Matokeo ni batili - Odinga azungumza kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa ameshindwa

Mshindi wa pili katika uchaguzi wa urais nchini Kenya amezungumza na kusema “Takwimu zilizotangazwa na Bw Chebukati ni batili na ni lazima zifutiliwe mbali na mahakama.

Moja kwa moja

  1. Ruto aipongeza Tume ya uchaguzi na kuahidi 'serikali yenye uwazi'

    William Ruto- Rais Mteul Kenya
    Maelezo ya picha, William Ruto- Rais Mteul Kenya

    Ruto aipongeza Tume ya uchaguzi na kuahidi 'serikali yenye uwazi'

    William Ruto amehutubia taifa baada ya kutangazwa mshindi.

    "Watu wa Kenya wameonyesha kutuamini, sio kwa sera za makabila yetu, bali kwa kile tulichokuwa tunakizungumzia."

    Pia amepongeza mchakato wa uchaguzi, licha ya kwamba mapema kidogo kundi la makamishna walisema hawakuweza kushiriki katika utoaji wa matokeo.

    "IEBC ambayo ni tume ya uchaguzi ilitushangaza sote…ninataka kupongeza IEBC kwa kuongeza uaminifu wa viwango vingine.

    "Wafula Chebukati ambaye ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndiye shujaa wetu."

    Ruto aahidi 'serikali yenye uwazi'

    Alipokuwa anazungumza, Bw. Ruto amesema anafahamu kuwa anakabiliwa na wapinzani wengi baada ya kupata zaidi kidogo tu ya asilimia 50 ya kura.

    "Nitaendesha serikali ya uwazi, na ya kidemokrasia," amesema.

    "Ninataka kuwaahidi watu wote wa Kenya, kwa njia yoyote waliyopiga kura kwamba hii itakuwa serikali yao.

    "Nataka kuwaambia wapinzani kwamba hawana chochote cha kuogopa, hakuna nafasi ya kulipiza kisasi. Ninafahamu kabisa kwamba nchi yetu ipo katika hatua ambayo tunahitaji juhudi za pamoja ili kusonga mbele.’’

    "Hatuna haja ya kuangalia nyuma. Hatuna haja ya kunyoosheana vidole. Hatuna tamaa wala haja ya kutupiana lawama. Ni lazima tushirikiane kwa ajili ya Kenya inayofanya kazi, ya kidemokrasia na yenye ustawi."

    Soma zaidi:

  2. Viongozi mbalimbali wampongeza William Ruto

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amempongeza Rais Mteule wa Kenya William Ruto.

    Bw Abiy ameweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa anatazamia kufanya kazi naye kwa karibu.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Rais wa Zimbambwe Emmerson Mnangagwa amempongeza William Ruto kwa kuchaguliwa kuwa Rais ajaye wa tano wa Kenya.

    Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter:

    Hongera William Ruto kwa kuchaguliwa kuwa Rais ajaye wa Kenya.

    Sina shaka ataitumikia nchi yake, watu wake na bara letu kwa upekee.

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Waziri wa kwanza azungumza

    Waziri wa Utalii wa Kenya Najib Balala amekuwa waziri wa kwanza katika baraza la mawaziri kumpongeza William Ruto.

    Balala amekuwa miongoni mwa mawaziri ambao hawakumfanyia kampeni waziwazi mgombea wa Rais Uhuru Kenyatta Raila Odinga.

    Wakati wa kampeni yake, Bw Ruto aliwashtumu mawaziri waliokuwa wakihudhuria kampeni za mpinzani wake kwa kuingiza baraza la mawaziri kisiasa kinyume na sheria inayowazuia watumishi wa umma kujihusisha na siasa.

    Huu hapa ni ujumbe wa Balala:

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

  3. Habari za hivi punde, Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Ruto anazungumza baada ya kutangazwa mshindi

    William Ruto- Rais mteule Kenya

    Chanzo cha picha, William Ruto/ FACEBOOK

    Maelezo ya picha, William Ruto- Rais mteule Kenya

    Ruto anazungumza baada ya kutangazwa mshindi

    William Ruto baada ya kutangazwa kuwa mshindi, sasa anazungumza:

    ‘’Ni jioni nzuri sana... mamlaka yote ni ya watu wa Kenya. Nataka kumshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa.

