Urusi na Ukraine: Nini kitatokea ikiwa Urusi itadhibiti maeneo yote ya Ukraine?

Iliyochapishwa

Wanajeshi wa Urusi wanajaribu kuchukua miji miwili mikubwa ya Ukraine, Kiev na Kharkiv, lakini wanakabiliwa na upinzani mkali.

Wakati huo huo, takriban wakimbizi nusu milioni tayari wameikimbia Ukraine, na nchini Urusi, vikwazo vikali vimeanza kuathiri wakazi wa eneo hilo.

Wakati mzozo huo ukiendelea, waandishi watatu wa BBC walijibu maswali kutoka kwa hadhira.

Mwandishi wa BBC wa kimataifa, Lyse Doucet, na mwandishi wa BBC wa huduma za Ukraine, George Erman, walijibu maswali kutoka Kiev, mji mkuu wa Ukraine.

Mwandishi wa habari Mark Lowen anaripoti kutoka mpaka wa Poland na Ukraine.

Je, kwa nini Urusi ilichagua kushambulia au kuvamia Ukraine sasa, badala ya mwaka mmoja au miaka miwili iliyopita? Je, kuna kitu "kilichochea" hilo kutokea sasa? - Anna, Hawaii

Majibu ya Lyse Doucet:

Hili ni swali muhimu na hatuna majibu yote kwa sasa.

Vita hivi mara nyingi huitwa vita vya Rais Putin: inaaminika kuwa yeye ndiye mtu anayetoa maelekezo na hakuna mtu anayejua wazi kuhusu vita hii na hakuna anayejua wazi vita hii itaenda mpaka lini na yuko tayarikujaribu kumdhibiti jirani ake (Ukraine), na kwa mujibu wake, hapaswi jirani huyo kuwa kama nchi.

Wengi wanauliza ikiwa aliona udhaifu wa washirika wa muungano wa NATO, hasa Marekani, baada ya hatua kubwa ya kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Afghanistan na Taliban kutwaa madaraka.

Wengi pia wanahoji kuhusu hali ya kiongozi huyo wa Urusi baada ya kutengwa.

Je, jeshi la Urusi liko na nguvu zake kamili au ni matatizo ya vifaa ambayo yanawazuia kushindwa kuidhibiti Ukraine? - John, Marekani

Lyse Doucet anajibu:

Mjini Kiev, wengi walidhani kwamba kuona majeshi ya Urusi katikati ya mji mkuu ilikuwa ni suala la masaa kadhaatu.

Lakini vikosi vya Ukraine vinatoa upinzani mkali, na vikosi vya Urusi vinasemekana kuwa bado viko umbali wa kilomita 30 kutoka katikati ya mji.

Kila siku, vikosi zaidi na silaha nzito zaidi zinaingia kila upande kwenye mipaka ya Ukraine, lakini kwa kasi ya kawaida au kwa namna wengi walivyotarajia.

Ni vigumu kusema kama kila kitu kinakwenda "kulingana na mpango" kwa sababu hakuna anayejua mpango wa Rais Putin ni nini.

Lakini kumekuwa na ripoti za misafara ya Urusi iliyoishiwa mafuta, wanajeshi wa Urusi wakipoteza hamu ya kupigana, huku Ukraine, wanajeshi na raia wake wakiendelea kupambana, wengine wakiwa na silaha wengine kwa nguvu ya uzalendo.

Pia kumekuwa na mapigano makali mitaani katika maeneo ikiwa ni pamoja na mji wa pili kwa ukubwa, Kharkiv.

Wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakisonga mbele na kushambulia, katika mji wa kaskazini mashariki wa Chernigov na mji wa kusini wa Maripul, miongoni mwa miji mengine mingi.

Raia wa Ukraine wanaozungumza Kirusi wanamtazamo gani kuhusu uvamizi wa Urusi kwa Ukraine? -Man Chun Siu, London

Lyse Doucet anajibu:

Tuliona baadhi ya matukio ya sherehe katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine ambayo yamekuwa yakidhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi tangu 2014.

Baadhi ya watu waliokimbia kutoka eneo hili waliwaambia waandishi wa BBC kuwa wanafurahi kwamba Urusi iliitambua Donetsk na Luhansk. Lakini ni vigumu kujua walipokea kwa namna gani.

Maisha yamekuwa magumu zaidi kwa wakazi wa maeneo haya katika miaka minane iliyopita: wametenganishwa na familia zao, hata viinua mgongo vyao vilichukuliwa.

Kuzungumza Kirusi haimaanishi kuwa unaiunga mkono Urusi. Raia wengi wa Ukraine wanazungumza lugha zote mbili, ikiwemo na Rais Zelensky.

Nini maslahi ya NATO katika haya yote? - Adrian Marino

George Erman anajibu:

Kabla ya kuanza kwa vita hivi miaka minane iliyopita, raia wengi wa Ukraine hawakutaka Ukraine kuwa sehemu ya NATO.

