Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Morgan Rogers kujiunga na Arsenal

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Morgan Rogers
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Kiungo wa kati wa Aston Villa na England Morgan Rogers anataka kuhamia kwa mabingwa wa Ligi ya Premia Arsenal msimu ujao, huku The Gunners wakimfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuwa nyota wanayemlenga zaidi (Talksport)

Mshambulizi wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 28, yuko tayari kukatwa mshahara ili kujiunga na Tottenham kwa pauni milioni 40 msimu huu baada ya mkopo wake wa Barcelona. (i Paper)

Tottenham wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Newcastle Sandro Tonali kwa ada ya karibu £85m, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, 26, angependelea kujiunga na wapinzani wao Arsenal. (Daily Mail - Subscription Required)

Beki wa Chelsea, 26, Trevoh Chalobah, ambaye alichelewa kuitwa kwenye kikosi cha England kwenye Kombe la Dunia, anasakwa na mkufunzi wa Como Cesc Fabregas. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chalobah

Bayern Munich na Tottenham zote zinamtaka beki wa Juventus Bremer, 29, lakini Mbrazil huyo ana furaha kusalia Turin. (Gianluca DiMarzio - In Itali)

Barcelona wamefanya mkabala wa kushtukiza kuona kama mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 32, atakuwa tayari kuondoka Bayern Munich na kujiunga na klabu hiyo ya Uhispania. (Sport - In Spanish)

Manchester United wako tayari kukubali hasara kwa kiungo wa kati wa Uruguay Manuel Ugarte, 25, ili kumuuza msimu huu wa joto. (Sun)

Leeds United wamekaribia kukamilisha dili la kiungo wa kati wa Southampton na Ireland Kaskazini Shea Charles, 22, ambaye amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake wa sasa. (TeamTalks)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ugarte

Brighton wanakaribia kuinasa saini ya beki wa Venezia na Austria Michael Svoboda mwenye umri wa miaka 27. (Sky Sports)

Arsenal bado hawajakubali dili la kumsajili kiungo wa kati wa Kolkheti na Georgia Andria Bartishvili, huku Liverpool na Paris FC pia wakitafuta njia ya kumnunua kinda huyo mwenye umri wa miaka 17. (Talksport)

Beki wa West Ham na Ufaransa Jean-Clair Todibo, 26, anakaribia kukubali kuhamia Fenerbahce kwa mkopo baada ya The Hammers kushuka daraja. (Star - In Turkey ),