    ‘’Najua kulikuwa na utabiri kwamba hatungefika hapa - lakini kwa sababu kuna Mungu mbinguni, tuko hapa. Shukrani nyingi ziende kwa watu wa Kenya.’’

    Soma zaidi:

  4. Habari za hivi punde, Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Vurugu zaibuka katika kituo cha kutolea matokeo

    Kufuatia tangazo la makamishna wanne wa uchaguzi kwamba hawawezi kushiriki katika kutangaza matokeo, kumekuwa na matukio ya fujo katika kituo cha matokeo.

    Ilionekana kuwa msaidizi wa Raila Odinga alijaribu kumzuia mkuu wa tume ya uchaguzi kutoa hotuba. Kisha polisi mmoja akamsimamisha na kumpeleka eneo lililo mbali na jukwaa.

    Soma zaidi:

  5. Habari za hivi punde, Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Tume Huru ya uchaguzi ya Kenya (IEBC) yagawanyika

    Baadhi ya Makamishna wa Tume Huru ya uchaguzi Kenya
    Maelezo ya picha, Baadhi ya Makamishna wa Tume Huru ya uchaguzi Kenya

    Makamishna wanne wa Tume Huru ya uchaguzi ya Kenya(IEBC) wamefanya mkutano na waandishi wa habari wakisema ‘’hawawezi kumiliki matokeo’’ kwa sababu ya ‘’hali isiyoeleweka ya jinsi awamu hii imekuwa ikishughulikiwa’’.

    Soma zaidi:

  6. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022:Timu ya Raila inasema imeshindwa kuthibitisha matokeo ya mwisho

    Ajenti mkuu wa uchaguzi wa Raila Odinga Saitabao Kanchory akizungumza na vyombo vya habari

    Chanzo cha picha, Citizen

    Maelezo ya picha, Ajenti mkuu wa uchaguzi wa Raila Odinga Saitabao Kanchory akizungumza na vyombo vya habari

    Wakala mkuu wa uchaguzi wa Raila Odinga Saitabao Kanchory amesema timu yake haijaweza kuthibitisha baadhi ya matokeo na hivyo basi haitamtaka mgombea wao wa urais kufika katika kituo cha kujumlisha matokeo.

    Katika maelezo mafupi ambayo yaliwasilishwa kwa watangazaji wa ndani, aligusia baadhi ya dosari za uchaguzi.

    Bw Kanchory alikuwa ameandamana na baadhi ya viongozi kutoka muungano wa Bw Odinga wa Azimio, Gavana wa Kisumu Anyang Nyong'o na Gavana Mteule wa Siaya James Orengo.

    Soma zaidi:

  7. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Raila Odinga yuko wapi?

    Raia wakiwa nje ya ofisi ya rais

    Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wanashangaa alipo Raila Odinga, kabla ya kutangazwa kwa rais mteule.

    Bado hajafika katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura kama ilivyo kwa mpinzani wake mkuu William Ruto.

    Kulikuwa na shamrashamra fupi wakati msafara wa magari uliposimama katika kituo cha matokeo, lakini ikafahamika kwamba alikua mama yake Ruto.

    Walinzi nje ya ofisi ya Bw Odinga katika kitongoji cha Karen jijini Nairobi wamemweleza mwandishi wa BBC Mercy Juma kwamba mgombea huyo bado yumo ndani ya eneo hilo.

    Timu za waandishi wa habari zimekita kambi kwenye kizuizi karibu na ofisi yake.

    Kuna uvumi kwamba huenda Odinga asifike katika kituo cha kujumlisha kura kipindi hiki.

    Hata hivyo, hakuna sharti kwamba wagombea wote wawepo kwenye eneo la utangazaji wa matokeo na Odinga hakuwepo katika eneo hilo la ujumlishaji wa matokeo wakati alipowania urais mara nne.

