Cristiano Ronaldo na Lionel Messi: Ni nani atakayewarithi nyota wa mchezo wa kandanda duniani muongo huu?

BBC Sport Insight banner
Iliyochapishwa

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi walitawala muongo wa 2010 kwa ubora wao .

Hakuna hata mtu mmoja aliyewakaribia. lakini mshambuliaji wa Juventus Ronaldo 34 na mshambuliaji wa Barcelona Messi 32 hawaezi kuendelea kusakata soka kwa maisha yao yote.

Hivyobasi tunauliza ni nani atakayewarithi?

Waandishi wa BBC Sport na wachambuzi wa soka wanachanganua ni wacchezaji gani wanaoweza kuchipuka na kuwa viongozi katika soka katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Short presentational grey line

Kylian Mbappe (Paris St-Germain na Ufaransa )

Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbappe ana thamani ya £215m kulingana na shirika la CIES football observatory

Siku ya kuzaliwa: Tarehe 20 Disemba 1998

Nafasi: Mshambuliaji

Mwandishi mkuu wa BBCsport Phil McNulty:

Mbappe ana umri wa miaka 21 na tayari ni mshindi wa kombe la dunia akiichezea Ufaransa nchini Urusi 2018 na anaonekana mchezaji bora anayechipuka wa soka .

Akiwa amebarikiwa na kasi na uwezo wa kufunga magoli ni vigumu kusema kwamba huenda akabadilika katika muongo unaokuja.

Ni mrithi wa moja kwa moja ambaye atasalia baada ya Messi na Ronaldo kuondoka huku mataji yote yakiwa mbele yake.

Mbappe kwa sasa anaichezea klabu ya PSG , akiongoza lengo lao la kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya ambalo limekuwa likiwaponyoka.

Lakini thamani yake itaonekana atakapoondoka - pengine msimu ujao kwa kile ambacho kinatarajiwa kuwa dau litakalovunja rekoodi ya dunia na klabu ya Real Madrid inayoongozwa na Zinedine Zidane.

Uchambuzi wa Mwandishi wa soka wa Ulaya Kristof Terreur:

Mbappe lazima aorodheshwe juu , kwasababu tayari yuko hapo , . tayari yeye ni miongoni mwa wachezaji bora duniani akiwa na umri wake mdogo.

Ulimwengu upo katika miguu yake .

Ni tabia mbaya pekee itakayomzuia kushinda mataji yote . Ana kila kinachohitajika kuchukua matangazo ya Messi na Ronaldo: Ana kasi, uwezo na nidhamu ya kushinda mataji hayo.

Beki wa zamani wa klabu ya Manchester City Micah Richards anasemaje?:

Punde Messi na Ronaldo watakapoondoka katika soka, Mbappe ndie mchezaji atakayeshinda mataji makubwa ya soka .

Sidhani iwapo atafunga magoli mengi kama wachezaji hao wawili kwasababu idadi yao ya magoli ipo juu sana lakini ndie mchezaji bora aliye na umri mchanga ambaye nimewahi kumuona.

Iwapo Sergio Aguero anaondoka na wanataka wachezaji wawili , ningependelea Gabriel Jesus na Mbappe hata iwapo itatugharimu £150m.

Short presentational grey line

Joao Felix (Atletico Madrid na Portugal)

Joao Felix

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Felix alishinda taji la Golden Boy trophy mbele ya Jadon Sancho na Kai Havertz

Alizaliwa tarehe 10 Novemba 1999

Nafasi: Mshambuliaji

Uchambuzi wa muandishi wa soka ya Uhispania Guillem Balague:

Akiwa na umri wa miaka 20, Atletico Madrid ilitumia £113m kumsaini Joao Felix kutoka Benfica mnamo mwezi Julai .

Ulikuwa uhamisho wa tatu kwa ukubwa duniani ukilipiwa kijana ambaye wakati huo alikuwa amecheza mechi 43 za kikosi cha kwanza cha timu.

Mwandishi mkuu wa kitengo cha BBC Sport Phil McNulty:

Felix tayari anaandaliwa nchini Portugal kumrithi Ronaldo , akimaliza mwaka kwa kutuzwa taji la Golden Boy mjini Dubai.

Mshambuliaji huyo ana kipaji cha kupamba mashindano makubwa wakati klabu yake itakaposhiriki pamoja na taifa lake kwa miaka mingi.

Short presentational grey line

Jadon Sancho (Borussia Dortmund & England)

Jadon Sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sancho aliondoka Man City na kujiunga na Dortmund katika uhamisho uliogharimu £8m Agosti 2017

Alizaliwa tarehe 25 Machi 2000

Nafasi: Winga

Uchambuzi wa Mchezaji wa zamani wa Tottenham Jermaine Jenas:

Jadon Sancho yuko katika klabu anayoichezea kwa sasa Dortmund kwasababu anaifanyia mambo makubwa.

Nimekuwa nikimtazama na amekuwa akiimarika kila uchao- amefunga magoli ametoa pasi za kusababisha magoli na ana motisha wa juu.

Je anahitaji kufanya nini? Tayari anaonekana yuko vizuri kila wiki.

Amekuwa na tatizo kidogo la nidhamu ambalo pengine anahitaji kuliangazia , lakini mbali na hilo ni mchezaji aliekamilika na maalum..

Short presentational grey line

Ansu Fati (Barcelona na Uhispania U21)

Ansu Fati

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Fati alianza kuichezea klabu kubwa ya barcelona mwezi Agosti mwaka jana

Alizaliwa tarehe 31 Octoba 2002

Nafasi : Winga

Mwandishi wa soka Uhispania Guillem Balague:

Ana kasi ya umeme, anaweza kutamba na mpira , na mfungaji mzuri mwenye uelewa mzuri na malengo ya kandanda ya siku zijazo.

Mtoto huyo wa muhamiaji kutoka Guinea Bissau , aliwasili nchini Uhispania na mamake akiwa na umri wa miaka sita baada ya babake kuwasili mapema akitafuta kazi.

Ana kipaji kutoka mwanzo , alisajiliwa na Barcelona katika taasisi yao ya soka akiwa na umri wa miaka 10 na msimu huu alijiunga na timu kubwa bila hata kuchezeshwa katika timu ya Barcelona B.

Akiwa na umri wa miaka 17 ni mchezaji mdogo zaidi kuweza kufunga katika timu kubwa ya Barcelona.