Matokeo ni batili - Odinga azungumza kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa ameshindwa

Mshindi wa pili katika uchaguzi wa urais nchini Kenya amezungumza na kusema “Takwimu zilizotangazwa na Bw Chebukati ni batili na ni lazima zifutiliwe mbali na mahakama.

Moja kwa moja

  1. Ukraine yatangaza shambulio kubwa dhidi ya kambi ya wanajeshi wa Urusi

    Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine viliharibu kambi ya wanajeshi wa Urusi huko Nova Kakhovka, mkoa wa Kherson, kulingana na huduma ya vyombo vya habari ya Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine na huduma ya mpaka wa serikali.

    Video inayoonyesha athari ya shambulio la kombora imeibuka mtandaoni.

    Upande wa Ukraine unakadiria mauaji ya kati ya 10-15 wa Urusi.

    BBC hatahivyo haiwezi kuthibitisha kwa haraka habari katika hali ya mapigano.

  2. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa hii leo.

  3. Kuna ukweli kuhusu madai ya makosa ya hesabu ya matokeo ya uchaguzi?

      • Author, Peter Mwai
      • Nafasi, BBC Reality Check

    Makamishna wanne wa tume ya uchaguzi waliojitenga na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa hapo jana Jumamatu wamedai kwamba matokeo hayo sio sahihi kwasababu Jumla ya asilimia iliyotolewa inapita asilimia 100.

    Ni madai ambayo yamewekwa mitandaoni na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Amollo Odinga.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Asilimia 100.10% inaweza kuelezewa kupitia hesabu.

    Kwasababu ya kukadiria juu au chini wakati unapopiga hesabu za kila asilimia mpaka nafasi mbili za desimali, uwezekano wa kupata chini au zaidi ya 100% hutokea.

    Unaweza tu kupata asilimia halisi ya 100% unapofanyia kazi sehemu zote za desimali.

    Kulingana na matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa IEBC, mshindi William Ruto alipata 50.49% ya kura, Odinga (48.85%), George Wajackoyah (0.44%) na Mwaure Waihiga (0.23%).Jumla ni 100.01%.

    Nambari zote zimekadiriwa hadi nafasi mbili za desimali na 0.01% ya ziada inaonekana kwa sababu nambari ya desimali kabla ya kukadiriwa ilikuwa tano au zaidi.

    Makamishna hao hao pia walitoa madai yasiyo ya kweli kuwa 0.01% ya jumla ya kura halali zilizopigwa zingewakilisha kura 142,000 na kusema "italeta mabadiliko makubwa katika matokeo."Hatahivyo, idadi sahihi itakuwa kura 1,420.

    Hata hivyo kuna tofauti ya kura 110 kati ya jumla ya kura halali zilizotangazwa na mwenyekiti, 14,213,137, na jumla ya kura zilizopatikana na wagombea wote wanne.

    Soma zaidi:

    • Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Raila Odinga apinga matokeo ya uchaguzi
    • Makamishna wa Tume ya Uchaguzi waliojitenga na matokeo wazungumza
  4. Je wafuasi wa Rais Mteule wa Kenya wana hofia ushindi wake kupingwa mahakamani?

    Je wafuasi wa Rais Mteule wa Kenya wana hofia ushindi wake kupingwa mahakamani?

    Tazama video hii...

    Maelezo ya video, Je wafuasi wa Rais Mteule wa Kenya wana hofia ushindi wake kupingwa mahakamani?

    Soma zaidi:

  5. Rais wa Kenya akaa kimya baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

    Ni wiki moja sasa tangu Wakenya walipomuona ama kumsikia Rais Uhuru Kenyatta.

    Alizungumza kwa ufupi na wanahabari Jumanne iliyopita baada ya kupiga kura katika mji aliozaliwa nje kidogo ya mji mkuu, Nairobi.

    Alikuwa anamuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kuchukua nafasi yake badala ya naibu wake, William Ruto, ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Agosti 9.

    Wawili hao walipochukua madaraka mwaka wa 2013 walikuwa na uhusiano wa karibu, kila mara wakiitana “kaka”, wakipiga makofi hadharani baada ya kutaniana na wakati mwingine kuwa na mahusiano ya karibu sana.

    Haijulikani kwanini walikosana, lakini uhusiano wao ulizidi kuwa mbaya na kuzorota kuelekea siku za kuelekea uchaguzi wa mwaka huu ambapo walirushiana maneno makali.

