Anastrozole, dawa inayoweza kuzuwia kusambaa kwa saratan ya matiti

Iliyochapishwa

Dawa inayopunguza nusu ya hatari saratani ya matiti kwa mwanamke huendelea kufanya kazi muda mrehu hata mtu anapoacha kuitumia, wanasema watafiti.

Dawa hiyo kwa jina Anastrozole huzuwia uzalishwaji wa homoni za oestrogen, zinazochochea uvimbe wa saratani ya matiti.

Tayari dawa hiyo inatumiwa katika hospitali za umma, nchini Uingereza lakini watafiti katika Chuo Kikuu cha Queen Mary mjini London wanasema ni wanawake 10 wanao said only a tenth of eligible women were receiving it.

Watafiti wa saratani nchini Uingereza wanasema kuwa matokeo ya uchunguzi wao yalikua ni ya kuaminika.

Ni nani anayeweza kuitumia?

Anastrozole inaweza kutolewa tu kwa wanawake ambao hawana uwezo wa kujifungua kwani dawa hii haiwezi kuzuwia utendaji wa homoni za uzazi oestrogen miongoni mwa wanawake wenye umri mdogo.

Tayari Anastrozole inatumiwa sasa kama tiba pale saratani ya matiti inapogunduliwa, lakini majaribio ya dawa hii yanaangazia zaidi juu ya kuzuwia saratani zinazojitokeza kwa mala ya kwanza.

Utafiti wa awali , umeonyesha kuwa anastrozole huzuwia hatari ya saratani ya matiti kwa nusu wakati wa miaka mitano anayotumia dawa hiyo mwanamke.

Lakini sasa, majaribio yaliyofanyika kwa wanawake 3,864 yanaonyesha kuwa kwa wale wanaoitumia 49% walikuwa na saratani , na hata miaka saba baadae baada ya kuitumia.

Kwa maana nyingine-faida za dawa hii zinadumu.

Matokeo ya utafiti huu yalichapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet yaliowasilishwa katika Mkutano wa San Antonio wa saratani mjini Texas Marekani.

"Saratani ya matiti ni saratani inayowakumba zaidi wanawake na inaendelea kuongezeka kwa haraka ," Prof Jack Cuzick, mkurugenzi wa taasisi ya Wolfson ya dawa za kuzuia magonjwa katika Chuo Kikuu cha Queen Mary mjini London, aliiambia BBC : " Kwa sasa tuna dawa ambayo inaonekana kufanya kazi vema, ikiwa na athari kidogo."

Je dawa hii inapatikana ?

Wanawake waliozidi umri wa kuzaa walio katika hatari ya kupata saratani ya matiti , kutokana na historia ya familia na hatari nyingine , wamekua wakishauriwa kumeza dawa hiyo tangu mwaka 2017.

"Idadi ya wanaozitumia imekuwa ni ya chini sana," alisema Prof Cuzick.

"Kwa sasa ni takriban 10% ya wanawake hawa na tunafikiri idadi yao ingepaswa kuwa ni ya juu."

Moja ya masuala yanayofikiriwa ni kwamba kuna hofu ya madaktari juu ya ikiwa kweli kuna faida ya muda mrefu ya dawa hii.

Suala jingine ni athari zake kama vile maumivu ya viungo, kutokwa na mapele na kukauka kwa uke.

Hata hivyo, utafiti ulionyesha kuwa 75% ya wanawake waliopewa anastrozole waliweza kuendelea na dawa hizo vema, ikilinganishwa na 77% ambao waliombwa wameze tembe ya sukari kila siku.

Wasomi wanasema hii inaonyesha kuwa athari za dawa hii sio mbaya za kuwafanya wanawake kuacha kutumia dawa.

Dawa hii inazuia vipi saratani?

Saratani ni seli za nyama yenye afya iliyoharibiwa.

Hata hivyo, seli zenye afya haziwezi kuwa na saratani mara moja. Badala yake hupitia mchakato mbali mbali wa kumeguka ambao hatimae huzigeuza kutoka hali ya kuwa zenye afya na kuzifanya kuwa zenye saratani.

Anastrozole inaonekana kuwa na uwezo wa kuua baadhi ya seli ambazo ziliazna safari ya kuwa saratani.

"Inarudisha saa nyumba kwa miaka 20 na lazima uanzie mwanzo kutengene saratani ,jambo ambalo linaweza kuchukua muda mrefu ," Prof Cuzick aliiambia BBC

Unaweza pia kutazama:

Je hii itaondoa haja ya matibabu ya kuondolewa matiti (mastectomies)?

Hapana.

Dawa za kuzuwia saratani ya matiti inamaanisha kuondoa matiti sio njia pekee ya kuzuwia saratani.

Lakini , baadhi ya wanawake wako katika hatari ya juu zaidi ya kupata saratani ya matiti kiasi kwamba hatari inaweza kuwa kubwa zaidi hata kwa dawa.

Wanaweza kuamua kufanyiwa mastectomy ambalo bado ni chaguo bora.

Siku zijazo inatumainiwa kuwa utafiti utaweza kubashiri ni nani mwenye uwezekano mkubwa wa kunufaika na dawa au kuwa na walau kupata athari kidogo za dawa, jambo ambalo litasaidia katika uchukuaji wa maamuzi ya aina hiyo kuwa rahisi.

Je kuna dawa nyingine ?

Dawa nyingine ambazo zinaingilia homoni za oestrogen - tamoxifen - zinaweza pia kutumiwa ili kupunguza hatari za saratani ya matiti.

Kulikua na punguzo la 49% ya saratani ya matiti kutokana na dawa ya anastrozole baada ya miaka 12 (mitano ya matibabu na miaka saba baada ya matibabu yake).

Idadi sawa kwa dawa ya tamoxifen ni 28%.

Dokta Ivana Sestak, kutoka Chuo Kikuu cha Queen Mary, alisema: "Matokeo ya utafiti yanamaanisha kuwa kwa kila wanawake 29 wanaotumia dawa ya anastrozole kwa miaka mitano, mwanamke mmoja kati yao mwenye saratani ya matiti atazuiwa kwa kipindi cha miaka 12.

"takriban wanawake 49 watahitaji kutumia tamoxifen kwa miaka mitano kuzuwia saratani ya titi moja katika kipindi swa na hicho ."

Hata hivyo, tamoxifen inafanya kazi vema miongoni mwa wanawake kabla ya kufikia kipindi cha ukutokua na uwezo wa kujifungua (menopause).

Anastrozole inagarimu pauni takriban 4 kwa tembe moja.

Wataalamu wanasema nini ?

Baroness Delyth Morgan, Mkurugenzi mkuu katika kituo cha saratani ya matiti cha Breast Cancer Now, anasema: " Matokeo haya makubwa ya utafiti yanaweza kuwa muhimu sana katika kusaidia wanawake walio katika kipindi cha baada ya kuwa na uwezo wa kupata ujauzito ( post-menopausal) walio katika hatari kubwa ya kupata satarani ya matiti kuamua anastrozole ni chaguo linalofaa kwao.

" Inatia hofu kusikia kwamba huenda haiwafikii wale wote wanaotakiwa kufikiwa na tunataka kufahamu ni ukubwa gani wa tatizo

"Ni muhimu tuwahamasishe watu na kuwaelewesha juu ya chaguo hili la tiba miongoni mwa madaktari na wagonjwa ."

Unaweza pia kusoma:

Prof Charles Swanton, kutoka kituo cha utafiti wa saratani nchini Uingereza -Cancer Research UK , anayehusika na masuala ya kliniki anasema: " Hadi sasa tulifahamu tu kwamba tamoxifen ina faida za muda mrefu, kwa hivyo hili ni hakikisho kwamba utafiti ulioangaziwa zaidi katika anastrozole, ambayo ina athari mbaya chache za muda mrefu, inatoa kinga nzuri kwa wanawake miaka baada ya kusitisha matumizi ya dawa.

"Madaktari bado wanaweza kuamua kwamba tamoxifen inafaa zaidi kwa baadhi ya wanawake, lakini ni vizuri kwamba kuna chagu la dawa .

Unaweza pia kutazama: