea Kusini kwa pamoja zilikua na vifo vichache kuliko nchi zilizathiriwa zaidi.

Idadi ya watu waliofanyiwa vipimo inaweza kuwa muhimu kwa takwimu katika kubashiri viwango vya chini vya vifo.

Taarifa zaidi kuhus virusi vya corona: