Luka Romero: 'Messi mpya' aliezinduliwa kushiriki katika ligi ya Uhispania akiwa na umri wa miaka 15 pekee

Luka Romero

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Akiwa na umri wa miaka 15 na siku 219 , alizaliwa mwezi January tarehe mosi 2004 - na alishriki kwa mara ya kwanza katika ligi kuu akiichezea timu yake Real Club Deportivo Mallorca.
Iliyochapishwa

Luka Romero ni mchezaji mchanga kwa mambo mengi ikiwemo kuwa mchezaji wa kulipwa.

Lakini Romero ambaye ana umri wa miaka 15 ameweka historia kwa kuwa mchezaji mchanga zaidi kushiriki katika ligi kuu ya Uhispania.

Akiwa na umri wa miaka 15 na siku 219 , alizaliwa mwezi Januari tarehe mosi 2004 - na alishiriki kwa mara ya kwanza katika ligi kuu akiichezea timu yake Real Club Deportivo Mallorca.

Na alicheza dhidi ya Real Madrid , katika mechi ambayo mji huo wa Uhispania ulipata ushindi wa 2-0.

Alizaliwa nchini Mexico na kusafiri na familia yake yote hadi nchini Uhispania wakati alipokuwa na umri wa miaka 3.

Babake , aliyekuwa kiungo wa kati wa Argentina Diego Romero , alikua akiichezea timu ya Mexico Alacranes de Durango wakati Luka alipozaliwa.

Luka Romero anachezea timu ya vijana ya kandanda nchini Argentina

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Luka Romero anachezea timu ya vijana ya kandanda nchini Argentina

Wengi wamekuwa wakimuita 'Messy wa Mexico' huku katika mataifa ya latini wakimuita 'Messi mpya'.

Romero alihitaji ruhusa maalum katika ligi ili kuweza kushiriki kama mchezaji wa kulipwa wakati ambapo ana umri wa miaka 15.

Kinda huyo anafikiria kuwa mmoja ya washambuliaji bora katika kizazi chake.

Barcelona na Real Madrid tayari wameonesha hamu ya kumsajili mchezaji huyo lakini kwa sasa anaichezea Real Mallorca.

Katika timu hiyo anashirikiana na mchezaji wa Colombia Juan Camilo 'Cucho' Hernandez.

Je ni nani aliyempatia jina hilo la utani?

Sio mwengine isipokuwa mchezaji matata wa Brazil Dani Alvez, wakati huo akiichezea klabu ya Barcelona alimpatia jina 'Messi mpya'.

Klabu ya Messi Barcelona imeorodheshwa katika nafasi ya pili katika jedwali la ligi ya Uhispania, nyuma ya Real Madrid

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Klabu ya Messi Barcelona imeorodheshwa katika nafasi ya pili katika jedwali la ligi ya Uhispania, nyuma ya Real Madrid

Yeye na Messi wote wanacheza kama washambuliaji, wana vipaji vya kutamba na mpira na wana umbo la watu wafupi:-

Kijana huyo ana urefu wa sentimita 167 huku mchezaji huyo wa Barcelona akiwa na urefu wa sentimita 1.70.

Vyombo vya habari vinasema kwamba Messi aliwasili Barcelona akiwa na umri wa miaka 13 na urefu wa sentimita 143.

Kucheza katika fukwe za bahari

Wanasema kwamba Romero na Alves walikutana katika ufukwe wa bahari wa Formentera, ikiwa ndo kisiwa kidogo zaidi miongoni mwa visiwa vya Balearic.

'Nilikuwa na umri wa miaka 12 wakati huo'

Walicheza pamoja na kupigiana pasi , na Alves akaridhishwa na uwezo wa kijana huyo, ''walipiga picha naye . Yeye ndio Messi mpya''

wakati utaamua iwapo Luka ndio atakeychukua mikoba ya Leo