Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afrika Kusini yafanya mazishi ya kitaifa kwa ajili ya Askofu mkuu Desmond Tutu
Ibada ya wafu ya mwanaharakati aliyepinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Askofu Mkuu Desmond Tutu inafanyika katika Kanisa kuu mjini Cape Town.
Tutu, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya amani ya nobel ambaye alisaidia kumaliza utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, alifariki Jumapili iliyopita akiwa na umri wa miaka 90.
Kifo chake kiliibua majonzi makubwa miongoni mwa raia wa Afrika Kusini.
Maelfu wametoa heshima zao za mwisho katika Kanisa kuu la St George's ambako mwili wake umekuwa ukilazwa katika jeneza la kawaida.
Tutu alikuwa mmoja wa watu waliokuwa na msukumo mkubwa nyuma ya vuguvugu la kumaliza sera ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi kwa ujumla iliyotekelezwa na serikali ya wazungu wachache dhidi ya weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kuanzia mwaka 1948 hadi 1991.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa asoma wasifu wake mkuu katika mazishi ya kitaifa Jumamosi, ambako watu 100 pekee ndio watakaohururia kwasababu ya masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Tutu alikuwa amesisistiza kuwa hapapaswi kuwa na matumizi ya "majivuno au ya kifahari" katika mazishi yake na akasema "anapaswa kuzikwa katika jeneza la bei ya chini kabisa iwezekanavyo".
Alisema pia kwamba ni maua tu katika kanisa kuu "kutoka kwa familia yake ", kulingana na Wakfu wa Tutu IP Trust na the Desmond and Leah Tutu Legacy
Majivu ya mwili wake yanatarajiwa kuwekwa nyuma ya madhabahu katika kanisa kuu la St George mjini Cape Town - Kanisa la Kianglikana ambalo alilihudumia kama Askofu mkuu kwa miaka 35.
Awali ilifichuliwa kuwa mwili wa Tutu utachomwa kwa kutumia mbinu ya maji -inayofahamika kama aquamate-iliyoelezewa kama mbinu Rafiki kwa mazingira kuliko kuuchoma kwa moto wa kawaida,
PICHA:
Watu wengi katika Cape Town walijitokeza kuupatia heshima mwili wa Tutu ambao umelala ndani ya jeneza.
Mwanaume mmoja kwa jina , Wally Mdluli, aliyesafiri kwa baiskeli umbali wa kilomita zaidi ya 1,000 (maili 620) kutoka upande Bloemfontein hadi Cape Town - alielezea jinsi alivyoomba msaada kutoka kwa marafiki na familia wamsaidie kulipia safari yake n ahata alivyolala kweney kituo cha mafuta njiani alipokuwa akija kwa mazishi.
"Nilihisi nimeridhika baada ya kuliona jeneza. Ni kama roho yake iko ndani yangu," alimwambia mwandishi wa BBC Nomsa Maseko mjini Cape Town.
Tutu alitumia haiba na utambulisho wake wa juu kuzuzungumza wazi dhidi ya ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa watu weusi katika nchi yake, kila mara akisema anazungumzia hivyo kwa misingi ya kidini na sio kisisasa.
Baada ya Nelson Mandela kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994,Tutu aliteuliwa naye katika Tume ya ukweli na maridhiano iliyobuniwa kuchunguza uhalifu uliofanywa na wazungu na weusi wakat iwa enzi ya ubaguzi wa rangi.
Unaweza pia kusoma:
Tutu alitunukiwa Tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1984 kwa mchango wake katika mapambano ya kumaliza mfumo wa ubaguzi wa rangi.