Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afghanistan: Je Qatar na Uturuki ni wakombozi wa Taliban Ulimwenguni?
Milio ya risasi kutoka kwa kundi la Taliban ilisikika katika mji wa Kabul kusheherekea kuondoka kwa mataifa ya kigeni wiki hii. Kuondoka kwa vikosi vya majeshi ya kigeni, kunaiacha Taliban wakitawala, huku mamilioni wa raia wa Afghanistan wakiwa hawana uhakika na maisha yao ya kesho.
Mataifa mbalimbali yenye nguvu yanapambana kufanya ushawishi wakati huu utawala wa kiislam ukirejea katika nchi hiyo. Katika mchakato huo mataifa mawili kutoka ulimwengu wa kiarabu na kiislamu yamejitokeza kuwa wapatanishi na wawezeshaji muhimu - Qatar na Uturuki.
Mataifa haya yanaangalia fursa, yote yanajaribu bahati yao, ambayo huenda ikaibua hata upinzani uliokuwepo nyuma, katika eneo hilo la mashariki ya kati.
Maafisa kutoka nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta Qatar wamekuwa wakisaidia nchi ambazo zinajaribu kujiondoa.
"Hakuna aliyeweza kuondoa raia wake wengi Afghanistan bila kuihusisha Qatar kwa namna moja ama nyingine," anaeleza Dina Esfandiary, mshauri mkuu wa shirika la msaada la kimataifa la ICG.
"Afghanistan na Taliban itakuwa ushindi muhimu kwa Qatar, sio tu kwa sababu itaonyesha ni kwa namna gani wanauwezo wa kushirikiana na Taliban, lakini pia itawafanya wawe watu muhimu kwa nchi za magharibi zinazohusika na mzozo wa Afghanistan," aliiambia BBC.
Wakati mataifa ya magharibi yakiondoka Kabul, thamani ya kidiplomasia kwa nchi hizi inaongezeka. Twitter iliyochapishwa na msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Qatar, Lolwah Alkhater, ilisema "Qatar… itaendelea kuwa msuluhishi wa kuaminika katika mzozo huu," aliandika hivi karibuni.
Kuzidi kutengeneza ukaribu na Taliban huenda katika siku zijazo kukasababisha makosa na mzozo zaidi huko mashariki ya kati.
Uturuki na Qatar ziko karibu na eneo lenye harakati nyingi za kiislamu, ambapo mara nyingi kumeleta mivutano na mamlaka za Misri, Saudi Arabia na UAE, ambao wanaoona makundi hayo yanayoendesha harakati ni hatari na tishio.
Ikiwa mataifa haya mawili yanaimairisha mahusiano yake na kidiplomasia na kundi la Taliban huko Asia ya Kusini, je, watu hawa wanaweza kuruhusiwa katika mataifa ya Mashariki ya Kati?
Dina Esfandiary anasema "Katika kipindi cha miaka 10 eneo hilo la mashariki ya kati limekuwa likisonga mbele na kurudi nyuma kati ya makundi ya kiislam na makundi yasiyo ya kiislam," anasema.
Kuzungumza na kundi la Taliban
Wakati wa utawala wa mwanzo wa Taliba katika miaka ya 1990 nchi tatu pekee zilikuwa na mahusiano na kundi hilo: Pakistan, Saudi Arabia na UAE.
Baade walikata uhusiano wao baada ya mashambulio ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani. Hata hivyo inaelezwa misaada ya kifedha iliendelea kutolewa na watu binafsi wa Saudi kwa miaka mingi.
Maafisa wa taifa hilo awali walikana kusaidia kundi la Taliban kifedha na kusema inachukua hatua kali kuzua fedha binafsi kuingizwa Afghanistan kutoka Taliban.
Lakini uwepo wa vikosi vya jeshi la Marekani nchini Afghanistan ni jambo lisiloungwa mkono na wamarekani wengi, milango iko wazi kwa mataifa yanayotaka kufanya diplomasia..
Kwa Qatar na Uturuki, mawasiliano na uhusiano wao la Taliban yalikuwa kwa njia tofauti.
Wakati utawala wa rais Barack Obama ukitaka kumaliza vita nchini Afghanistan, Qatar waliwakaribisha viongozi wa Taliban kuzungumzia juhudi za amani kuanzia mwaka 2011.
Ilikuwa hatua iliyoleta utata. Kuonekana kwa bendera ya Taliban ikipepea katika vitongoji vya Doha viliwaudhi wengi. Kwa Qatari hatua hiyo ilisaidia kuendeleza tamaa ya miongo mitatu ya kuwa na sera ya kigeni inayojitegemea - ambayo inaona kuwa ni muhimu kwa taifa ambalo ni nguzo muhimu kwenye kanda yake inayojumuisha pia mataifa ya Iran na Saudi Arabia.