    Soma zaidi:

  8. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Foleni ndefu zashuhudiwa kwenye barabara kadhaa

    Foleni ndefu zimeshuhudiwa katika barabara mbalimbali kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

    Vyombo vya habari vya ndani na Wakenya kwenye mtandao wa Twitter wanaripoti msongamano wa magari katika sehemu za jiji hilo.

    Huku Jumatatu ikiwa siku ya kazi, wakati wa mchana Wakenya wengi wamejipata wakiwa katika harakati za kukimbilia kwenda majumbani mwao mapema, wengine wakiwa na wanafunga biashara zao, huku raia wengine wakiwa wanakimbilia kununua bidhaa.

    Kuna msongamano wa magari kwenye barabara kuu mbili za Nairobi.

    Barabara ya Mombasa na barabara ya Thika.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Soma zaidi:

  9. Ukraine yashambulia makao makuu ya mamluki ya Wagner Urusi mashariki

    Popasna ipo karibu na Severodonetsk (kama inavyoonekana kwenye picha) - sasa iko mikononi mwa Warusi baada ya mapigano makali

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Popasna ipo karibu na Severodonetsk (kama inavyoonekana kwenye picha) - sasa iko mikononi mwa Warusi baada ya mapigano makali

    Ndege za kijeshi za Ukraine zimeshambulia makao makuu ya kundi la jeshi la mamluki la Wagner mashariki mwa Ukraine, ripoti zinasema.

    Shambulio hilo la Popasna liliripotiwa na Serhiy Hayday, Gavana wa Ukraine wa mkoa wa Luhansk, na waandishi kadhaa wanaoripoti kuhusu mambo ya vita wanaounga mkono Kremlin.

    Idadi ya waliopoteza maisha bado haijulikani na maelezo yanabaki kuwa ya mchoro.

    Picha zinazosemekana kuonesha uharibifu ziliwekwa kwenye mtandao wa Telegram.

    Kundi la Wagner limekuwa likihusishwa na uhalifu wa kivita.

    Kundi hilo lilitumwa Crimea na eneo la Donbas nchini Ukraine mwaka 2014, wakati wanajeshi wanaoungwa mkono na Kremlin walipowatimua wanajeshi wa Ukraine katika maeneo ambayo baadaye walitangaza kuwa sehemu ya Urusi.

    Vikosi vya Wagner pia vimetumwa Syria, Libya, Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Kremlin haikubali kuwepo kwa kundi la Wagner, lakini ujasusi wa Magharibi unahusisha kundi hilo na Yevgeny Prigozhin - jina la utani ‘’mpishi wa Putin’’ kwa sababu biashara yake ya upishi imemsaidia kwa muda mrefu Rais Vladimir Putin na vikosi vya jeshi.

    Bw Prigozhin, kama maafisa wengine wengi wa Urusi, yuko chini ya vikwazo vya Magharibi.

    Kundi la Wagner linajulikana kama PMC - kampuni binafsi ya kijeshi.

    Lakini ni mamluki wanaofadhiliwa na serikali ambao wanafanya kazi kwa maslahi ya Kremlin, wataalamu wa Magharibi wanasema.

    Wameshutumiwa kwa uhalifu wa mara kwa mara wa kivita na ukiukaji wa haki za binadamu.

    Soma zaidi:

  10. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Matokeo yanavyoweza kuwa

    Ukumbi wa IEBC
    Maelezo ya picha, Ukumbi wa IEBC

    Tunapoendelea kusubiri matokeo,nikukumbushe tu kwamba kuna matokeo matatu yanayoweza kutokea baada ya kura ya Jumanne iliyopita:

    • William Ruto atangazwe kuwa mshindi

    • Raila Odinga atangazwe kuwa mshindi

    • Uchaguzi uingie katika duru ya pili ya uchaguzi

    Duru ya pili ya uchaguzi itatangazwa ikiwa hakuna hata mmoja kati ya wagombea aliyepata kura zaidi ya 50% ya kura - hii inawezekana kwa kuwa kuna wagombea wengine wawili wanaowania urais, ingawa kwa pamoja wameonesha kupata chini ya 1% ya kura.