    Licha ya Bw Kenyatta kutokuonekana hadharani, serikali yake ilitangaza leo kwamba mchakato wa kumpata Rais mpya bado unaendelea.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Soma zaidi:

  6. Matokeo ni batili - Odinga azungumza na kumshutumu Chebukati kwa uonevu

    Raila Odinga amehutubia taifa

    Chanzo cha picha, AFP/Getty

    Maelezo ya picha, Raila Odinga amehutubia taifa

    Raila Odinga amehutubia taifa baada ya kushindwa katika uchaguzi

    Mgombea wa pili wa Urais Raila Odinga, ambaye muungano wake wa Azimio La Umjoa unadai kulikuwa wizi wa kura katika matokeo ya Jumatatu, amezungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kwake.

    Akihutubia taifa kutoka Makao Makuu ya vyombo vya habari vya Azimio jijini Nairobi, anasema: “Mamilioni ya Wakenya walijitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wao... Lakini jana demokrasia yetu ilikabiliwa na msukosuko mkubwa.’’

    Raila Odinga amshutumu Chebukati kwa uonevu

    ‘’Kwa kuepuka shaka, nataka kurudia: Tunakataa kabisa na bila kusita matokeo ya urais yaliyotangazwa jana na [Mwenyekiti wa tume Huru ya uchaguzi] Bw Chebukati,’’ Bw Odinga asema.

    Pia anamshutumu mwenyekiti wa uchaguzi kwa kuwadhulumu wanachama wengine wa Tume hiyo ambao hawakukubaliana naye.

    Soma zaidi:

  7. Kenya yawahakikishia raia usalama na kuwataka kurejelea shughuli za kibiashara

    Kitengo cha juu cha usalama nchini Kenya chazungumza
    Maelezo ya picha, Kitengo cha juu cha usalama nchini Kenya chazungumza

    Kitengo cha juu cha usalama nchini Kenya kimewahakikishia raia usalama kufuatia hofu ya kuwepo kwa ghasia zinazohusiana na uchaguzi.

    Mamlaka imewataka Wakenya kuanza tena shughuli zao za kibiashara wakisema nchi iko salama na usalama umeimarishwa katika kipindi hiki.

    Wingu la wasiwasi limetanda nchini kufuatia machafuko yaliyotangulia baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais Jumatatu.

    Kamati ya ushauri ya usalama wa taifa nchini imechukua hatua ya kuondoa hofu ya kutokea ghasia kufuatia mzozo wa matokeo ya uchaguzi wa Rais.

    Timu hiyo ilisema hali ya usalama nchini iko shwari baada ya tathmini ya awali mapema Jumanne na mamlaka imechukua hatua kuhakikisha nchi iko salama.

    Kulikuwa na ripoti za ghasia katika maeneo ya mji mkuu Nairobi na katika mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya baada ya waandamanaji kupinga kuthibitishwa kwa William Ruto kama mshindi wa uchaguzi wa Agosti 9.

    Chaguzi za urais zilizoshindaniwa hapo awali zimesababisha ghasia zilizogharimu maisha ya watu wengi na uharibifu wa mali.

    Soma zaidi:

  8. Viongozi kadhaa kutoka ngome ya Raila wasihi wafuasi wao kudumisha amani

    Gavana wa Kisumu Anyang Nyongo

    Chanzo cha picha, Gavana wa Kisumu Anyang Nyongo ?TWITTER

    Maelezo ya picha, Gavana wa Kisumu Anyang Nyongo

    Gavana wa Kisumu Anyang Nyong'o amewataka wakaazi wa Kisumu kusitisha maandamano yao yanayoendelea na kusalia kwa amani huku uongozi wa Azimio ukitoa mwanya wa kusonga mbele.

    Nyong'o kupitia taarifa iliyotolewa Jumanne asubuhi aliwaambia wakazi hao kusalia na amani hata iwapo tangazo la William Ruto kuwa Rais mteule litapingwa.

    “Tafadhali sitisha aina yoyote ya maandamano na uharibifu wa mali tunapojiandaa kuwajulisha hatua inayofuata,” alihimiza.

    Nyong'o aliendelea kuwaomba wakaazi hao kuwa na imani na uongozi wa Azimio wanapojitahidi kuhakikisha mgombea wao anapata haki.

    Wakati huo huo, Gavana mteule wa eneo la Homa Bay Mheshimiwa Gladys Wanga, ametoa taarifa akishirikisha wafuasi wa eneo lake uchungu na kukatishwa kwa matumaini ambako pamoja na wafuasi wa Muungano wanapitia kwa sasa.

