Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tristan Da Cunha:Kisiwa cha Uingereza katikati ya bahari ya Atlantic
Katikati ya bahari ya Atlantic kuna msururu wa visiwa vingi ambavyo havina watu
Katikati ya visiwa hivi kunakimoja kwa jina Tristan da Cunha ambao una mji wa kipekee wenye watu 244 pekee wanaoishi hapa,wote ni raia wa Uingereza lakini eneo hili lina katiba yake .
Mji huu kwenye kisiwa cha Tristan da cunha unaitwa Edinburgh of the seven seas na kuna mengi kuuhusu ambayo yanavutia na na mengine ya kushangaza
Mji ulio mbali kabisa na eneo lolote duniani
Huu ndio mji duniani ambao uko mbali sana na sehemu yoyote ya dunia.
Licha ya kuwa sehemu ya Uingereza mji huu uko mbali na taifa hoilo na sehemu pekee unayoweza kuufikia ni kutokea mji wa Capetown nchini Afrika Kusini .
Itakuchukua siku sita kusafiri kwa boti kufika kisiwa hicho kwani ni mwendo wa kilomita zaidi ya 2700.
Mji wa watu 244
Kila mtu katika mji huu anamjua mwingine na hivyo basi ni kama familia kubwa inayoishi katika kisiwa hiki . Familia zote 80 zinaozishi hapa zina mashamba makubwa ya kufanya kilimo .
Hakuna Hoteli
Hakuna sekta ya utalii hapa na ili kuja lazima upange safari yako mwaka mmoja kabla .
Ili kuja katika kisiwa hiki lazima umjulishe katibu wa msimamizi wa kisiwa kupitia barua pepe ambaye atafanya maandalizi ya jinsi utakavyoishi kwa muda wa ziara yako.
Mara nyingi utapewa makaazi kwa boma la mmoja wa wakaazi wa mji huu .
Hakuna uwanja wa ndege
Ili kusafiri hadi kisiwa hiki lazima utumie usafiri wa majini kwa sababu hakuna uwanja wa ndege.
Inawachukua watu siku kadhaa kusafiri wa boti hadi kisiwa hiki na hali inakuwa ngumu zaidi kwa watalii wa kushtukizia kwa sababu lazima uwe umeopanga safari yako mwaka mmoja kabla ya kuja .
Hakuna uhalifu
Wakaazi wa kisiwa hiki huwa hawafungi milango kuhofia kuibiwa majumbani mwao .
Milango yao huachwa wazi wanapokwenda kufanya shughuli zao za kila siku kwa sababu hakuna anayweza kuiba chochote .Watoto nao huruhusiwa kucheza kote bila vikwazo au kukaripiwa na yeyote .
Kisiwa hiki kina shule moja inayowahudumia wakaazi na pia daktari anayewatibu watu wote ni mmoja .
Kuwalisha watu wake
Kisiwa hiki kinategemea kilimo cha viazi na pia uuzaji wa samaki wa kamba wanaosafirishwa hadi nje ya mji kwa kipaton chake .
Malipo hapa yanafanywa na pesa taslimu na hakuna huduma za simu zinazotegemewa .Huduma za intaneti ni tete na kufanya mawasiliano kuwa magumu katika eneo hili .
Tristan da Cunha ni kisiwa chenye uwezo wa kuwalisha watu wake wote hakuna chakula kinachoagizwa kutoka nje .
Hakuna kulipa kodi ya nyumba
Hakuna asiyekuwa na makaazi hapa na hivyo basi hakuna kulipa kodi ya nyumba .Wakaazi wanaishi kwa starehe ka sababu kila mtu ana uwezo wa kujikumu na kujitiosheleza kimaisha .
Dharura ikitokea mji wa karibu wanakopelekwa watu kwa usaidizi wa matibabu ni Cape own nchini Afrika Kusini .Tatizo hapa ni panya .Panya wanatishia viumbe wa kisiwa hiki na huletwa na boti za wasafiri wanaokuja hapa
.Kila mwaka kuna sherehe ya 'Ratting day' ambapo wanaume hushindana kuwashika panya na wanaofaulu kuwanasa panya wengi hutuzwa