Kikundi cha Warusi kimerejea duniani baada ya kuchukua picha za filamu kwa mara ya kwanza katika anga za mbali

Klim Shipenko na muigizaji Yulia Peresild walipokuwa wakirejea duniani kutoka anga za mbali
Maelezo ya picha, Klim Shipenko na muigizaji Yulia Peresild walipokuwa wakirejea duniani kutoka anga za mbali
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Kundi la filamu la Urusi limerejea baada duniani baada ya kupiga picha za filamu kwa mara ya kwanza katika anga za mbali.

Klim Shipenko na muigizaji Yulia Peresild waliondoka katika Kituo cha kimataifa cha anga za mbali na kutua katika - kukutana na kundi jingine lililokuwa likichukua filamu ya tukio la kuwasili kwao.

Uchukuaji wa filamu katika Kituo cha kimataifa cha anga za mbali ISS haukufanyika tu bila masaibu-ambayo huitwa changamoto ya uchukuaji wa filamu.

Ijumaa eneo la ISS bila kutarajia lilipokea roketi, ambayo ilitulia kuchukua filamu ya eneo hilo la anga za mbali. Haikuwa sehemu uandishi wa filamu.

Katika ujumbe wa twitter wa kuaga ISS, Peresild alionyesha video ambapo wasafiri ambo nywele zao zilikuwa zinapepea huku wakielea ndani ya roketi ili kuondoa dhana potofu za wale wanaofikiria kuwa picha zao zote zilichukuliwa duniani:

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Filamu hiyo imekuwa ya aina yake ya mbio za anga za mbali-pampoja na Tom Cruise. Kwa Bw Cruise ni sehemu ya mradi wa Hollywood unaochukua filamu katika anga za mbali unaohusisha Nasa na SpaceX ya Elon Tusk.

Unaweza pia kusoma:

Chombo kilichowabeba Peresild na Shipenko, pamoja na Oleg Novitskiy, kilitua kwa parachuti duniani nyakati za muda wa chakula cha mchana Jumapili katika eneo la Kazakhstan.

kuondoka kwao kulicheleweshwa na hitilafu ya kimtambo ya kawaida , ambayo ilisababisha kupotea kwa udhibiti wa mkao wake kwa karibu saa moja na nusu.

The hatch was eventually opened and Peresild and her fellow crew members entered the ISS

Chanzo cha picha, Roscosmos

Maelezo ya picha, Peresild na wasafiri wenzake waliingia katika akituo cha nga za mbali ISS baada ya kupata tatizo la mtambo wa breki

Safari hiyo ilitangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya Urusi

Si wachukuaji wa filamu tu waliokumbana na tatizo la kiufundi. Walipowasili tarehe 5 Novemba mfumo wa moja kwa moja wa breki wa chombo chao Soyuz ulishindwa kufanya kazi na kamanda alilazimika kutumia mikono kuweza kukidhibiti.

Muigizaji na Muongozaji sasa watapelekwa katika ngome ya Urusi ya mafunzo ya nyota kwa siku 10 za ukarabati.