    Soma zaidi:

  11. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Tume ya uwiano inawataka Wakenya kudumisha amani

    Tume ya uwiano nchini Kenya imewataka Wakenya kudumisha amani wakati na baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais.

    Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imewataka Wakenya wote “kukubali matokeo na kuruhusu masuala yoyote yatakayojitokeza kushughulikiwa na mahakama zetu”.

    ‘’Tangazo hili muhimu litatoa mwelekeo wa mustakabali wa nchi yetu lakini sio hali ya kufa na kupona. Kenya itasonga mbele kwa mafanikio bila kujali nani ni rais kwa hivyo watu wetu hawana haja ya kuwa na wasiwasi,’’ anasema mwenyekiti wa NCIC Samuel Kobia.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    NCIC ilianzishwa kufuatia ghasia zilizofuatia uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo watu wasiopungua 1,200 waliuawa na 600,000 kukimbia makazi yao baada ya madai ya kuibiwa kwa kura.

    Soma zaidi:

  12. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Matokeo kutangazwa saa mbili zijazo

    Tangazo la IEBC
    Maelezo ya picha, Tangazo la IEBC

    Maandalizi yanaendelea kupamba moto kwa ajili ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

    Watu ndani ya kituo kikuu cha kutangazwa kwa matokeo wamekuwa wakifurahia kwaya zinazoendelea tumbuiza - lakini burudani hii italazimika kuendelea kwa saa mbili zaidi.

    Tume ya uchaguzi imesema kwamba matokeo ya mwisho yatatoka saa 15:00 kwa saa za ndani (12:00 GMT).

    Soma zaidi:

  13. Matokeo ya Uchaguzi Kenya: Wagombea wa uchaguzi Wajakoyah na Mwaure wawasili katika ukumbi wa Bomas

    wajakoyah

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, David Mwaura na George Wajackoyah wamekuwa wakipata kura chache zaidi katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais

    Wagombea wa urais George Wajackoyah wa chama cha Roots na David Mwaure wa chama cha Agano Party wamewasili katika ukumbi wa Bomas, inakofanyika shughuli ya kujumlisha kura, huku rais mteule akitarajiwa kutangazwa rasmi

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Wawili hao wamekuwa wakipata idadi ya chini ya kura katika matokeo ya awali tya urais ambayo yamekuwa yakitangazwa na vyombo vya habari - wakiwa na chini ya 1% ya kura kila mmoja

    Bw Mwaure alikubali kushindwa Jumapili na kumuidhinisha Naibu Rais William Ruto.

  14. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Wakenya wasubiri kutangazwa kwa Rais Mteule

    IEBC
    Maelezo ya picha, Ukumbe wa Bomas of Kenya, umeshuhudia vikundi vya kwaya za kidini ambazo zimekuwa zikitumbuiza Wakenya huku wakisubiri matokeo ya uchaguzi mkuu

    Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya(IEBC), imekamilisha mchakato wa uhakiki wa kura za urais

    Macho yote sasa ni kwa Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati wakimsubiri atangaze matokeo.

    Wakati hayo yakijiri viongozi wa vyama vyote vya kisiasa walio katika ukumbi wa Bomas ambao ndio kituo kikuu cha kujumlisha kura wameonekana wakicheza nyimbo za dini, zinazotumbuizwa na kwaya katika ukumbi huo .

    Tume ya uchaguzi inatarajiwa kumtangaza rais mteule leo. Tume hiyo ina siku hadi saba za kutangaza matokeo baada ya uchaguzi kufanyika. Uchaguzi mkuu wa Kenya ulifanyika Jumanne wiki iliyopita tarehe 9 Agosti.

    Iwapo mshindi wa urais atatangazwa leo,na iwapo hapatakuwa na pingamizi ya ushindi wake mshindi anafaa kuapishwa tarehe 30 mwezi huu wa Agosti.

