Mkalimani ambaye alimsaidia Joe Biden 2008 aondoka Afghanistan

Bw. Khalili na familia yake

Chanzo cha picha, Safi Rauf/Human First Coalition

Maelezo ya picha, Bwana Khalili (wa tatu upande wa kushoto) na familia yake
Iliyochapishwa

Mkalimani wa Afghanistan aliyemuokoa Joe Biden ambaye wakati huo alikua seneta katika mazingira mabaya ya vijijini Afghanistan amefanikiwa kuondoka eneo hilo na familia yake.

Mwaka 2008, upepo mkali ulilazimishi helikopta iliyokuwa imembeba Bw. Biden na wabunge wengine wa Marekani kutua kwa ghafla katika bonde lenye theluji ambalo lilikuwa linawaweka hatarini kushambuliwa.

Aman Khalili alikua miongoni mwa wafanyakazi wa Marekani nchini Afghanistan ambao waliwapeleka Biden na kundi lake katika eneo salama.

Tangu mwezi Agosti, amekua akiomba asaidiwe kutatua masuala yake ya visa ili aweze kuondoka nchini humo.

Sasa anaungana na maelfu ya Waafghanistan waliokimbia nchini humo kwa kuhofia kuishi chini ya utawala wa Taliban.

Siku ya Jumatatu, mwakilishi wa idara ya mambo ya nje ya Marekani aliambia BBC kuwa Bw.Khalili na familia yake wameondoka "salama Afghanistan na baadaye kuendelea na safari kutoka Pakistan".

"Walifanya hivyo kwa ushirikiano wa hali ya juu na kutoka kwa serikali ya Marekani, na tunashukuru sana pia misaada kutoka kwa wahisani wengine waliotushika mkono."

Miaka 13 baada nafasi yake ya kukutana na rais wa baadaye wa Marekani, pamoja na maseneta Chuck Hagel na John Kerry - Bwana Khalili alikua anahangaika kupata Visa yake Maalum ya uhamiaji nchini Marekani (SIV)ili aweze kuondoka Afghanistan.

Kufuatia shughuli iliyokumbwa na vurughu ya kuwaondoa Afghanistan wafanya kazi wa Marekani msimu karibu miezi miwili iliyopita, Bw. Khalili alitoa wito kwa Bw. Biden kumuokoa yeye , mke wake na watoto wake watano," aliambia CNN. "Naamini anaweza kufanya kila kitu."

Alipoulizwa kuhusu hali ya Bw. Khalili mwezi Septemba, Msemaji wa Ikulu ya White House Jen Psaki alimshukuru kwa "kuwasaidia watu wangu kadhaa ninaowaenzi kutoka kwa Dhoruba ya theluji na kwa kazi yote uliofanya" na kusema kwamba Marekani "imejitolea" kuwaondoa washirika wake.

Shirika la Human First Coalition, ambalo linasaidia kuwaokoa zaidi ya Waafghanistan 200 ambao sasa wako Pakistan, limeambia BBC kuwa "linawashukuru sana" maafisa wa Marekani na Pakistan kwa kuwasaidia "katika juhudi zetu za kumhamisha mahali salama mkalimani wa Rais Biden na famili yake".

SIV ni Visa maalum ya uhamiaji ambayo ulitolewa hususan kwa raia wa Afghanistan na Iraq waliofanya kazi na vikosi vya Marekani katika nch ihizo zote mbili zilizokumbwa na mzozo. Haijabainika ikiwa Bwana Khalili amepatahati hiyo ya usafiri au anasafiri Marekani.

Tangu mwaka 2008, inakadiriwa kuwa karibu Waafghanistan 70,000 wamehamia Marekani kupitia mpango wa SIV.

Maelezo ya video, 'Tuliisaidia NATO na Marekani sasa tunawindwa kama wanyama'-Wakalimani wa Afghanistan