Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini dawa zilizotengenezwa India zinazua hofu?
Katika msimu wa majira ya baridi wa 2019, idadi ya watoto wanaoishi katika mkoa wa Jammu nchini India walianza kuugua ugonjwa ambao wengi waliouita, ugonjwa wa ajabu.
Watoto hao, walikuwa wanasumbuliwa na kikohozi na baridi, walikuwa wamembiwa watumie dawa za kikohozi na madaktari wa ndani. Badala ya kupona, waliugua zaidi tena sana, kutapika, homa kali na figo kushindwa kufanya kazi. Kufikia wakati fumbo hilo lilipotatuliwa, watoto 11, wenye umri wa kati ya miezi miwili na miaka sita, walikuwa wamepoteza maisha.
Uchunguzi uligundua kuwa sampuli tatu za dawa ya kikohozi, iliyotengenezwa na kampuni ya dawa ya Kihindi iitwayo Digital Vision, ilikuwa na diethylene glycol au DEG, kiyeyusho cha viwandani kinachotumika kutengenezea rangi, wino, na vilainishi vya breki. Kushindwa kwa figo kufanya kazi ni kawaida baada ya kunywa kilevi cha aina hii chenye sumu.
Mapema mwezi huu, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa onyo la kimataifa kuhusu dawa nne za kikohozi zilizotengenezwa India zinazohusishwa na vifo vya watoto 66 nchini Gambia.
Uchambuzi wa maabara wa sampuli za dawa hizo zilizotengenezwa na kampuni yenye uzoefu wa miaka 32 iitwayo Maiden Pharmaceuticals Limited ilithibitisha kuwepo kwa "kiasi kisichokubalika" cha diethylene glikoli na pombe nyingine yenye sumu inayoitwa ethylene glycol.
Dawa hizo zinazohusishwa na vifo vya kusikitisha vilifanya dunia kuiangazia tena na tena India kama mtengenezaji mkubwa wa dawa duniani ikijiingizia karibu dola bilioni 42 – ambazo ni nusu ya mapato yatokanayo na mauzo ya nje ya dawa.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aliwahi kunukuliwa kuisifu nchi yake kama "duka la dawa duniani".
Utaalamu wa kitamaduni wa India katika kutengeneza dawa za kurefusha maisha umesaidia kuifanya kuwa mtengenezaji wa dawa za bei nafuu na kuwa msingi wa utengenezaji wa kimataifa.
40% ya dawa za madukani na zinazouzwa Marekani (generic medicines ) na robo ya dawa zote zinazotolewa nchini Uingereza zinatoka India. Nchi inatoa theluthi mbili ya dawa za kupunguza makali ya VVU duniani kote.
Nje ya Marekani, India ina idadi kubwa zaidi ya viwanda vya kutengeneza dawa - 800 - ambavyo vinafuata mahitaji ya afya na usalama ya Marekani.
Tasnia ya dawa India imekuwa ikiendelea kukua kwa kasi ya zaidi ya 9% kila mwaka kwa karibu muongo mmoja uliopita- lakini imegubikwa na madai ya matatizo ya ubora na udhibiti dhaifu.
Wengi wanaamini kwamba India daima imekuwa ikipambana na mafuriko ya dawa ghushi, nyingi zinazouzwa katika miji midogo na vijiji. Lakini wachambuzi wanasema madaktari na wagonjwa wana uwezekano wa kuchanganya dawa zisizo na viwango na kile wanachofikiri ni dawa bandia.
Mnamo mwaka wa 2013, baada ya uchunguzi wa muda mrefu wa miaka saba, kampuni ya kubwa ya kutengeneza dawa za Kihindi ya Ranbaxy Laboratories iliamriwa kulipa faini ya rekodi ya $500m nchini Marekani, faini kubwa zaidi iliyotolewa kwa mtengenezaji wa dawa, kwa utengenezaji usiofaa, kuhifadhi na kupima dawa.
