Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Dirisha la uhamisho wa Ligi Kuu ya Uingereza linafunguliwa - Wafahamu Wachezaji wanaohama
Dirisha la usajili la Ligi Kuu ya Uingereza lilifunguliwa siku ya Ijumaa, huku vilabu vikiwa na uwezo wa kusajili wachezaji rasmi msimu huu.
Timu kadhaa za madaraja ya juu tayari zimetangaza watakaojiunga nao msimu utakaokamilika sasa au tarehe 1 Julai, wakati mikataba ya wachezaji wengi kwenye vilabu vyao vya zamani itakapomalizika.
Dirisha la uhamisho litafungwa saa 23:00 BST siku ya Alhamisi, 1 Septemba.
Dirisha la uhamisho la Scotland, kama lile la Premier League, lilifunguliwa Ijumaa.
Vilabu vya Ligi ya Soka ya Uingereza vimeruhusiwa kusajili wachezaji tangu mchezo wao wa mwisho wa msimu huu.
Nini kimetokea tayari?
Ni nini kinaweza kutokea msimu huu?
Moja ya matukio makubwa ya uhamisho wa msimu huu huenda zikamhusisha mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane.
Nyota huyo wa Senegal anahusishwa sana na kuhamia Bayern Munich.
Bayern wanaweza kuhitaji mshambuliaji mpya kwa sababu nyota wao Robert Lewandowski ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kuondoka, huku Barcelona wakimtaka.
Paul Pogba na Jesse Lingard pia watakuwa kwenye uhamisho baada ya kuondoka Manchester United wakiwa wachezaji huru.
Mshambulizi wa zamani wa Real Madrid Gareth Bale anapatikana pia.
Winga wa Barcelona Ousmane Dembele atakuwa kwenye uhamisho pindi mkataba wake utakapomalizika.
Manchester United, Liverpool, Arsenal na Newcastle United zote zimehusishwa na mshambuliaji wa Benfica Darwin Nunez.
Mshambulizi wa RB Leipzig Christopher Nkunku anavutia timu nyingi za juu za Uropa pia.
Magpies wa Eddie Howe wanaweza kuwa wachezaji wakubwa sokoni msimu huu na utajiri wao mpya, baada ya kukwepa kushushwa daraja.
Wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Stade de Reims, Hugo Ekitike.
Beki wa Burnley James Tarkowski yuko kwenye mazungumzo na Everton.
Meneja wa Manchester United Erik ten Hag huenda akataka kuunda upya timu yake pia.