    Bi Wanga amewahakikishia wafuasi kwamba timu yao ya sheria inashughulikia kile kilichotokea kwa madai kwamba makosa yaliyotokea ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.

    Pia amewataka wakazi kuwa watulizu, kumuunga mkono Raila Odinga na kumuombea.

    Aidha, aliwahakikishia wafuasi wa Raila kwamba timu ya wanasheria ya Azimio la Umoja itafanya yote wanayoweza ili kuhakikisha mshindi sahihi wa uchaguzi anatangazwa.

    ‘’Zoezi hilo lilikuwa na dosari kubwa na kuthibitishwa na makamishna wanne ambao ndio wengi wa tume ya IEBC. Kwa hivyo suala hili halijaisha,’’ Gladys Wanga ameandika.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Soma zaidi:

  9. Raila Odinga kuvunja ukimya mchana wa leo baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais

    Kuna uvumi kwamba huenda akapinga matokeo mahakamani (picha kutoka maktaba)

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Kuna uvumi kwamba huenda akapinga matokeo mahakamani (picha kutoka maktaba)

    Mshindi wa pili katika uchaguzi wa urais nchini Kenya anatazamiwa kuzungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatatu.

    Imetangazwa kuwa Raila Odinga atahutubia wanahabari saa 14:00 saa za eneo (11:00 GMT).

    Hii ilikuwa mara ya tano kwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 77 kugombea nafasi hiyo ya juu na wengi wanadhani itakuwa mwisho wake.

    Salim Lone, aliyekuwa mshauri wa Bw Odinga, aliambia BBC Jumanne kwamba bosi wake wa zamani alifananisha mchakato mzima na ‘’ubakaji wa demokrasia’’.

    Kabla ya Bw Ruto kutangazwa na mkuu wa tume ya uchaguzi kuwa mshindi Jumatatu kwa asilimia 50.49 ya kura, maajenti wa uchaguzi wa Bw Odinga walikuwa wamesema hawakuweza kuthibitisha matokeo.

    Pia yalitiliwa shaka na makamishna wanne kati ya saba wa uchaguzi, ambao waliambia waandishi wa habari hawakuweza ‘’kuchukua umiliki wa matokeo’’.

    Soma zaidi:

  10. Kundi la waangalizi wa uchaguzi wa Kenya ELOG lasema matokeo ya IEBC yanaendana na yake

    Wakenya

    Kundi la waangalizi wa uchaguzi wa Kenya ELOG limesema matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa Jumatatu na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati yanaendana na hesabu walizofanya kundi hilo,zilizoonesha ushindi wa Bwana William Ruto na kuyataja matokeo hayo kuwa ya wazi.

    Matokeo huru yaliyofanywa na kundi hilo la waangalizi yalimuweka William Ruto mbele kwa asilimia 50.7, ilhali matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC yalionesha Bwana Ruto alishinda kwa asilimia 50.49 dhidi ya mshindani wake wa karibu Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga aliyepata asilimia 48.7 ya kura hilo.

    Kulingana na ELOG, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati alikuwa na haki kikatiba kama afisa mkuu wa kitaifa wa Uchaguzi kutangaza mshindi wa uchaguzi wa Rais.

    Makamishna wanne kati ya saba wa tume ya IEBC walikataa kutambua matokeo ya urasi wakihoji hayakuwa wazi.

    ELOG ikiongozwa na mwenyekiti wake Anne Ireri, imewataka walio na mashaka na matokeo ya uchaguzi mkuu kupeleka pingamizi la kisheria katika mahakama ya juu na kutoa wito kwa wanasiasa wa pande zote kusalia watulivu. Aidha ELOG imesema inaendelea kufuatilia kwa karibu mazingira ya kisiasa Kenya.

    Kundi hilo la waangalizi liliendesha zoezi huru la kuhesabu na kujumuisha matokeo kutoka kwa waangalizi elfu moja waliofuatilia matokeo kutoka kwa vituo kadhaa kote nchini.

    Kwa jumla,kundi hilo lilikuwa na waangalizi elfu tano kote nchini kufuatilia uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika Agosti Tisa.

    Muungano wa Azimio unaoongozwa na Bwana Odinga umekataa kutambua matokeo ya Urais na baadhi ya wandani wake wamesema wanakusudia kuelekea katika mahakama ya juu kupinga matokeo yaliyompa ushindi Bwana Ruto.