Rekodi rasmi za serikali zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2007 na 2020, zaidi ya dawa 7,500 zilizochukuliwa sampuli katika majimbo matatu kati ya 28 ya India na maeneo matatu ya muungano zilifeli majaribio ya ubora na kutangazwa kuwa dawa "sio za ubora wa kawaida" au duni, utafiti wa Dinesh Thakur, aliyekuwa mtendaji mkuu wa dawa za Kihindi ambye sasa ni mtaalam wa afya ya umma, aligundua.
Dawa hizi zilifeli vipimo vya kutokuwa na viambato vya kutosha vya kemikali, kutokuwa na uwezo wa kuyeyuka katika damu ya wagonjwa au kugundulika kuwa na vimelea. Kila sampuli iliyofeli kwa kawaida huwakilisha kundi la dawa, ambalo kwa upande wake linaweza kuingia katika mamia ya maelfu ya vidonge na sindano.
"Idadi ya jumla ya wagonjwa walioathiriwa na dawa hizo duni huenda ikafikia mamia ya maelfu, labda mamilioni katika muongo uliopita," asema Bwana Thakur, ambaye pia ni mwandishi mwenza wa The Truth Pill, kuchunguza na kufuchia yanayoendelea katika udhibiti wa dawa nchini India.
"Kwa kuzingatia dawa zilizogunduliwa kutokuwa na ubora ubora wa kawaida" katika muongo mmoja uliopita sokoni ni dhahiri kwamba idadi kubwa ya vifaa vya utengenezaji vinakiuka kabisa ubora na taratibu za udhibiti wa mchakato ambazo huunda msingi wa 'mazoea bora ya utengenezaji. '" anasema Bw Thakur.
Kwa kutumia sheria ya haki ya kupata habari, Bw Thakur aligundua maabara nyingi za serikali ya India za kupima dawa hazina vifaa muhimu. Zoezi la kuchukua sampuli za dawa, lilianza kupitia sheria ya kikoloni ya 1875 ambapo wakaguzi huchukua idadi ndogo ya sampuli kutoka sokoni.
India imekuwa ikijadili sheria ya kuziondoa dawa ambazo zimegundulika kuwa duni kutoka sokoni tangu karibu nusu karne.
"Yote iliyo nayo ni miongozo, ambayo wasimamizi wengi wa serikali wanaonekana kutoifahamu. Je, umewahi kusikia kuhusu dawa iliyorejeshwa nchini India?" Anasema Bw Thakur. Ni vigumu kuelewa ukubwa wa tatizo - viwanda vingi vya dawa nchini India ni vya kiwango cha kimataifa. Madaktari wanasema wanaamini zaidi dawa zinazotengenezwa India.
Baada ya vifo vya watoto hao nchini Gambia, India ilidai mamlaka ya udhibiti wa dawa iko "imara" na imeomba maelezo zaidi kutoka WHO kuhusu chanzo cha vifo hivyo kwa kutumia dawa ya kikohozi iliyosafirishwa nje ya nchi.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA), ambayo hudhibiti bidhaa za matibabu nchini Marekani, imetoa taarifa na barua ya onyo kuhusu hali ya ukaguzi wa makampuni yanayosambaza dawa Marekani.
Msemaji mmoja aliniambia kuwa sera zake zinahakikisha kwamba "kampuni - bila kujali ziko wapi - zinakidhi viwango vikali vya FDA vya kutengeneza dawa kwa wagonjwa wa Marekani ambazo ni za ubora wa juu, salama na zinazofaa".
Kiongozi wa sekta ya dawa, akisisitiza kutokutajwa jina, aliniambia kuwa "ingawa baadhi ya nchi zina viwango vya ubora vilivyo ngumu", dawa za India zilikuwa salama kabisa. "Hatutetei makosa," alisema, "lakini haya ni makosa".
Bw Thakur anasema: "tatizo linapaswa kutokea mara moja tu. Huwezi kucheza na maisha ya watu".