Moja kwa moja, Bunge la Marekani laidhinisha mpango wa kusitisha vita na Iran

Azimio hilo kwa kiasi kikubwa ni la kiishara, lakini linaongeza shinikizo kwa Ikulu ya White House kumaliza mzozo huo mara moja.

Skip Video and continue reading
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • xx
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

NaAmbia Hirsi

  1. Trump alisuta bunge la Marekani kwa kusitisha hatua za kijeshi dhidi ya Iran: Hii ilikuwa ni kumsaidia adui

    Rasi wa Marekani Donald Trump ameandika ujumbe mtandaoni kukosoa hatua ya bunge la seneti la nchi hiyo kuidhinisha mswada wa kudhibiti mamlaka yake ya vita. Trump alisema:

    ''Nilikuwa nimeiweka Iran chini ya shinikizo kali, walikuwa tayari kurudi nyuma, na walikuwa karibu kutupatia chochote. Kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa, Iran iliiheshimu sana Marekani na rais wake, (mimi). Lakini Seneti ya Marekani iliamua wakati mbaya zaidi, kupiga kura isiyo na maana ya Sheria ya Nguvu za Kivita, kutuma ujumbe kwa taifa linalofadhili ugaidi kwamba Marekani haijafurahishwa na hatua ninazochukua dhidi yao na kwamba lazima niache. Wamempa msaada adui. Warepublican wanne walipiga kura na Democrats, na sasa Iran inawauliza wawakilishi wangu, 'Kura hii inamaanisha nini?' Maseneta hawa wamefanya kazi yangu kuwa ngumu zaidi, lakini sitarudi nyuma, hata iweje, kwa sababu hivyo ndivyo ninavyofanya kazi kila wakati!"

  2. Oman yatangaza kuunda njia ya muda ya baharini kuwezesha meli kupita Hormuz

    ,

    Chanzo cha picha, Reuters

    Oman imetangaza kuanzisha njia ya muda ya baharini kwa ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) ili kurahisisha usafiri wa meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz.

    Shirika la habari la serikali ya Oman liliripoti kwamba meli zinazonuia kuvuka Mlango-Bahari wa Hormuz lazima zifanye mipango inayohitajika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini na mamlaka ya Oman.

    Taarifa hizi zinakuja saa chache baada ya Mohammad Baqer Qalibaf, mkuu wa ujumbe wa wanadiplomasia wa Iran, kuzuru nchi hiyo.

    Ilikuja baada ya Iran na Oman kutangaza katika taarifa ya pamoja siku ya Jumanne kwamba zimejitolea kudumisha Mlango-Bahari wa Hormuz kama njia ya maji salama na iliyo wazi kwa meli za kimataifa, wakati huo huo zikitilia mkazo uhuru wao na haki zao za kujitawala juu ya eneo la bahari la Hormuz.

    Pia wametangaza kwamba watachunguza usimamizi wa siku zijazo wa Mlango-Bahari wa Hormuz na gharama ya huduma zinazotolewa katika njia hii ya maji kwa kuunda kamati ya pamoja.

    Kauli hiyo imetolewa baada ya mkutano kati ya maafisa wakuu kutoka nchi hizo mbili mjini Muscat.

    Baada ya kuondoka Uswizi, Mohammad Baqer Qalibaf, mkuu wa timu ya mazungumzo ya Iran na Abbas Araqchi,

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran walikwenda Oman na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje Badr Busaidi na Sultan Haitham bin Tariq, Mfalme wa Oman.

    Siku ya Jumanne, Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini, ambalo ni mshirika wa Umoja wa Mataifa,

    lilitangaza kuanza kwa mchakato wa kuwarejesha nyumbani wanamaji zaidi ya 11,000 waliokuwa wamenasa kwenye Mlango Bahari wa Hormuz; mabaharia ambao wamekwama katika eneo hilo tangu vita vya Marekani na Israel na Iran na kuzuiliwa kwa trafiki katika Mlango wa bahari wa Hormuz.

    Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini limesema kuwa operesheni ya kuwahamisha mabaharia hao itafanywa kwa ushirikiano wa karibu na nchi zote za eneo hilo na Marekani.

  3. Kombe la Dunia: DRC yalazwa na Colombia

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Katika mechi ya mwisho siku ya Jumanne, timu ya soka ya Colombia ilifanikiwa kuishinda DRC Congo kwa bao moja na kujihakikishia kusonga mbele kwa pointi 6.

    Colombia walianza mchezo kwa kasi kuanzia dakika za kwanza kabisa, na mshambuliaji wa timu hiyo Luis Diaz, alifunga dakika ya 10, lakini mwamuzi akatangaza kuwa ameotea.

    Diaz pia alifunga bao zuri mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya kuwapiga chenga walinzi kadhaa wa Congo, lakini mwamuzi akakataa tena kuwa ameotea mara tu alipopata pasi.

    Mchezaji wa Colombia Mones, hatahivyo aliifungia Colombia bao la pekee katika dakika ya 76.

    Hivyo, Colombia, ambayo ilikuwa imeishinda Uzbekistan katika mechi ya kwanza, ilipata pointi 6 kupitia ushindi huo na kuwaweka kileleni mwa jedwali juu ya Ureno na kusonga mbele.