    Soma zaidi:

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • Shangwe tele baada ya ushindi wa William Ruto
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • William Ruto: Muuza kuku aliyepanda ngazi hadi kushinda urais Kenya
  11. Vita vya Ukraine: Milipuko yatikisa ngome ya Urusi katika Crimea ya Ukraine

    Kulikuwa na milipuko ya mara kwa mara katika kambi ya jeshi la Urusi mapema Jumanne

    Chanzo cha picha, SCIAL MEDIA

    Maelezo ya picha, Kulikuwa na milipuko ya mara kwa mara katika kambi ya jeshi la Urusi mapema Jumanne

    Kambi ya kijeshi huko Crimea inayokaliwa na Urusi imekumbwa na msururu wa milipuko, ikiripotiwa kuwaacha takriban watu wawili wakwa wamejeruhiwa.

    Maafisa wa Urusi walisema moto ulisababisha milipuko katika ghala la silaha eneo la Dzhankoi kaskazini mwa Crimea.

    Moto pia ulionekana kwenye kituo kidogo cha umeme.

    Kilichosababisha milipuko hiyo hakijulikani, lakini wiki iliyopita ndege za kivita za Urusi ziliharibiwa katika shambulio dhahiri la Ukraine kwenye pwani ya Crimea.

    Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema moto huo ulizuka katika eneo la kuhifadhia silaha kwa muda karibu na kijiji cha Maiske mwendo wa 06:15 saa za Moscow (03:15 GMT) na kwamba chanzo kinachunguzwa.

    Wizara hiyo ilisema hakukuwa na ‘majeruhi mbaya’, lakini afisa mmoja aliyeteuliwa na Urusi alisema watu wawili wamejeruhiwa.

    Mshauri wa ofisi ya rais wa Ukrain Mykhailo Podolyak alielezea tukio hilo kama ‘’kuondoa wanajeshi’’, akionyesha kuwa milipuko hiyo haikutokea kwa bahati mbaya.

    Kiongozi wa Tatar wa Crimea, Refat Chubarov, pia alielezea milipuko hiyo kama ‘pigo’.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Crimea ilitekwa kutoka Ukraine na kisha kutwaliwa na Urusi mapema 2014, na wakati majeshi ya Urusi yalipoanzisha uvamizi mpya mwezi Februari walitumia vituo vyao kwenye rasi kukamata maeneo makubwa ya kusini mwa Ukraine.

    Soma zaidi:

  12. Wafuasi wa Raila Odinga: Kulikuwa na 'Ubakaji wa demokrasia' katika uchaguzi wa Kenya

    Wafuasi wa Odinga

    Mgombea wa upinzani na Waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila hajazungumza hadharani baada ya hasimu wake William Ruto kutangazwa kuwa Rais mteule.

    Haijawa wazi iwapo Bw Odinga atawasilisha mashitaka kupinga matokeo ya uchaguzi Mshauri wa zamani wa Bw Odinga, Salim Lone, ameieleza BBC maoni yake kuhusu kupoteza ushindi kwa mkuu wake wa zamani.

    Ujumbe wa nukuu ’’Nimekuwa na mazungumzo marefu nay eye na amesema wazi kwamba anadhani ni kama huu ulikuwa ni ubakaji wa demokrasia.

    Kwahiyo, haoni kuwa hii inakubalika kabisa’’ Unumbe wa nukuu : ‘’Tatizo letu ni kwamba huu ni uchaguzi wa nne wenye ushindani mkali na huu ulikuwa mbaya zaidi wakati tulidhani kuwa hatimaye huu ungekuwa bora zaidi.

    Sio wa kuaminika kwa sababu makamishna wanne kati ya saba hawakusaini katika tangazo kuhusu kutangazwa kwa Bw Ruto kwamba alichaguliwa kisheria ." Mgombea mwenza wa Bw Odinga Martha amesema kwenye Twitter kwamba : "haijaisha hadi iishe’’

  13. Afisa wa uchaguzi wa Kenya aliyetoweka apatikana amefariki - ripoti

    TH

    Aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi katika kituo cha kupigia kura katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, amepatikana akiwa amefariki siku chache baada ya familia yake kuripoti kuwa ametoweka, vyombo vya habari vya Kenya vinaripoti.

    Mwili wa Daniel Mbolu Musyoka ulipatikana katika msitu wa Loitoktok chini ya Mlima Kilimanjaro karibu na mpaka na Tanzania, ripoti zinamnukuu mkuu wa polisi akisema.

    Mwili huo ulitambuliwa na dada zake wawili, gazeti la Daily Nation linaongeza. Inasema mwili huo ulipatikana na wafugaji na ulikuwa na alama zinazoonyesha alifanyiwa mateso.