    Unaweza pia kusoma:

    • Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022:Kenya huenda ikamjua rais ajaye leo-IEBC itamtangaza Raila Odinga ama William Ruto?
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Raila Odinga na William Ruto katika ushindani mkali
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Waliokuwa vigogo na kutupwa nje kwa muda wachaguliwa tena
  15. Matokeo ya Uchaguzi Kenya:Picha katika ukumbi wa Bomas,Kisumu na Eldoret

    Kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya ,baadhi ya wakazi katika maeneo ya Kisumu na Eldoret wamefurika barabarani kuanza kusherehekea huku wakitaka mshindi kutangazwa.Katika Picha:

    th
    TH
    TH
    TH
    TH
    TH
    TH
    TH
    TH
    TH
    TH
    th
    th
    th
    th
    th
  16. Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Fatuma Achani gavana pekee wa kike pwani ya Kenya

      • Author, Aboubakar Famau
      • Nafasi, BBC News, Mombasa
    Fatuma

    Chanzo cha picha, Fatuma Achani/Facebook

    “Haikuwa kazi rahisi, nilinyanyaswa nilitukanwa na watoto wangu, ilikuwa sio siasa tena, lakini ni mashambulizi dhidi yangu”

    Vikundi vya ngoma za kienyeji vilikuwa kila pembe ya kaunti ya Kwale, huku wengine wakitanda nje ya uzio wa jengo ambalo Tume Huru ya Uchaguzi ilikuwa ikiendesha shughuli zake.

    Sherehe zilizokuwa zikiendelea ilikuwa ni furaha ya ushindi wa kiti cha gavana wa Kwale, ambacho mara hii kimekwenda kwa Fatuma Achani, mwanamke pekee aliyeibuka kidedea katika nafasi hiyo Pwani ya Kenya.

    Achani, mwenye miaka 38, anasema ingawa alikuwa naibu gavana katika serikali iliyopita, lakini kampeni ya kutaka nafasi ya gavana haikuwa kazi rahisi.

    “Nilitukanwa, nilidhalilisha mitandaoni pamoja na watoto wangu, haikuwa siasa tena, ilikuwa ni mashambulio binafsi,” anasema Achani.

    Achani anaongeza kusema kuwa, kwa sababu yeye ni mwanamke katika jamii ambayo haijazoea kuongozwa na wanawake, yeye aliongeza juhudi kuliko wapinzani wake wa kiume, ili kuthibitisha uwezo wake wa kazi.

    Wakiwa wamebeba bango lenye picha ya Achani, mmoja wa wafuasi wake alisema, “Tunafuraha kupata ushindi. Tuna matumaini mama atatuwakilisha vizuri.”

    BBC

    Wanawake kadhaa wameingia katika kinyang’anyiro cha nafasi ya gavana katika eneo la Pwani, lakini ni Achani pekee ndie aliyeweza kuwafuta machozi wenzake walioshindwa. Mpaka sasa kuna magavana saba wanawake walioshinda katika maeneo mengine kati ya 47 nchi nzima.

    Safari inaonekana bado ndefu kwa kina mama hawa, ambao licha ya kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika siasa, lakini bado wana kazi kubwa ili kujihakikishia ushindi.

    Unaweza pia kusoma:

    • Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022:Kenya huenda ikamjua rais ajaye leo-IEBC itamtangaza Raila Odinga ama William Ruto?
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Raila Odinga na William Ruto katika ushindani mkali
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Waliokuwa vigogo na kutupwa nje kwa muda wachaguliwa tena
  17. Matokeo ya uchaguzi 2022:Maafisa Zaidi wa polisi waingia katika ukumbi wa Bomas

    BBC
    Maelezo ya picha, Katika ukumbi wa IEBC, maafisa wa usalama wanaonekana kuimarisha ulinzi

    Usalama umeimarishwa ndani na nje ya ukumbi wa Bomas unaotumiwa kama kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura za urais .

    Jumatatu asubuhi maafisa zaidi wa polisi waliingizwa katika ukumbi huo ili kuimarisha usalama huku tume ya Uchaguzi na mipaka IEBC ikitarajiwa kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais hii leo .

