Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kikundi cha Warusi kimerejea duniani baada ya kuchukua picha za filamu kwa mara ya kwanza katika anga za mbali
Kundi la filamu la Urusi limerejea baada duniani baada ya kupiga picha za filamu kwa mara ya kwanza katika anga za mbali.
Klim Shipenko na muigizaji Yulia Peresild waliondoka katika Kituo cha kimataifa cha anga za mbali na kutua katika - kukutana na kundi jingine lililokuwa likichukua filamu ya tukio la kuwasili kwao.
Uchukuaji wa filamu katika Kituo cha kimataifa cha anga za mbali ISS haukufanyika tu bila masaibu-ambayo huitwa changamoto ya uchukuaji wa filamu.
Ijumaa eneo la ISS bila kutarajia lilipokea roketi, ambayo ilitulia kuchukua filamu ya eneo hilo la anga za mbali. Haikuwa sehemu uandishi wa filamu.
Katika ujumbe wa twitter wa kuaga ISS, Peresild alionyesha video ambapo wasafiri ambo nywele zao zilikuwa zinapepea huku wakielea ndani ya roketi ili kuondoa dhana potofu za wale wanaofikiria kuwa picha zao zote zilichukuliwa duniani:
Filamu hiyo imekuwa ya aina yake ya mbio za anga za mbali-pampoja na Tom Cruise. Kwa Bw Cruise ni sehemu ya mradi wa Hollywood unaochukua filamu katika anga za mbali unaohusisha Nasa na SpaceX ya Elon Tusk.
Unaweza pia kusoma:
Chombo kilichowabeba Peresild na Shipenko, pamoja na Oleg Novitskiy, kilitua kwa parachuti duniani nyakati za muda wa chakula cha mchana Jumapili katika eneo la Kazakhstan.
kuondoka kwao kulicheleweshwa na hitilafu ya kimtambo ya kawaida , ambayo ilisababisha kupotea kwa udhibiti wa mkao wake kwa karibu saa moja na nusu.
Safari hiyo ilitangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya Urusi
Si wachukuaji wa filamu tu waliokumbana na tatizo la kiufundi. Walipowasili tarehe 5 Novemba mfumo wa moja kwa moja wa breki wa chombo chao Soyuz ulishindwa kufanya kazi na kamanda alilazimika kutumia mikono kuweza kukidhibiti.
Muigizaji na Muongozaji sasa watapelekwa katika ngome ya Urusi ya mafunzo ya nyota kwa siku 10 za ukarabati.