Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 21.11.2019: Bale, Aubameyang, Dzeko, Maddison, Haaland, Giroud, Mbappe, Morelos

Jose Mourinho

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jose Mourinho amrithi Mauricio Pochettino baada ya kupigwa kalamu Tottenham
Iliyochapishwa

Mkufunzi mpya wa Tottenham Jose Mourinho atajaribu kumsajili tena mshambuliaji wa zamani wa Spurs Gareth Bale, 30, kutoka Real Madrid. (AS - in Spanish)

Mourinho pia anamlenga kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Portugal Bruno Fernandes, 25, beki wa kati wa Benfica Mreno Ruben Dias, 22, na kiungo wa kati wa Manchester United Mserbia Nemanja Matic, 31. (Independent)

Beki wa zamani wa Arsenal Martin Keown anaamini kuwa Gunners inahitaji kumuajiri mkufunzi wa zamani Tottenham, Mauricio Pochettino. (Mail)

Barcelona na Bayern Munich ziko tayari kumpatia kazi Mauricio Pochettino. (Sun)

Mauricio Pochettino

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vilabu vya Barcelona na Bayern Munich ziko tayari kumpatia kazi Mauricio Pochettino.

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, bado hajasaini mkataba mpya na Arsenal kwa sababu anasubiri uamuzi wa Barcelona. (Mirror)

Real Madrid imemuunga mkono Bale na kupuuzilia mbali tetesi kuwa nyota huyo huenda akaondoka klabu hiyo mwezi Januari, licha ya mchezaji huyo kupiga picha akiwa na bendera ilioandikwa 'Wales. Golf. Madrid. katika usanjari huo,' akiwa katika jukumu la kimataifa. (Marca)

Real Madrid imetaja hatua ya Bale "Wales. Golf. Madrid. " kama ''utani uliovuka mpaka." (ESPN)

Gareth Bale

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Real Madrid imemuunga mkono Bale na kupuuzilia mbali tetesi kuwa nyota huyo huenda akaondoka klabu hiyo mwezi Januari

Manchester United inatafakari uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Roma wa miaka 33, mzaliwa wa Boznia, Edin Dzeko. (ESPN)

Kiungo wa kati wa England, James Maddison, 22, kusaini mkataba mpya na Leicester licha ya azma kuu ya Manchester United ya kutaka kumnunua. (Manchester Evening News)

Ajenti wa Zlatan Ibrahimovic, Mino Raiola amekutana na AC Milan kuhusu uwezekano wa mshambuliaji huyo wa Sweden kurejea katika klabu hiyo. (Corriere dello Sport - in Italian)

Zlatan Ibrahimovic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ajenti wa Zlatan Ibrahimovic, Mino Raiola akutana na AC Milan

Arsenal imeongeza juhudi za kumnunua mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Erling Haaland, 19, baada ya kumwalika baba ya mchezaji huyo, Alf-Inge Haaland ambaye alikuwa kiungo wa kati wa zamani wa Leeds, kutembelea ukumbi wao wa mazoezi. (Sport Bild, via Metro)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer pia anapania kumsaini Haaland. (Mail)

Juventus inatarajiwa kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kupuuzilia mbali Real Madrid na kujiunga na klabu hiyo ya Serie A kutoka Paris St-Germain. (Tuttosport, via Sky Sports)

Kylian Mbappé

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Juventus kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kujiunga nao

Mpango wa Inter Milan wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, huenda ukatibuliwa na matakwa ya mchezaji huyo. (La Gazzetta dello Sport, via Mail)

Chelsea imeungana na Liverpool na Napoli katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Genk na Norway, Sander Berge,21. (goal)

Mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, 27, na beki wa kushoto na kulia wa Scotland left-Andrew Robertson, 25, watakosa meshi ya Liverpool dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi.(Sky Sports)

Mohamed Salah

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mohamed Salah atakosa meshi ya Liverpool dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi

Arsenal na Liverpool wamehusishwa na tetesi ya usajili wa mshambuliaji wa Red Bull Salzburg ya Ujerumani Karim Adeyemi,17. (Transfermarkt, via HITC)