Mzozo wa Ukraine: Fahamu mali ya Ukraine inayodaiwa kuporwa na wanajeshi wa Urusi

Chanzo cha picha, Reuters
Wiki iliopita chombo huru cha habari nchini Urusi Mediazone kilichapisha ripoti iliodai kwamba vikosi vya Urusi vilisafirisha takriban tani 58 za nafaka ilioibwa kutoka maeneo yaliopo karibu na mpaka wa Ukraine na Urusi pamoja na Belarus tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine uanze.
Bidhaa hizo zinadaiwa kushirikisha vitu kama viatu, vyakula vilivyowekwa mkebeni, runinga, matairi ya gari na mahema
Urusi haijajibu madai hayo ya wizi lakini maafisa wameshtumu Ukraine kwa utengeneza video bandia za kuishutumu Urusi kwa kutekeleza wizi.
Hatua hiyo inajiri baada ya mkimbizi wa Ukraine nchini Uingereza kusema kwamba alitambua vitu vyake vya nyumbani vilivyoibwa nyumbani kwake baada ya kuviona vimewekwa juu ya kifaru cha wanajeshi wa Urusi katika picha iliochukuliwa hivi karibuni.
Alina Koreniuk anasema kwamba boksi lililo na boiler yake alilotaka kuweka nyumbani kwake kabla ya vita kuzuka lilikuwa juu ya kifaru hicho.
Yeye na watoto wake aliondoka Ukraine tarehe nane April na sasa wanaishi na wanandoa wa Uingereza katika mji wa Nottinghamshire.
Picha hiyo iliochukuliwa mnamo mwezi Mei , inaonesha kifaru hicho kikipita mbele ya makaazi yalioharibiwa kwa mashambulizi ya mabomu katika mji wa Popasna.
Vikosi vya Urusi vimekuwa vikidhibiti mji huo , katika jimbo la Luhansk tangu Mei 8. Bi Koreniuk anasema kwamba picha hiyo ilichukuliwa katika barabara dakika tano mbali na nyumba yake. Ilitambuliwa na mumwe wake.
Alisema kwamba: Je umegundua kitu chochote kisicho cha kawaida kuhusu picha hii na akiniuliza iwapo niliona alichokiona, aliambia BBC.
Mbali na boiler hiyo , vitu vingine vilivyokuwa juu ya kifaru hicho ni pamoja na kitambaa cha mezani, shiti za kulała za watoto na blanketi nyekundu, anaongezea.
Wizi wa nafaka

Chanzo cha picha, NADIYA STETSIUK
Katika tukio jingine, Ukraine imeishutumu Urusi kwa wizi wa nafaka katika baadhi ya maeneo inayokalia , kitendo ambacho imesema kimeongezea tishio la usalama wa chakula duniani kwa kuathiri msimu wa upanzi mbali na uzuiaji wa bandari ya Ukraine wakati wa vita.
Ilipoulizwa kuhusu madai hayo , Kremlin ilisema haikuwa na habari zozote kuhusu madai hayo.
Wizara ya masuala ya kigeni ya Ukraine ilisema katika taarifa ilioandikwa kwamba inashtumu vikali vitendo vya kihalifu vya Urusi katika wizi wa mimea kutoka kwa wakulima waliopo katika eneo la Kherson, kusini mwa Ukraine.
Hatahivyo haikutoa habari zaidi za madai hayo ya wizi wa nafaka , katika mji huo ambao umetekwa na vikosi vya Urusi tangu Urusi ivamie taifa hilo mnamo tarehe 24 mwezi Februari.
Wizi wa nafaka kutoka jimbo la Kherson pamoja na uzuwiaji wa meli katika bandari za Ukraine unatishia usalama wa chakula kote duniani , ilisema.
''Tunataka Urusi kusitisha wizi wa nafaka , kufungua bandari za Ukraine , kuwacha meli ziingie na kutoka''.
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine ilisema katika taarifa tofauti kwamba ilifungua kesi ya jinai kwa madai kwamba wanajeshi wa Urusi, wakitishia vurugu, mnamo Aprili 26 waliiba tani 61 za ngano kutoka kwa biashara ya kilimo katika mkoa wa Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine.
Wizi wa chuma huko Mariupol

Chanzo cha picha, MAX DELANY/AFP
Kutoka bandari ya Mariupol inayodhibitiwa na jeshi la Urusi kuelekea Rostov-on-Don, meli iliyobeba bidhaa za chuma zilizovingirishwa, meli ya mizigo ya Astrakhan kavu, iliondoka. Kyiv ilikiita kitendo hicho kama cha uporaji na wizi.
Kwa mujibu wa shirika la serikali la Urusi RIA Novosti, meli hiyo ilikuwa ikipakiwa kwa siku mbili, upakiaji ulifanywa na kreni inayoelea. "kreni za bandari bado hazina nguvu kutokana na kukatika kwa usambazaji wa umeme wa bandari wakati wa mapigano," mwandishi wa shirika hilo anabainisha.
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Kama alivyoandika Denis Pushilin, kiongozi wa kundi la DPR , aliandika katika mtandao wa telegram, kwamba tani 2500 za vyuma ziliibwa kutoka katika bandari ya Mariupol .
Ukraine iliitaja hatua ya Urusi kuiba vyuma vyenye thamani ya mamia ya madola kutoka Mariupol kama kitendo cha wizi wa mabavu .
Kulingana na Lyudmika Denisova, kamishna wa haki za kibinadamu katika eneo la Verkhova Rada Ukraine, kabla ya kuuteka mji huo, kulikuwa na tani 200,000 za vyuma zenye thamani ya $170m katika bandari ya Mariupol.












