Tetesi za soka Ulaya Alhamisi tarehe 09.06.2022: Origi, Lukaku, Nunez, Fofana, Lingard, Bale, Jesus

Iliyochapishwa

Divock Origi ni miongoni mwa wachezaji saba ambao wataondoka Liverpool wakati kandarasi zao zitakapokamilika mwishoni mwa Juni, Reds wamethibitisha.

Kipa Loris Karius, winga Sheyi Ojo na kiungo Ben Woodburn pia wataondoka Anfield, pamoja na wachezaji watatu wa akademi.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alikuwa tayari amesema mshambuliaji wa Ubelgiji Origi ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea imemwambia mshambuliaji wao Mbelgiji Romelu Lukaku, 29, anaweza kujiunga tena na Inter Milan kwa mkataba wa mkopo iwapo malipo ni sahihi katika kwa klabu hiyo ya Ligi ya Primia . (Guardian)

Mshambuliaji wa Benfica Muruguay Darwin Nunez, 22, anasitasita kujiunga na Manchester United kwasababu hawakufuzu kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Mirror)

Liverpool wamejiondoa kabla ya Mashetani wekundi (Red Devils) katika mbio za kumsaka Nunez. (Star)

Manchester United na Chelsea wanamtaka mlinzi wa Leicester mwenye umri wa miaka 21 Mfaransa Wesley Fofana. (RMC Sport - in French)

Juventus wametuliza nia yao katika mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Jesse Lingard baada ya awali kutangaza njia ya kusaini mkataba na mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 29 kwa uhamisho wa mkopo. (Goal)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 32, anaweza kusaini mktataba na klabu ya Getafe yenye makao yake Madrid kwasababu ya hamu yake ya kutoiondoa familia yake kufuatia kuondoka kwake katika Real Madrid. (Mail)

Wakala wa Bale Joshua Barnett ametupilia mbali kuwepo kwa uhusiano wowote baina ya mteja wake na klabu ya La Liga club. (Fabrizio Romano)

Meneja wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal amemuonya mlinzi wa Ajax na Uholanzi Jurrien Timber, 20, dhidi ya kuhamia Old Trafford msimu huu . (TalkSPORT)

Mshambuliaji wa Manchester City Mbrazil Gabriel Jesus amepewa ofa ya kuhamia Tottenham likiwa ni pigo kwa mahasimu wao wa kaskazini mwa London Arsenal, ambao wamekuwa wakigusishwa na kijana huyo mwneye umri wa miaka 25 . (Times - subscription required)

Inter Milan wataendelea kumshikilia mlinzi Muitalia Alessandro Bastoni, 23, likiwa ni pigo kwa Manchester United na Tottenham zilizotaka kumchukua. (Mirror)

Kiungo wa kati wa PSV Eindhoven Ibrahim Sangare amejipanga kuhamia katika Primia Ligi , huku Liverpool, Chelsea, Manchester United na Newcastle zikimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa kikataifa wa Ivory Coast mweye umri wa miaka 24. (Sky Sports)

Southampton wamechukua hatua ya kudsaini mkataba na mlindalango wa Jamuhuri ya Ireland Gavin Bazunu, 20, kutoka Manchester City. (Mail)

Arsenal wamepewa ofa ya fursa ya kusaini mkataba na mlinzi wa Uswidi mwenye umri wa miaka 26 Manuel Akanji kutoka klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund. (Sun)