    Soma:

  4. 'Nimerudi' - Ronaldo awajibu wakosoaji baada ya kuvunja rekodi

    Ronaldo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    "Nimerudi! Nimerudi!" alisema Baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-0 wa timu yake dhidi ya Uzbekistan, Cristiano Ronaldo alikodolea macho kamera ya televisheni na kuwakejeli kwa wale waliodai kuwa yeye ndiye tatizo la Ureno kwenye Kombe la Dunia la 2026.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 hakuweza kuficha hisia zake, wala kuzuia furaha yake alipokuwa akisherehekea mafanikio ya kihistoria ya kuwa mchezaji wa kwanza kuzifumania nyavu katika matoleo sita ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya kandanda. Ilikuwa pia jibu kamili kwa wakosoaji ambao walikuwa wamempuuza.

    Ronaldo alikosolewa vikali baada ya Ureno kutoka sare ya 1-1 na DR Congo katika mechi yao ya kwanza ya Kundi K, huku nyota wengine wa kimataifa wakiwemo Lionel Messi wa Argentina, mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, Erling Haaland, wa Norway, Vinicius Jr wa Brazil na nahodha wa Uingereza Harry Kane wote wakionyesha umahiri wao katika wiki mbili za kwanza za michuano ya Kombe la Dunia 2026.

    Ronaldo alihitaji dakika sita pekee kufunga bao lake la kuvunja rekodi, akitumia vyema krosi ya Joao Cancelo, na kisha akafunga bao lengine kabla ya kipindi cha mapumziko kwa ushirikiano na Bruno Fernandes.

    Licha ya juhudi za wachezaji wenzake kipindi cha pili, nahodha huyo wa timuya taifa ya Ureno hakufanikiwa kupata hat-trick aliyotamani.

    Maelezo zaidi:

  5. Umoja wa Mataifa kuwaondoa mabaharia waliokwama katika Mlango-Bahari wa Hormuz

    Rubio

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya baharini (IMO) linajianda kuwahamisha zaidi ya mabahari 11,000 ambao wamekwama katika eneo la Ghuba kutokana na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

    Katibu mkuu wa IMO Arsenio Dominguez amesema "operesheni hiyo kubwa" itafanywa kwa ushirikiano na Iran, Oman, Marekani, mataifa mengine ya pwani katika eneo hilo.

    "Tumehakikishiwa usalama wetu na tumethibitisha kwa kina masharti ya urambazaji salama ili kusaidia shughuli hizi," aliongeza.

    Makubaliano ya muda yalitiwa saini wiki iliyopita ili kumaliza mzozo huo, lakini Marekani na Iran zinaendelea kuzozana kuhusu maelezo ya Mkataba wa Maelewano (MoU).

    Marekani imesema Makubaliano hayo yanajumuisha hakikisho la mpango wa silaha za nyuklia wa Iran kufanyiwa ukaguzi na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA).

    Rais wa Marekani Donald Trump alichapisha ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii Jumanne kusema kuwa: "Iran imekubali kufanywa jwa ukaguzi wa Nyuklia wa kiwango cha juu zaidi hadi siku zijazo (usio na kikomo!!!). Hii itahakikisha 'Usalama wa Nyuklia.'

    Muda mfupi kabla ya ujumbe huo wa Trump, Iran ilisema shirika hilo la Umoja wa Mataifa halitaweza kukagua maeneo ya nyuklia yaliyolipuliwa na Marekani na Israel mwaka jana.

    Soma zaidi:

  6. Bunge la Marekani laidhinisha mpango wa kusitisha vita na Iran

    Donald Trump

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Donald Trump

    Bunge la Seneti la Marekani linalodhibitiwa na chama cha Republican limeidhinisha mswada ambao utamlazimu Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha vita na Iran au kutafuta kibali cha bunge kabla ya kuendelea na hatua za kijeshi.

    Katika kura iliyopigwa Jumanne jioni, maseneta kadhaa wa chama cha Republican walijiunga na wenzao wa Democratic kupitisha mswada huo kwa kura 50 dhidi ya 48, hatua inayoonyesha upinzani wa pande mbili dhidi ya kuendeleza vita.

    Mswada huo pia ulipitishwa katika Bunge la Wawakilishi la Marekani mwezi Juni, ambapo wabunge wanne wa Republican walipiga kura ya ndio pamoja na wabunge wate wa Dempcratic wote, na matokeo yakiwa 215 kwa 208.

    Hii ni mara ya kwanza tangu kupitishwa kwa Sheria ya Nguvu za Kivita mwaka 1973 ambapo mabunge yote mawili ya Marekani yamepitisha azimio la pamoja la kusitisha hatua ya kijeshi ya rais.

    Hata hivyo, azimio hilo kwa kiasi kikubwa ni la kiishara, kwani licha ya kuidhinishwa na mabunge yote mawili, halitatumwa kwa rais kutiwa saini na halilazimishi kisheria.

    Umuhimu wa kura hii ni kwamba inaongeza shinikizo kwa Ikulu ya White House kumaliza vita na Iran, haswa wakati huu ambapo bei ya mafuta imepanda na upinzani wa umma dhidi ya vita hivyo umeongezeka.

    Hata hivyo, afisa wa Ikulu ya White House aliambia BBC kwamba tangu makubaliano ya kusitisha mapigano yalikubaliwa Aprili 7, kwa sasa hakuna mzozo wowote ambao utahitaji kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani.

    Soma Zaidi:

  7. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.