Jose Mourinho: Kwa nini mtu huyu ana ushabiki mkubwa, mbali na kuwa mkufunzi?

Chanzo cha picha, Tottenham Hotspur
Iwapo ungemuuliza yeyote kumtaja mkufunzi wa soka , Jose Mourinho bila shaka angekuwa miongoni mwao mahala popote duniani.
Huenda Jurgen Klopp ama Pep Guardiola walipata ufanisi mkubwa nchini England katika siku za hivi karibuni, lakini hata mafanikio yao hayajawapatia umaarufu mkubwa kama ule wa Mourinho.
Ni kweli kwamba umaarufu wake mwingi unatokana na mafanikio yake - jinsi alivyoshinda mataji zaidi ndio jinsi uwepo wake umeonekana katika sekta ya kandanda duniani.
Lakini Mourinho ni nyota aliye na ushabiki mwingi kwa kiwango ambacho Jurgen klopp na Pep Guardiola hawawezi kufikia. Na hii ndio sababu.
Anaweza kujikuza

Chanzo cha picha, Mark Leech/Offside
Mourinho ni miongoni mwa watu maarufu katika soka . Amekuwa maarufu tangu 2004 wakati alipoingia uwanjani katika uwanaja wa Old Trafford baada ya timu yake ya Porto kuiondoa Man United katika kombe la mabingwa Ulaya.
Wakati huo tayari alikuwa amejikuza kwa kuvalia koti refu jeusi, kitambaa shingoni na nywele zilizonyolewa.
Picha za zamani zaidi wakati wake alipokuwa naibu mkufunzi akiwa Barcelona wakati alipopendelea kuvalia nguo kubwa ya mazoezi inaonyesha jinsi alivyoimarika kimavazi kufikia sasa.
Matamshi yake

Chanzo cha picha, BJORN LARSSON ROSVALL
Umaarufu wa Mourinho sio jinsi anavyoonekana kama The Special one lakini kile anachosema.
Utambulisho wake kama mtu maalum ni zaidi na sawa na anavyotoa mzaha kwamba sasa sio maalum sana kila timu yake inaposhindwa.
Lakini licha ya kukana kuwa mtu maalum, jina hilo la The Special One limesalia kwa muda mrefu - ikiwa ni miaka 15 tangu alipojitambulisha kwa kulitumia kwa mara ya kwanza.
Hilo linaonyesha jinsi alivyo na kipawa cha maneno , wakati ambapo anafanya kazi kwa kutumia lugha ya pili.
Ukweli ni kwamba hakusema kwamba yeye ni maalum - nukuu nzima kutoka kwa mazungumzo na vyombo vya habari ilikuwa ikisema, tafadhali musiniite mjeuri, lakini mimi ni bingwa wa Ulaya na nadhani ni mtu maalum.
Vyombo vya habari vya Uingereza vilipenda sana neno hilo. Katika mechi yake ya kwanza ya ligi ya Uingereza , timu yake ya Chelsea ilitoka sare ya 0-0 dhidi ya Spurs, na alisema: Walileta basi na kuliwacha basi hilo mbele ya goli.
Ni matamshi haya ambayo yamepata umaarufu wa kuegesha basi ikimaanisha kushiriki mechi kwa lengo la kulinda lango pekee.
Mourinho amefanikiwa kutumia kipawa cha lugha ili kuvuruga maoni ya matokeo mabaya ya mechi.
Baada ya sare ya 0-0 dhidi ya West Ham , kwa mfano alisema hii sio ligi bora duniani, hii ni soka kutoka karne ya 19 , na baadaye alisema: Mimi ni mkufunzi wa mojawapo ya klabu bora duniani lakini pia mimi ni miongoni mwa wakufunzi bora duniani.
Alimaanisha kwamba kushindwa kwa klabu hiyo kupata ushindi hakuwezi kufanya alaumiwe kwa kuwa ameweza kufanikiwa pakubwa.
Alituma ujumbe mzito baada ya kuondoka katika klabu hiyo akisema: Najivunia kumaliza katika nafasi ya pili nikiifunza Man United katika ligi ya Premia.
Ni taarifa ambayo imejadiliwa kwa kipindi kirefu na kila mara klabu hiyo inapopokea matokeo mabaya matamshi hayo ya Mourinho yanazidi kujadiliwa.
Hisia zake

Chanzo cha picha, Serena Taylor
Wakufunzi wengine kama vile - Arsene Wenger hujitokeza akilini - ni wataalamu wa kuficha hisia zao , huwezi kuwadadisi, wakitoa hisia zao kulingana na mazingiya yao.
Lakini Jose Mourinho sio miongoni mwao.
Hujiingiza katikati ya kila habari

Chanzo cha picha, Getty Images













