Visa vya Monkeypox kuchunguzwa Ulaya, Marekani, Canada na Australia

Chanzo cha picha, Getty Images
Kesi za ugonjwa wa Monkeypox zinachunguzwa katika nchi kadhaa za Ulaya na vile vile Marekani, Canada na Australia, hii ni kwa mujibu wa mamlaka ya afya na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.
Kesi mpya zimeripotiwa Ubelgiji, Ufaransa, Australia na Ujerumani.
Hii inafuatia maambukizi yaliyothibitishwa nchini Italia, Uswidi, Uhispania, Ureno, Marekani, Canada na Uingereza ambapo kesi ya kwanza Ulaya iliripotiwa.
Monkeypox ni ugonjwa uliopo katika sehemu za ndani ndani katika Afrika ya Kati na Magharibi.
Matukio ya ugonjwa nje ya ukanda huo mara nyingi huhusishwa na kusafiri hadi katika eneo hilo.
Monkeypox ni ugonjwa nadra wa virusi ambao kwa kawaida sio mkali na ambao watu wengi hupona baada ya wiki chache, kwa mujibu wa watoa Huduma ya Kitaifa ya Afya Uingereza.
Virusi hivyo havisambai kwa urahisi miongoni mwa watu na hatari kwa umma inasemekana kuwa ndogo sana.
Kesi ya kwanza ya ugonjwa huo nchini Uingereza iliripotiwa Mei 7. Mgonjwa huyo alikuwa amesafiri hivi karibuni hadi Nigeria, ambako wanaaminika kuambukizwa virusi hivyo, kabla ya kusafiri kwenda Uingereza, Shirika la Usalama la Afya la Uingereza lilisema.

Chanzo cha picha, Science Photo Library
Sasa kuna kesi 20 zilizothibitishwa nchini Uingereza, Katibu wa Afya Sajid Javid alisema Ijumaa.
Hakuna chanjo mahususi ya monkeypox, lakini chanjo ya ndui hutoa kinga ya 85% kwa kuwa virusi hivi viwili vinafanana kabisa.
Mamlaka nchini Uingereza walisema walikuwa wamenunua hifadhi za chanjo hiyo na kuanza kuitoa kwa wale walio na "viwango vya juu vya kuambukizwa" monkeypox
Mamlaka za afya za Uhispania pia zimeripotiwa kununua maelfu ya chanjo za ndui ili kukabiliana na mlipuko huo, kulingana na gazeti la Uhispania El País.
Kisa cha kwanza cha Australia kiligunduliwa kwa mtu ambaye aliugua baada ya kusafiri kwenda Uingereza, Idara ya Afya ya Victoria ilisema.
Huko Amerika Kaskazini, maafisa wa afya katika jimbo la Massachusetts la Marekani walithibitisha kwamba mtu aliambukizwa baada ya kusafiri kwenda Canada hivi karibuni.
Alikuwa katika "hali nzuri" na "haitoi hatari kwa umma," maafisa walisema.
Huko Amerika Kaskazini, maafisa wa afya katika jimbo la Massachusetts Marekani walithibitisha kwamba mtu ameambukizwa baada ya kusafiri kwenda Canada hivi karibuni. Alikuwa katika "hali nzuri" na "haileti hatari kwa umma," maafisa walisema.














