Kombe la Dunia 2026: Jinsi BBC inavyoziorodhesha timu zote baada ya mzunguko wa kwanza wa mechi

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Waandishi wa BBC Michezo
- Iliyochapishwa
- Muda wa kusoma: Dakika 7
Mabingwa watetezi Argentina walianza michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi mnono - lakini sio timu bora katika Kombe hili la Dunia kufikia sasa, kulingana na wataalam wetu wa BBC Michezo.
Tumewaleta pamoja waandishi wa habari ambao wametazama mchezo wa ufunguzi wa kila upande.
Na wameziorodhesha timu zote 48 kwenye michuano hiyo, kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho.
Je, unakubaliana na maamuzi yao? Tupatie maoni yako.
1-10

Chanzo cha picha, Getty Images
1. Ufaransa
Kundi I. Iliifunga Senegal 3-1.
Imefikia sifa iliyopewa kabla ya michuano hasa utendakazi wake katika kipindi cha pili. Uwezo mkubwa katika kila nafasi. Inastahili kupigiwa upatu.
2. England
Kundi L. iliifunga Croatia 4-2.
Ilifunga mabao manne. Wangelifunga mabao zaidi. Uchezaji mzuri wa mashambulizi ukiongozwa na Harry Kane ulichangoa matokeo hayo. Safu yao ya nyuma ililegea kidogo.
3. Argentina
Kundi G. Iliifunga Algeria 3-0.
Wana Lionel Messi na uwepo wake bila shaka unainua timu na mtazamo wake. Inatosha kuwa tatu bora.
4. Ujerumani
Kundi E. Iliishinda Curacao 7-1.
Timu yoyote inayoshinda mabao saba katika mechi yake ya ufunguzi haiwezi kupuuzwa - hata kama timu pinzani haikuwa bora
5. Marekani
Kundi D. Iliishinda Paraguay 4-1.
Haikutarajiwa kuwa miongoni mwa timu katika tano bora. Lakini uchezaji wake mzuri dhidi ya Paraguay umeimiminia sifa kedekede kutoka kwa mashabiki wa nyumbani.

Chanzo cha picha, Getty Images
6. Norway
Kundi I. Iliifunga t Iraq 4-1.
Timu ambayo imejengwa karibu na mshambuliaji Erling Haaland na imeundwa kucheza kwa uwezo wake.
7. Colombia
Kundi K. Iliifunga Uzbekistan 3-1.
Timu hii ya inashikiliwa na Luis Diaz. Colombia itazikabili timu nyingi katika michuano hii.
8. Morocco
Kundi C. Sare 1-1 na Brazil.
Ilionekana kana kwamba ingeinyuka Brazil katika dakika 20 za ufunguzi. Lakini hatimaye ilimazia udhia kwa sare katika kipindi cha pili.
9. Brazil
Kundi C. Ilitoka 1-1 na Morocco.
Mwanzo wa kusuasua ulitoacha na maswali ikiwa hii ni Brazil tuliyoijua zamani. Lakini kikosi hicho kilijizatiti na kumaliza mechi bila kushindwa.
10. Sweden
Kundi F. Iliishinda Tunisia 5-1.
Kikosi chao kina washambuliaji wawili matata na kiungo anayepania kufunga mabao wa Ligi Kuu ya England.

Chanzo cha picha, Getty Images
11-20
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
11. Australia
Kundi D. Iliichapa Uturuki 2-0.
Uchezaji wa Pacy ulihakikisha kwamba waliiweka kando timu ya Uturuki ambao, kwenye karatasi, walikuwa wakipewa nafasi kubwa kuelekea kwenye mechi.
12. Uhispania
Kundi H. Sare 0-0 na Cape Verde.
Ni mechi iliwaacha wengi vinywa wazi katika michuano hii kufikia sasa. Lakini ni timu ambayo ina uwezo wa kushinda mechi zake zilizosalia. Itafika mbali.
13. Uholanzi
Kundi F. Sare 2-2 na Japan.
Ingeliishinda mechi yake dhidi ya Japan. Mabao yangelikuwa mengi laiti safu yake ya ulinzi haingetetereka.
14. Mexico
Kundi A. Iliifunga Afrika Kusini 2-0.
Ilionekana kuwa na uwezo mkubwa dhdi ya timu ya Afrika Kusini. Kadi nyekundu ya Cesar Montes ilikuwa pigo.
15. Japan
Kundi F. Sare ya 2-2 na Uholanzi.
Lilikuwa pambano la kuvutia lililoishiwa kwa sare. Lakini tulitarajia mabao zaidi zaidi kutoka kwa Uholanzi.
16. Scotland
Kundi C. Iliichapa Haiti 1-0.
Matokeo mazuri. Utendaji mbaya. Lakini huenda hivyo ndivyo shinikizo la miaka 28 litakavyoathiri timu.
17. Cape Verde
Kundi H. Sare 0-0 na Uhispania.
Timu ya pili ya kila mtu kwenye Kombe la Dunia sasa. Sifa nyingi zinamuendea kipa mkongwe Vozinha kwa uokoaji wa kutia moyo kwa timu yake.

