Israel na Iran wafunga anga zao kwa safari za ndege za raia
Israel imefunga anga yake kwa safari za ndege za kiraia kufuatia shambulio dhidi ya Iran Jumamosi asubuhi, kulingana na ripoti katika vyombo vya habari vya Israeli.
Shirika la Habari la Tasnim, ambalo lina uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, linaripoti anga ya Iran pia imefungwa.
Majid Akhavan, msemaji wa Shirika la Usafiri wa Anga nchini Iran, alitangaza: "Kulingana na NOTAM iliyotolewa, anga ya nchi nzima imefungwa hadi ilani nyingine."
Wakati huo huo, Wizara ya Afya ya Iran imetangaza kuwa hospitali ziko katika hali ya kusubiri na kwamba idadi ya waliojeruhiwa itatangazwa baada ya uthibitisho wa mwisho.
Soma pia: