Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 22.11.2019: Mourinho, Ibrahimovic, Pochettino, Torreira, Neymar

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Tottenham, Jose Mourinho anatafakari uwezekano wa kuvunja jaribio la AC Milan la kumsajili mshambulizi mahiri wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, na kumleta nyota huyo London. (Telegraph)
Kocha wa Lille Christopher Galtier amemkosoa Mourinho kwa kuwanunua maafisa wawili katika kundi lake la wakufunzi kujiunga na Spurs. (RMC Sport via Evening Standard)
Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini anasema Mourinho sio rafiki wala adui wake . (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino ananyatiwa na Bayern Munich kushikilia wadhifa wa kocha wa kudumu. (Sky Sports)
Barcelona pia wanamtaka raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 47, ambaye aliwahi kuwa meneja wa mahasimu wao Espanyol. (Sun)
Kiungo wa kati wa Arsenal na raia wa Uruguay Lucas Torreira, 23, hajapinga uwezekano wa kuondoka klabu hiyo mwezi Januari. (Sport 860 via Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji anasalia kuwa kipaumbele cha Manchester United mwezi Januari- na mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer amekuwa akifanya mikutano ya kila mwezi na timu yake ya usajili katika juhudi ya kufikia orodha ya wachezaji watatu. (Evening Standard)
Winga wa Celtic raia wa Norway Mohamed Elyounoussi, 25, amedokeza kuwa Stuart Armstrong atahamia Parkhead kwa mkopo. (The Scotsman)
Sunderland huenda wakamsajili beki wa kushoto na kulia wa Uingereza Marcus Maddison,26, kwasababu Peterborough wamekataa kupunguza bei yao. (Newcastle Chronicle)

Chanzo cha picha, Reuters
Mlinzi wa Uhispania Gerard Pique, 32, anasema atamaliza taaluma yake ya michezo katika klabu ya Barcelona ifikapo mwaka 2022. (Mundo Deportivo)
Mkufunzi wa Paris St-Germain, Thomas Tuchel anasema hakuridhishwa na hatua ya mshambuliaji Neymar kwenda Madrid kuhudhuria kombe la Davis. (Marca)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Real Madrid, Gareth Bale anasema kuwa mchezaji hujaathiriwa na hatua ya mashabiki wa Los Blancos kufuatia piacha aliyopiga akiwa na bendera iliyoandikwa, 'Wales. Golf. Real Madrid. Katika usanjari huo'. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Ubelgiji imeadhibiwa na Uefa kutokana na dosari ambapo mlinzi wa Hertha Berlin, Dedryck Boyata alivalia fulana ya mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi wakati wa kusherehekea ushindi wao dhidi ya Urusi katika mechi ya kufuzu kwa michuano ya Euro 2020. (Daily Mail)
TETESI ZA SOKA ALHAMISI

Chanzo cha picha, Reuters
Mkufunzi mpya wa Tottenham Jose Mourinho atajaribu kumsajili tena mshambuliaji wa zamani wa Spurs Gareth Bale, 30, kutoka Real Madrid. (AS - in Spanish)
Mourinho pia anamlenga kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Portugal Bruno Fernandes, 25, beki wa kati wa Benfica Mreno Ruben Dias, 22, na kiungo wa kati wa Manchester United Mserbia Nemanja Matic, 31. (Independent)
Beki wa zamani wa Arsenal Martin Keown anaamini kuwa Gunners inahitaji kumuajiri mkufunzi wa zamani Tottenham, Mauricio Pochettino. (Mail)
Barcelona na Bayern Munich ziko tayari kumpatia kazi Mauricio Pochettino. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, bado hajasaini mkataba mpya na Arsenal kwa sababu anasubiri uamuzi wa Barcelona. (Mirror)
Real Madrid imemuunga mkono Bale na kupuuzilia mbali tetesi kuwa nyota huyo huenda akaondoka klabu hiyo mwezi Januari, licha ya mchezaji huyo kupiga picha akiwa na bendera ilioandikwa 'Wales. Golf. Madrid. katika usanjari huo,' akiwa katika jukumu la kimataifa. (Marca)
Real Madrid imetaja hatua ya Bale "Wales. Golf. Madrid. " kama ''utani uliovuka mpaka." (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United inatafakari uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Roma wa miaka 33, mzaliwa wa Boznia, Edin Dzeko. (ESPN)
Kiungo wa kati wa England, James Maddison, 22, kusaini mkataba mpya na Leicester licha ya azma kuu ya Manchester United ya kutaka kumnunua. (Manchester Evening News)
Ajenti wa Zlatan Ibrahimovic, Mino Raiola amekutana na AC Milan kuhusu uwezekano wa mshambuliaji huyo wa Sweden kurejea katika klabu hiyo. (Corriere dello Sport - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal imeongeza juhudi za kumnunua mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Erling Haaland, 19, baada ya kumwalika baba ya mchezaji huyo, Alf-Inge Haaland ambaye alikuwa kiungo wa kati wa zamani wa Leeds, kutembelea ukumbi wao wa mazoezi. (Sport Bild, via Metro)
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer pia anapania kumsaini Haaland. (Mail)
Juventus inatarajiwa kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kupuuzilia mbali Real Madrid na kujiunga na klabu hiyo ya Serie A kutoka Paris St-Germain. (Tuttosport, via Sky Sports)

Chanzo cha picha, Reuters
Mpango wa Inter Milan wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, huenda ukatibuliwa na matakwa ya mchezaji huyo. (La Gazzetta dello Sport, via Mail)
Chelsea imeungana na Liverpool na Napoli katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Genk na Norway, Sander Berge,21. (goal)
Arsenal na Liverpool wamehusishwa na tetesi ya usajili wa mshambuliaji wa Red Bull Salzburg ya Ujerumani Karim Adeyemi,17. (Transfermarkt, via HITC)