Chanzo cha picha, Getty Images
18. Ubelgiji
Kundi G. Sare ya 1-1 na Misri.
Ilihitaji kujifunga ili kupata sare na Mafarao wa Misri. Wametengeneza nafasi nzuri na sasa wameacha nyuma mechi yao ngumu zaidi ya makundi.
19. Misri
Kundi G. Sare ya 1-1 na Ubelgiji.
Walikuwa wanatazamia ushindi wao wa kwanza kabisa wa Kombe la Dunia. Bao la Emam Ashour lilikuwa zuri lakini walitengeneza nafasi chache.
20. Senegal
Kundi I. Ilifungwa 3-1 na Ufaransa.
Hakuna cha aibu kupoteza mechi dhidi ya Ufaransa. Hawakutoa nafasi hadi dakika ya 66 na hata wangelishinda mechi hiyo kama mkwaju wa Nicolas Jackson haukugonga mwamba katika kipindi cha kwanza.
21-30
21. Ureno
Kundi K. Sare ya 1-1 na DR Congo.
Bado wana Cristiano Ronaldo. Na timu ambayo inalemewa na hamu yake ya kuwa sehemu ya kila kitu.
22. Croatia
Kundi L. Walifungwa 4-2 na England.
Alifunga mabao mawili mazuri dhidi ya washambuliaji wakubwa England. Lakini haina safu imara ya ulinzi na anategemea sana nyota wa zamani.
23. DR Congo
Kundi K. Sare ya 1-1 na Ureno.
Ureno ilishtua kwa ulinzi mzuri na uliopangwa. Na walionekana kutisha wakati wa mapumziko.
24. Uswizi
Kundi B. Walitoka Sare ya 1-1 na Qatar.
Kukatishwa tamaa kwa kweli. Imetengeneza nafasi nyingi lakini ikapoteza sana katika ushambuliaji.
25. New Zealand
Kundi G. Sare ya 2-2 na Iran.
Uchezaji wa kusisimua ambao ulikanusha hadhi yao kama timu iliyo na nafasi ya chini zaidi ya mashindano. Wana nyota ibuka kama Eliya Just.
26. Iran
Kundi G. Sare ya 2-2 na New Zealand.
Ilionekana dhaifu mwanzoni lakini ikabahatika na kutoroka na pointi.
27. Saudi Arabia
Kundi H. Walitoka Sare 1-1 na Uruguay.
Ijipanga vizuri wakati wa mapumziko kukabiliana na tishio. Zama za kuwa vijana wa kuchapwa viboko huenda zimepungiwa mkono na Wasaudia.
28. Haiti
Kundi C. Walifungwa 1-0 na Scotland.
Iliikimbiza Scotland lakini ikhaikupata fursa ya kusawazisha.
29. Korea Kusini
Kundi A. Iliichapa Jamhuri ya Czech 2-1.
Ilijitahidi kwa muda kuidhibiti Jamhuri ya Czech lakini hadi ikafikia lengo. Huenda ikakosa nafasi hiyo katika mechi zaijazo.
30. Uruguay
Kundi H. Sare ya 1-1 na Saudi Arabia.
Alikuwa na mikwaju 28 dhidi ya Saudi Arabia kabla ya kusawazisha dakika za lala salama. Kikosi cha Marcelo Bielsa kitahitaji kufanyia kazi umaliziaji wao.

Chanzo cha picha, Getty Images
31-40
31. Uturuki
Kundi D. Ilifungwa 2-0 na Australia.
Walishangazwa na Australia katika mechi ambapo walimiliki mpira kwa zaidi ya 70%. Hakuna ndoto ya Kombe la Dunia kurejea katika mechi ya kwanza nyuma tangu kumaliza nafasi ya tatu mwaka 2002.
32. Austria
Kundi J. Iliichapa Jordan 3-1.
Ilihitaji goli la kujifunga na penati. Haina msukumo. Wanaofuata, mabingwa wa dunia Argentina.
33. Ivory Coast
Kundi E. Waliichapa Ecuador 1-0.
Aliyechanganyikiwa na kujivuna katika kopo na Equador. Utangulizi wa Amad Diallo uliongeza cheche na kuwapa matumaini ya kusonga mbele.
34. Ghana
Kundi L. Iliichapa Panama 1-0.
Ilionekana kuwa duni katika vipindi vikubwa dhidi ya Panama lakini iliokolewa na bao la ushindi dakika ya 95. Atapambana dhidi ya upinzani bora. Uingereza na Croatia kuja.
35. Algeria
Kundi J. Limepoteza kwa Argentina 3-0.
Ilikabiliwa na umahiri wa Messi. Haikufanya shambulizi lolote kulenga goli.
36. Jordan
Kundi J. Limepoteza kwa Austria 3-1.
Ilifunga bao zuri sana. Lakini haikuwahi kutishia kuipiga Austria. Watahangaika kujiondoa kwenye kundi.
37. Bosnia-Herzegovina
Kundi B. Walitoka Sare ya 1-1 na Canada.
Walitazamiwa kupata ushindi katika mechi ya ufunguzi lakini walizimwa na bao lililowekwa kimiani na Toronto.
38. Canada
Kundi B. Ilitoka Sare 1-1 na Bosnia-Herzegovina.
Inacheza mbele ya umati wa mashabiki wa nyumbani lakini ilihitaji mchezaji wa kusawazisha aliyepotoka ili kuambulia sare iliyopatikana dakika za lala salama.
39. Iraq
Kundi I. Ilifungwa 4-1 na Norway.
Sio timu nyingi zinazoweza kumzuia Erling Haaland na Iraq hakika isingeweza.
40. Equador
Kundi E. Ilifungwa 1-0 na Ivory Coast.
Walionekana kama timu ambayo haitafika kufika mbali lakini, licha ya kutengeneza nafasi chache, lakini walikatishwa tamaa kwa kipigo cha 1-0 kna Ivory Coast. Jezi zao ni nzuri hata hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
41-48
41. Jamhuri ya Czech
Kundi A. Ilifungwa 2-1 na Korea Kusini.
Hii sio Jamhuri ya Czech iliyokonga mioyo ya mashabiki katika michuano ya Euro 96.
42 Uzbekistan
Kundi K. Ilifungwa 3-1 na Colombia
Hawakuwa na ujasiri na walifurahia bao lao la kwanza kabisa la Kombe la Dunia. Lakini ilikuwa vigumu kukabiliana na Colombia.

Chanzo cha picha, Getty Images
43. Afika Kusini
Kundi A. Ilifungwa 2-0 na Mexico.
Isingeweza kuinyuka waandalizi wa michuano ya Kombe La Dunia katika mechi ya ufunguzi. Imetolewa kidogo katika shambulio. Alitoa mpira nje kiholela. Na kumaliza mechi wakiwa na wachezaji tisa.
44. Qatar
Kundi B. Ilitoka Sare ya 1-1 na Uswizi.
Sare ya bahati nzuri. Walipigwa na Uswizi ambao walikuwa na uwezo wa kuwadhibiti.
45. Paraguay
Kundi D. Walifungwa 4-1 na Marekani.
Imepigwa na Marikani na inaweza kuwa mbaya zaidi. Safi yao ya ulinzi inatia hofu kutazama.
46. Tunisia
Kundi F. Ilifungwa 5-1 na Uswidi.
Watengenezaji historia - walipomfuta kazi meneja wao baada ya mechi yao ya ufunguzi. Ndivyo Tunisia ilivyokuwa mbaya.
47. Panama
Kundi L. Walifungwa 1-0 na Ghana.
Kushiriki katika moja ya michezo mbaya zaidi ya Kombe la Dunia hadi sasa. Walikuwa wakichezea sare baada ya kupigwa bao la ushindi la Ghana dakika ya 95.
48. Curacao
Kundi E. Ilifungwa 7-1 na Ujerumani.
Kipigo cha 7-1 katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia lakini bao lao la kusawazisha dhidi ya Ujerumani angalau itakuwa wakati ambao hawatasahau kamwe.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