    Ukumbi wa IEBC
    Maelezo ya picha, Ukumbi wa IEBC

    Shughuli katika ukumbi huo zimeendelea kwa utulivu baada ya visa kadhaa vya makabiliano hapo awali kati ya maajenti wa miungano ya Kenya kwanza na Azimio wakati mchakato wa kuhakiki kura ukiendelea.

    Wakati huo huo madawati yote ya uhakiki wa matokeo ya kura yamebaki matupu, eneo la wanadiplomasia linakaliwa na watu wengine kinyume na siku za nyuma wakati yamekuwa wazi.

    Unaweza pia kusoma:

    • Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022:Kenya huenda ikamjua rais ajaye leo-IEBC itamtangaza Raila Odinga ama William Ruto?
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Raila Odinga na William Ruto katika ushindani mkali
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Waliokuwa vigogo na kutupwa nje kwa muda wachaguliwa tena
  18. Vikosi vya Burkina Faso vimeshutumiwa kwa mauaji ya raia 40

    Reuters

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Jeshi la Burkina Faso ilikanusha shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu

    Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Burkina Faso yamelishutumu jeshi kwa kuwauwa zaidi ya watu 40 kaskazini mwa nchi.

    Shirika hilo la Collective Against Immunity and Stigmatisation of Communities limesema kumekuwa na visa vingi vya utekaji nyara na kufuatiwa na mauaji ya watu kunyongwa kiholela

    Ilisema miili ya wahasiriwa ilipatikana kwenye barabara kati ya Taffogo na Bouroum ikiwa imefungwa macho na mikono .

    Kundi jingine la kutetea haki za binadamu, Observatory of Human Dignity, lilisema wengi wa wahasiriwa walikuwa Wafulani - kabila lenye Waislamu wengi wa wafugaji wanaohamahama.

    Jeshi la Burkina Faso limekanusha madai ya mara kwa mara ya ukiukaji wa haki.

    Kisa hicho kinasemekana kutendeka mapema mwezi huu katika kijiji cha Taffogo huko Tougouri.

    Jeshi la Burkina Faso limekuwa likipambana na uasi wa makundi yanayoshukiwa kuwa na uhusiano na al-Qaeda au kundi la Islamic State, ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 na kuwalazimu takriban watu milioni 1.9 kuondoka makwao.

  19. Urusi yaapa kuimarisha uhusiano na Korea Kaskazini

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Urusi imeapa "kuimarisha uhusiano [wake] wa kina na wa kujiboresha " na Korea Kaskazini, amesema Rais wake Vladimir Putin.

    Katika barua iliyotumwa kwa mwenzake Kim Jong un siku ya ukombozi wa Pyongyang, Bw Putin alisema hatua hiyo itakuwa kwa maslahi ya nchi zote mbili.

    Kwa upande wake, Bw Kim alisema urafiki kati ya mataifa yote mawili ulianza katika Vita vya Pili vya Dunia na ushindi dhidi ya Japan.Aliongeza kuwa "uhusiano wao wa kirafiki" utaimarika zaidi.

    Kulingana na ripoti ya chombo cha habari cha serikali ya Korea Kaskazini KCNA, Bw. Putin alisema uhusiano huo uliyoimarishwa "utaendana na maslahi ya nchi hizo mbili."

    Katika barua yake, Bw Kim alisema urafiki wa Russia na Korea Kaskazini "ulioanzishwa katika vita dhidi ya Japan" "umeimarishwa na kuendelezwa karne baada ya karne" .

    Iliongeza "ushirikiano wa kimkakati na wa kimbinu, uungaji mkono na mshikamano" kati ya nchi hizo mbili "umewekwa kwenye hatua mpya ya juu, katika mstari wa pamoja kwa ajili ya kukatisha tamaa tishio la kijeshi la vikosi vya uhasama na uchochezi".

    Pyongyang haikutambua majeshi hayo kwa majina, lakini neno hilo limetumiwa mara kwa mara na Korea Kaskazini kurejelea Marekani na washirika wake.

    Umoja wa Kisovyeti ulikuwa mshirika mkuu wa Korea Kaskazini, ukitoa ushirikiano wa kiuchumi, mabadilishano ya kitamaduni na misaada.