Mazungumzo ya Doha yalifikia tamati katika makubaliano ya mwaka jana chini ya Rais Donald Trump wa Marekani aliyetangaza vikosi vya Marekani kuondoka nchini Afghanistan ifikapo Mei mwaka huu.
Na baada ya kuingia madarakani, Rais Joe Biden alitangaza kwamba anaongeza muda wa mwisho hadi Agosti 31, 2021 kwa Marekani na vikosi vyake kuondoka nchini humo.
Matumaini ya tahadhari
Uturuki, ambayo ina uhusiano mkubwa wa kihistoria na kikabila nchini Afghanistan, imekuwa na askari kanzu wengi nchini Afghanistan, na kusalia mwanachama pekee wa kiilsam kwenye muungano wa NATO katike eneo hilo.
Kwa mujibu wa wachambuzi, imetengeneza mahusiano ya karibu ya kijasusina baadhi ya wanamgambo wanaohusiwhaa na Taliban.
Uturuki pia ni mshirika wa karibu wan chi jirani ya Pakistan, ambako kutokana na mafunzo yake ya kidini , kundi la Taliban likaibuka.
Wiki iliyopita, maafisa wa Uturuki walifanya mazungmzo na Talibanyaliyodumu kwa masaa matatu ,wakati vurugu na ghasia zikiendelea kwenye uwanja wa ndege wa Kabul.
Baadhi ya mazungumzo yalikuwa ni kuhusu namna uwanja huo utakavyojiendesha wenyewe, ambao vikosi vya Uturuki viliulinda kwa miaka 6. Taliban imeshasisitiza kwamba vikosi vya Uturuki navyo viondoke kama ilivyo kwa vikosi vingine vyote vya kigeni nchini Afghanistan. Lakini mkutano wa juma lililopita unaonekana kama sehemu tu ya ajenda kubwa zaidi, anasema mchambuzi.
Rais Recep Tayyip Erdogan alisema anachukulua ujumbe kutoka kwa viongozi wa Taliban "matumaini ya tahadhari". Aliongeza kuwa "sihitaji ruhusa kutoka kwa mtu yeyote" kuhusu nani wa kuzungumza naye, pale alipoulizwa kuhusu kukosolewa kwake kutokana na mawasiliano na kundi hilo.
"Hii ni diplomasia," alisema alipozungumza na waandishi wa habar.
Akaongeza: "Uturuki iko tayari kutoa msaada wowote kwa ajili ya umoja wa Afghanistan lakini iitafanya hivyo kwa tahadhari."
Hatari ya kuharibu sifa
Nchi nyingi zimekuwa zikijaribu kutengeneza mahusiano fulani na kundi la Taliban tangu kundi hilo lishike hatamu Kabul, has akupitia usuluhishi wa Doha. Lakini Uturuki inaonekana iko kwenye nafasi nzuri zaidi, ingawa hilo linaonekana kuhatarisha sifa yake.
Prof Ahmet Kasim Han, mtaalam wa mahusiano kutoka chuo kikuu cha Altinbas huko Istanbul, Uturuki anaamini kwamba mahusiano zaidi nchini Afghanistan yatamruhusu Rais Erdogan "kupanua zaidi" ya sera yake ya kigeni na kwa kutumia msaada wa chama chake cha AK.
"Wanaichukuliwa Uturuki kama nchi muhimu kwenye ulimwengu wa kiislamu"
"Hata hivyo kama jukumu lao itafikia mahali ambapo nchi kama Uturuki inakuwa mfadhili, na kuanzisha utawala wa sheria za kiislam ambao kwa baadhi unahusishwa na ukatli, Uturuki isingetaa kujikuta katika hilo," aliomgeza.
Kwa Qatar, maafisa watakuwa na matuamini kuhusu wajibu wao kama msuluhushi utapungua badala ya kuongezeka.
Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikisimamia azungumzo ya mizozo kadhaa mikubwa katika eneo la mshariki ya kati. Lakini kuibuka kwa Arab Spring, wapinzani wake wamekuwa wakiituhumu kwa kuegemea zaidi kwa wapiganaji ama makundi ya kiislamu.
Mwaka 2017, Saudi Arabia, UAE, Misri na Bahrain zilikatiza mahusiano yao - tangu yaliporejeshwa Qatar imekuwa ikishutumiwa kwa kuwa karibu zaidi na Iran na kutingisha hali ya Amani ya eneo hilo kupitia kituo chake kikubwa cha habari cha
Al Jazeera; madai ambao nchi hiyo imeyapiga.
Kwa sasa kukiwa na hali ya sintofahamu kwa wananchi wa Afghanistan, Qatar na Uturukini miongoni mwa nchi zinazozungumza na kuwa karibu na Taliban huku China na Urusi zikivizia fursa hiyo siku za usoni.