    Bw Musyoka alikuwa afisa msimamizi katika eneo la Embakasi Mashariki jijini Nairobi.

    Kutoweka kwake kuliripotiwa Ijumaa iliyopita na tume ya uchaguzi, ambayo ilisema alitoweka akiwa kazini katika kituo cha kujumlisha kura.

    Soma zaidi:

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • Shangwe tele baada ya ushindi wa William Ruto
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • William Ruto: Muuza kuku aliyepanda ngazi hadi kushinda urais Kenya
  14. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Kwa picha ngome ya Raila Odinga Kisumu ni shwari baada ya matokeo

    BBC

    Biashara nyingi zimefungwa mjini Kisumu katika ngome ya Raila Odinga magharibi mwa Kenya, mwandishi wa BBC Roncliffe Odit anasema.

    Bw Odinga alishindwa kwa kura chache katika uchaguzi wa urais na William Ruto - ambaye alitangazwa mshindi Jumatatu kwa 50.49% ya kura.

    Baadhi ya maandamano katika ngome za Bw Odinga yalifuatia tangazo la Jumatatu la Bw Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

    Bw Odinga bado hajazungumza hadharani kuhusu matokeo ya uchaguzi huo. Jumanne asubuhi, ni shwari katika jiji, kama picha hizi kutoka mitaani zinavyoonyesha:

    BBC
    BBC
    BBC

    Soma zaidi:

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • Shangwe tele baada ya ushindi wa William Ruto
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • William Ruto: Muuza kuku aliyepanda ngazi hadi kushinda urais Kenya
  15. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Marekani yasema kutangazwa kwa ushindi wa Ruto ni 'hatua' muhimu

    Reuters

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, William Ruto alitangazwa kama mshindi kwa kupata 50.49% ya kura

    Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umewapongeza Wakenya kwa uchaguzi wa amani na kuzitaka pande zote kushirikiana kutatua hofu yoyote iliyosalia kwa amani.

    Ulisema kutangazwa kwa William Ruto kama rais mteule wa Kenya ni ‘’hatua muhimu katika mchakato wa uchaguzi”.

    “Kusonga mbele, tunaziomba pande zote kushirikiana kwa pamoja kutatua hofu zilizosalia kuhusu uchaguzi huu kwa njia zilizopo za utatuzi ” uliongeza.

    Ubalozi huo umewataka viongozi wa kisiasa kuwatolea wito wafuasi wao kuendelea kuwa watulivu na kuepuka ghasia wakati wa mchakato wa uchaguzi.

    Bw Ruto alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi akiwa na 50.49% ya kura- akimshinda mpinzani wake, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

    Mawakala wa uchaguzi wa Bw Odinga hatahivyo walisema hawakuweza kuhakiki matokeo na baadhi ya makamishha wa Tume ya uchaguzi walitangaza kwamba hawakuweza "kuchukua udhibiti wa matokeo".

    Bw Ruto aliahidi kufanya kazi kwa ajili ya Wakenya wote, akisema kuwa mchakato wa matokeo ulikuwa "wa uwazi zaidi kuwahi kushuhudiwa " nchini Kenya.

    Sherehe, vifijo, shangwe na nderemo viliibuka katika ngome ya Bw Ruto huku maandamano ya kupinga yakiripotiwa katika ngome kuu za Bw Odinga.

    Soma zaidi:

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • Shangwe tele baada ya ushindi wa William Ruto
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • William Ruto: Muuza kuku aliyepanda ngazi hadi kushinda urais Kenya
  16. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Salamu za pongezi kwa rais mteule wa Kenya William Ruto zaendelea kumiminika

    Viongozi mbali mbali wa kimataifa wameendelea kutuma salamu za pongezi kwa rais mteule wa Kenya William Ruto kufuatia kutangazwa kwake Jumatatu kama mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 9 Agosti.

    Katika ujumbe wake wa Twitter Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema ''ningependa kumpongeza rais mteule wa Kenya William Ruto na watu wa Jamuhuri ya Kenya kwa kuendesha uchaguzi wa huru, haki na wa amani.''

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Naye Rais wa Nigeria Mahammadu Buhari amesema ningependa kuwapongeza watu wa Kenya kwa uchaguzi wa amani, na matokeo yenye uwazi, ambayo kwa mara nyingine tena yanaonyesha kuwa mchakato wa demokrasia ,maadili na kanuni vinasalia kuwa njia bora kwa watu kwa kuwachagua viongozi wao na kuwawajibisha

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Naye Rais wa Tanzania Samia Suluhu kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema:’’ Ninawapongezaa Wakenya kwa uchaguzi wao mkuu wa amani na kutangazwa kwa Dr William Ruto kama Rais mteule. Tunatazamia kuendelea kufanya kazi na makaka na madada zetu nchini Kenya kuimarisha uhusiano wetu wa karibu. Tuko pamoja’’:

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

    Hali kadhalika Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahamud amendika kwenye ukurasa wa Twitter akimpongeza Bw William Ruto kwa kuwa rais wa tanowa Kenya:

    Ruka X ujumbe, 4
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 4

    Soma zaidi:

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • Shangwe tele baada ya ushindi wa William Ruto
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • William Ruto: Muuza kuku aliyepanda ngazi hadi kushinda urais Kenya
  17. Raia wa maeneo mbalimbali waendelea kusheherekea Kenya

    Nchini Kenya raia kutoka maeneo tofauti tofauti waendelea kusherehekea.

    Hili linawadia baada ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya Wafula Chebukati kumtangaza William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu.

    William Ruto ametangazwa kuwa Rais mteule wa Kenya, na kupata asilimia 50.49 ya kura.

    Mshindani wake wa karibu alikuwa Raila Odinga, ambaye tume ya uchaguzi inasema amepata 48.85%

    Waliofuatia kwa mbali walikuwa ni George Wajackoyah na David Mwaure ambao kwa pamoja wamepata chini ya 1% .

    Maelezo ya video, Raia wa maeneo mbalimbali waendelea kusherehekea Kenya
  18. Mgombea mwenza Martha Karua asema 'haijaisha'

    Hadi muda mfupi uliopita, hatukusikia lolote kutoka kwa kambi ya Raila Odinga.

    Lakini mgombea mwenza , Martha Karua, kwa sasa amevunja ukimya kwa kutuma ujumbe wa Twitter akisema "Haijaisha hadi iishe."

    Hatuwezi kusema kwa uhakika maana ya tweet hiyo yenye utata kidogo, lakini watu wengi wanashuku kwamba muungano wa Bw Odinga wa Azimio utapinga matokeo ya uchaguzi wa mahakamani.

    Chini ya sheria za Kenya, wagombea urais wana siku saba za kukata rufaa.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  19. Nini maana ya tume ya uchaguzi kugawanyika?

    Ukumbu wa Bomas
    Maelezo ya picha, Ukumbu wa Bomas

    Wakenya sasa wameambiwa kwamba walimchagua William Ruto kama rais wao ajaye, dakika chache kabla ya tangazo hilo makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Juliana Cherera, alisema yeye na makamishna wengine watatu wa uchaguzi hawakuweza kuwa na kauli juu ya matokeo.

    Kuna makamishna saba tu.

    Tangazo la kundi hilo lililojitenga limeongeza wasiwasi nchini humo.

    Sheria ya uchaguzi hata hivyo inampa mwenyekiti jukumu la kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais.

    Wafula Chebukati alifanya hivyo na sasa Bw Ruto ametangazwa kuwa rais ajaye.

    Timu ya Raila Odinga inaweza kupinga matokeo hayo mahakamani na ina siku saba kuwasilisha kesi.

    Kumbuka kwamba mwaka 2017 alifanya hivyo na hatimaye mahakama ya juu iliamua kwamba uchaguzi wa urais ulipaswa kurudiwa.

    Soma zaidi:

    • Shangwe tele baada ya ushindi wa William Ruto
    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto ndiye rais mteule Kenya
    • William Ruto: Muuza kuku aliyepanda ngazi hadi kushinda urais Kenya
  20. Wafuasi wa Raila Odinga waweka vizuizi barabarani

      • Author, Roncliffe Odit
      • Nafasi, BBC KISUMU
    Wafuasi wa Raila Odinga wakiwa wameweka vizuizi barabarani

    Chanzo cha picha, Supplied

    Kuna masikitiko makubwa na uchungu kwa wafuasi wa Raila Odinga kutokana na kupoteza nafasi ya kushinda nafasi ya urais.

    Mamia ya watu wamekuwa wakikusanyika katika mitaa ya Kisumu - ngome ya wafuasi wake - ambapo hali imebadilika kutoka kwa msisimko hadi kuwa hasira.

    Baadhi ya watu wameweka vizuizi vya barabarani na moto. Polisi wa kupambana na fujo walitumwa sehemu za jiji mapema.