Hii ilibadilika katika mwaka wa kwanza wa vita vya 2014, baada ya uvamizi wa Crimea na mwanzo wa mgogoro wa Dombas.

Raia wa Ukraine waliona kwamba Poland, Jamhuri ya Czech na nchi za Baltic zilikuwa zikilindwa na Marekani na nchi nyingine za NATO dhidi ya matukio yote ya vita, kutokuwa na utulivu na shinikizo kutoka nchi nyingine kama vile Urusi, kwa mfano.

Sasa wanaona kuingia NATO ni kama suluhisho kwa usalama wa Ukraine wakati ukiwa na jirani kama Urusi, ambaye ana uwezo mkubwa sana wa kijeshi na jeshi kubwa.

Kwa mujibu wa wataalamu, Putin anataka kuunda upya himaya mpya ya Urusi na hatambui waukraine kama watu tofauti.

Kwa sasa 59% ya waukraine, kwa mujibu wa kura za maoni za Desemba 2021, wanataka kujiunga na NATO na 27% tu wanapinga.

Lakini vita hivi vinaweza kubadili maoni ya watu wengi ambao hapo awali walikuwa na huruma na Urusi.

Nini chanzo cha mgogoro huu?

George Erman anajibu:

Mgogoro huo ulianza mwaka 2014 kwa watu walio nje ya mataifa hayo.

Lakini kwa Ukraine mgogoro huo ulianza mwaka 2013. Urusi ilitaka Ukraine iwe mwanachama wa Shirika la ushirikiano wa kiuchumi na Urusi, lakini Rais (Viktor) Yanukovych awali alitaka Ukraine iwe sehemu ya Umoja wa Ulaya(EU).

Urusi haijafurahishwa na uamuzi huo. Kufuatia mabadiliko ya uamuzi wa Yanukovych, maandamano ya kuunga mkono ushirikiano na EU na dhidi ya rais yalizuka nchini Ukraine.

Kulikuwa na majeruhi wengi katika maandamano na Rais Yanukovych aliikimbia Ukraine.

Kuna mikoa miwili Ukraine ambayo ni tofauti sana na maeneo mingine: Dombas na Crimea.

Crimea ilidhibitiwa haraka sana na jeshi la Urusi. Ni eneo pekee la Ukraine lenye Warusi wengi. Huko Dombas, nusu ni wana asili ya Urusi na nusu nyingine Ukraine. Lakini ni eneo ambalo watu wanazungumza Kirusi.

Hata hivyo, lugha haikuwa kiashiria kikuu cha mgogoro huu. Ilikuwa ni vita ya wasomi wa mkoa wa Donetsk dhidi ya wasomi wengine wa kikanda. Wale wa Donetsk walitaka ushirikiano na Urusi, wengine walitaka ushirikiano na Umoja wa Ulaya.

Je, nchi jirani za Urusi, ambazo ni sehemu ya NATO, zitakuwa salama kwa muda gani? - Cristina Onofras, Romania

Mark Lowen anajibu:

Nchi za mashariki mwa NATO, ambazo zinapakana na Ukraine, zina wasiwasi.

Lithuania ilitangaza hali ya dharura, wakati Sweden na Finland, ambazo sio wanachama wa NATO, zilijiunga na mkutano wa dharura wa umoja huo wiki iliyopita, na Marekani imeongeza idadi ya wanajeshi katika nchi kama Poland.

Baadhi ya raia wa Poland niliyozungumza nao karibu na mpaka wana wasiwasi juu ya usalama wao wenyewe, lakini lengo lao kuu bado ni kuwasaidia marafiki zao wa Ukraine au jamaa kwa upande mwingine au wale ambao wamekimbia.

Ikiwa Urusi itaweza kuichukua Ukraine, ni nini kinachofuata? - Nhlanhla, Afrika Kusini

Lyse Doucet anajibu:

Hilo ni swali kwa Ukraine na ni wakati wa kueleza mustakabali na hatari kwa ulimwengu.

Kwanza, vikosi vya Urusi vitalazimika kukamata sehemu kubwa zaidi za eneo la nchi ya pili kwa ukubwa barani Ulaya, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Kiev, mji wenye watu karibu milioni tatu wanaojulikana kuwa wanaunga mkono Ulaya na NATO.

Historia inatuambia kwamba mapinduzi ya kijeshi na uvamizi yamefanikiwa kuchukua vituo vya televisheni na majumba ya rais. Hii haitoshi.

Mashambulizi yatakuwa makali na uasi wa Kiukreni utaibuka haraka. Msaada utatoka kwa njia nyingi, vyanzo vingi, na kwa njia nyingi. Ni vigumu kufikiria kwamba risasi inaweza kuishi. Itaingia katika historia kama masaa ya kiza zaidi.

Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi