Mzozo wa Ukraine: Siku ya saba ya uvamizi wa Urusi kwenye ramani
Wiki moja baada ya Urusi kuvamia Ukraine, vikosi vyake vimepiga hatua kuingia nchini humo lakini kufikia sasa havijafanikiwa kuuteka mji mkuu Kyiv na miji mingine mikubwa.
Haya ndio matukio ya hivi punde siku hiii ya saba tangu uvamizi huo ulipoanza:
- Wanajeshi wa Urusi wanaotumia parachuti wametua Kharkiv- mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine
- Wizara ya Ulinzi ya Urusi pia imedai kuteka bandari ya kusini ya Kherson.
- Urusi imewaomba wakazi kuondoka Kyiv kabla ya kufanyika kwa shambulio la kupangwa dhidi ya jiji hilo.
- Msafara wa magari ya vita ya umbali wa maili 40 umesalia kaskazini mwa Kyiv.
Urusi ilianzisha mashambulizi yake mapema Alhamisi iliyopita kutoka pande tatu kuu: kaskazini, kusini na mashariki.
Tangu wakati huo, wanajeshi wake wamemiminika nchini Ukraine na maeneo kadhaa yamelipuliwa kwa mizinga kutoka angani.
Kupigania Kyiv
Wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakielekea mjini Kyiv kutoka upande wa kaskazini, ingawa juhudi hizo zimefifia katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Msafara huo wenye urefu wa maili 40 ulionaswa katika picha za satelaiti umetatizwa na magari yaliyoharibika, kulingana na wachambuzi.
Lakini mji mkuu umekubwa na mashambulio kadhaa kutoka angani.
Siku ya Jumanne, wanajeshi wa Urusi walishambulia mnara wa Televisheni mjini Kyiv, kuua watu watano na kukatiza matangazo ya vituo kadhaa ya habari.
Uwanja wa ndege wa Hostomel umeshhudia makabiliano makali na kudhibitiwa na pande tofauti katika siku chache zilizopita, kulingana na Taasisi ya Mafunzo ya Vita (ISW).
Vikosi vya Urusi karibu na Obolon viungani mwa Kyiv siku ya Ijumaa na mkabiliano yaliripotiwa kaskazini -magharibi mwa Kyiv mnamo wikendi.
Lakini kufikia sasa vifar vya Urusi na magari ya silaha hayajaonekana katika mji mkuu.

Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Wanajeshi wa Urusi wanaotumia parachuti waishambulia Kharkiv
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine

Mashambulio kutoka kaskazini
Wanajeshi wa Urusi waliokuwa wakielekea Kyiv walivuka mpaka na kuingia Ukraine kwenye makutano ya njia tatu kati ya Ukraine, Urusi na Belarus, huko Senkivka.
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza (MoD) siku ya Jumanne ilisema kwamba sehemu kubwa ya vikosi vya ardhini vya Urusi bado vimesalia zaidi ya kilomita 30 (maili 19) kutoka Kyiv.

Nguzo za kivita, ikiwa ni pamoja na mizinga na mifumo mingi ya kurusha roketi, zimeelekea Chernihiv, ambako zimekabiliwa na upinzani mkali kutoka Ukraine. Mji huo ulishambuliwa kwa makombora mazito kutoka kwa wanajeshi wa Urusi lakini bado uko mikononi mwa Ukraine.
Hatua ya pili, ya haraka zaidi imefika upande wa magharibi wa mto Dnieper kupitia Chernobyl, ikichukua udhibiti wa eneo kubwa kaskazini na magharibi mwa Kyiv.
Mashambulizi kutoka mashariki
Wanajeshi wa Ukraine wanasema wanajeshi wa Urusi wa kuruka kwa miavuli wametua mjini Kharkiv,kufuatia mashambulizi makali ya angani dhidi ya mji huo katika siku za hivi karibuni.
Siku ya Jumatano, meya wa jiji hilo amesema mashambulia hayo yaliwaua karibu watu 21 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vikosi vya Urusi mara ya kwanza viliingia Kharkiv siku ya Jumapili lakini shambulio hilo lilidhibitiwa.
Picha ziliibuka zikionyesha wanajeshi wa Ukraine wakirusha makombora ya kurushwa kwenye kando ya barabara na wanajeshi wa Urusi, waliokuwa wakitembea kwa miguu, wakisonga nyuma ya magari ya kivita.

Ripoti zinasema kuwa mashambulizi ya makombora yameendelea karibu na Donetsk, ambayo imeshambuliwa na wanajeshi wanaovuka kutoka Belgorod magharibi mwa Urusi.
Wanadhaniwa kuwa karibwapiganaji 15,000 wanaoungwa mkono na Urusi huko Donetsk na Luhansk, ambao wanaweza kusaidia Urusi kusonga mbelee. Ukraine inaamini takwimu hiyo iko juuzaidi.
Mapigano pia yameendelea karibu na Sumy.
Mashambulizi kutoka kusini
Vikosi vya Urusi vimepiga hatua kubwa kutoka Crimeana magharibu na kuelekea Kherson kwenda Mariupol.
Wanajeshi wake walisemekana kuingia Kherson siku ya Jumanne usiku, huku wizara ya ulinzi ya Urusi ikidai kuwa iliuteka mji huo wa kusini Jumatano asubuhi.

Katika siku chache kabla ya uvamizi huo, Urusi ilitumia meli za kutua zenye uwezo wa kupeleka mizinga kuu ya vita, magari ya kivita na wafanyikazi, nje ya pwani ya Ukraine katika eneo kubwa la Bahari Nyeusi na Bahari ya Azov.
Maelfu hukimbia kuvuka mipaka
Tangu uvamizi huo uanze, zaidi ya raia nusu milioni wamekimbia, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Muungano wa Ulaya unakadiria kuwa hadi watu milioni nne wanaweza kujaribu kuondoka nchini kwa sababu ya uvamizi wa Urusi.
Wakimbizi wanavuka mipaka kuelekea nchi jirani za magharibi, kama vile Poland, Romania, Slovakia, Hungary na Moldova.















