Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: Daraja linalounganisha Urusi na eneo la Crimea lililonyakuliwa na Urusi 2014 lachomeka moto
Moto mkubwa kwenye kivuko pekee kati ya rasi ya Crimea na Urusi ulisababishwa na mlipuko wa lori, maafisa wa Urusi wanasema.
Mlipuko kwenye sehemu ya barabara ulisababisha maloro ya mafuta kwenye sehemu ya reli kuwaka moto, kabla ya barabara hiyo kuporomoka.
Crimea ilitwaliwa mwaka 2014 na Urusi, ambayo sasa inatumia daraja la Krymskiy kuhamisha vifaa vya kijeshi nchini Ukraine.
Akaunti rasmi ya Twitter ya serikali ya Ukraine ilijibu moto huo kwa kutuma ujumbe kwenye Twitter: "Sickburn."
Mshauri wa Rais wa Ukraine Zelensky, Mykhailo Podolyak, aliutaja uharibifu huo "mwanzo" - lakini hakudai moja kwa moja kuhusika kwa Ukraine.
"Kila kitu haramu lazima kiharibiwe, kila kilichoibiwa lazima kirudishwe Ukraine, kila kitu kinachokaliwa na Urusi lazima kichukuliwe,"