Mzozo wa Ukraine: Je, Urusi inafanya biashara kiasi gani na China?

Iliyochapishwa

Australia imetoa wito kwa China kuongeza juhudi za kuitenga Urusi baadi ya uvamizi wake dhidi ya Ukraine, na kutekeleza vikwazo sawa na vile vya Marekani, Muungano wa Ulaya na Uingereza.

Waziri Mkuu Scott Morrison alikosoa makubaliano ya hivi majuzi ambayo China ilifanya kununua ngano zaidi kutoka Urusi, ikisema kuwa inaiweka nchi hiyo "njia ya kiuchumi".

Lakini je, China inaweza kusaikwamua Urusi kiuchumi?

Je, vikwazo dhidi ya Urusi vitaathiri biashara?

China inasema "itaendelea kama kawaida na ushirikiano wake wa kibiashara"na Urusi.

Lakini baadhi ya benki za Urusi sasa zimepigwa marufuku katika mfumo wa kimataifa wa malipo wa Swift. Hii inatumika kote duniani kwa miamala ya kifedha, na kuna uwezekano wa kufanya kulipa kwa mauzo yake ya nje kuwa ngumu zaidi.

Kwa sababu hiyo, China hivi majuzi ililazimika kupunguza baadhi ya ununuzi wake kutoka Urusi kwa sababu wafanyabiashara wametatizika kupanga ufadhili.

Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimekuwa zikifanya juhudi za kuunda mifumo yao mbadala ya malipo ili kupunguza utegemezi wao kwenye mifumo inayotumia dola kama Swift.

Urusi ina Mfumo wake wa Kupokezana Ujumbe wa Kifedha (STFM) huku Uchina ikiwa na Mfumo wa Malipo wa Benki baina ya Mipaka (CIPS), na hizi zinafanya kazi katika sarafu zao.

Utafiti uliochapishwa na kituo cha Carnegie Moscow unahoji kuwa mifumo hiyo ya malipo ya ndani "sio mbadala wa Swift".

Kufikia 2021, ni benki moja tu ya China ilikuwa imejiunga na STFM, ingawa benki nyingi zaidi za Urusi na taasisi za fedha za kimataifa zimeunganishwa na mfumo wa malipo wa Kichina.

Kwa sasa ni 17% tu ya biashara kati ya Urusi na China inayotumia Yuan ya China (kutoka 3.1% mnamo 2014), kulingana na ripoti za vyombo vya habari zinazoashiria takwimu rasmi za Urusi.

Na biashara yao ya nishati bado inafanywa kwa dola za Kimarekani,ingawa wanazidi kutumia Yuan.

Je, Urusi inafanya biashara kiasi gani na China?

Biashara kati ya hizo mbili imekuwa ikikua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.

Ilifikia kiwango cha juu zaidi cha karibu $147bn (£110bn) mwaka jana - ikiwa ni karibu asilimia 36 kutoka mwaka uliopita - na ilichangia takriban 18% ya biashara ya jumla ya Urusi mwaka wa 2021.

Wakati wa ziara ya Rais Putin mjini Beijing mwezi uliopita, nchi hizo mbili zilisema zitaongeza biashara yao hadi $250bn ifikapo 2024.

Mamlaka ya forodha ya China ilitangaza kuondolewa kwa vikwazo vyote vya uagizaji wa ngano na shayiri kutoka Urusi siku ambayo shambulio dhidi ya Ukraine lilipoanza.

Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi

Hapo awali ilitumika kuzuia uagizaji wa ngano kutoka maeneo fulani ya Urusi kwa sababu ya magonjwa.

Mwaka jana, China ilikuwa nchi ya nne duniani kwa mnunuzi mkubwa wa ngano na mnunuzi mkubwa zaidi wa shayiri, na Urusi ndiyo nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa nafaka zote mbili.

Mbali na bidhaa za kilimo, China pia kwa sasa ni soko moja kubwa la mauzo ya nishati ya Urusi kama vile mafuta, gesi na makaa ya mawe.

Ni mnunuzi mkubwa zaidi wa makaa ya mawe nchini Urusi, na nchi hizo mbili zilikubaliana juu ya mkataba mpya wenye thamani ya zaidi ya $20bn - wiki moja tu kabla ya uvamizi wa Ukraine.

Hata hivyo, EU ndiyo mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara na Urusi. Mnamo 2021, jumla ya biashara kati ya hizo mbili ilikuwa na thamani ya karibu mara mbili ya biashara ya China na Urusi.

Hiyo sasa inaanza kubadilika, kulingana na mchambuzi wa masuala ya uchumi Dr Rebecca Harding.

"Ni jambo lisiloepukika kwamba biashara ya EU-rusi inapungua kwa kuzingatia vikwazo. Mgogoro uliopo sasa hivi umeongeza mwelekeo ndani ya EU juu ya hitaji la kubadilisha usambazaji," alisema.

Biashara kati ya Urusi na Marekani ni ndogo zaidi.

Je, China inaweza kununua nishati zaidi ya Kirusi?

Uchumi wa Urusi unategemea sana uuzaji wa mafuta na gesi nje ya nchi, na vikwazo vya hivi karibuni havijalenga sekta hizo.

Mwaka jana, Urusi ilikuwa muuzaji wa pili wa mafuta wa China kwa ukubwa na muuzaji wa tatu wa gesi kwa ukubwa, na mauzo ya nje yalifikia $41.1bn na $ 4.3bn mtawalia, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

Hivi majuzi Bw Putin alizindua mikataba mipya ya Urusi ya mafuta na gesi na China yenye thamani ya takriban $117.5bn.

Hata hivyo, EU inasalia kuwa soko kuu la UrusI, na inauzia kanda hiyo karibu 40% ya gesi na karibu 26% ya mafuta yake.

China ndio mnunuzi mkubwa wa makaa ya mawe nchini Urusi, na nchi hizo mbili zilikubaliana juu ya mkataba mpya wenye thamani ya zaidi ya $20bn - hivi karibuni.