Tetesi za soka Ulaya Jumapili 13.10.2024

Harry Maguire

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United wanajiandaa kumuuza mlinzi wa Uingereza Harry Maguire, 31, mwezi Januari. (Star)

Mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 24, ameamua kuhusu mustakabali wake mbali na Manchester City lakini hatajiunga na Paris St-Germain. (El Nacional)

Manchester City wana nia ya kumsajili mlinda lango wa Ureno Diogo Costa, 25, kutoka Porto kama mbadala wa muda mrefu wa Mbrazil Ederson, 31. (Football Insider)

Diogo Costa

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid na Barcelona wanavutiwa na Mhispania mwenye umri wa miaka 21 wa Benfica na beki wa zamani wa Manchester United Alvaro Fernandez Carreras. (O Jogo - in portuguese)

Liverpool pia wako kwenye mbioni kumsajili mchezaji huyo wa Benfica. (AS )

Chelsea, Tottenham na Liverpool wametuma maskauti kumtazama winga wa Borussia Dortmund na England walio chini ya umri wa miaka 21 Jamie Gittens katika wiki za hivi karibuni (Bild)

 Jamie Gittens

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, anasalia kwenye mjadala kuhusu mkataba mpya na Manchester United lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa.(Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Porto na Uhispania Samu Omorodion, 20, anasema Mungu ndiye aliyemfanya kushindwa kuhama kutoka Atletico Madrid kwenda Chelsea msimu wa joto uliopita (Metro)

Samu Omorodion

Chanzo cha picha, Getty Images

Bayern Munich hawavutiwi na mlinda lango wa Liverpool na Brazil Alisson Becker, 32, licha ya mashaka kuhusu mustakabali wa Manuel Neuer katika klabu hiyo (ESPN)

Beki wa kulia wa Chelsea na England Reece James, 24, anatazama kupitia wawakilishi wake uwezekano wa kujiunga na Barcelona au Benfica. (Football Transfers)