Bernard Arnault: Jinsi tajiri wa mitindo, pombe anavyokaribia kuwa mtu mwenye pesa zaidi duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
Tajiri wa bidhaa za gharama kubwa Mfaransa Bernard Arnault amepanda kwa kasi katika chati ya mabilionea duniai na 'kutishia' kuchukua nafasi ya Jeff Bezos kama mtu tajiri zaid duniani.
Asubuhi ya jana Jumatatu Arnault ndiye alikuwa mtu tajiri zaidi duniani huku thamani yake ikifikia dola bilioni 186.3 - akimzidi Bezos ambaye utajiri wake ulikuwa dola bilioni 147.3.
Hata hivyo, Bezos tayari amerejea juu ya chati hiyo kwa sasa ambapo utajiri wake umefikia dola bilioni 188.2. Kwa sasa utajiri wa Arnoult ni dola bilioni 187.5. Tofauti ya wamatajiri hao wawili ni dola milioni 700 tu kwa sasa.
Utajiri wa Arnoult unatokana na nini?
Utajiri wa Arnault umepanda kutoka dola bilioni 76 alizokuwa nazo mwezi Machi 2020 sawa na ongezeko la zaidi ya dola milioni 110 kwa kipindi cha miezi 14 kutokana na kutoyumba kwa utendaji wa kampuni yake ya bidhaa za anasa ya LVMH (Louis Vuitton Moët Hennessy) wakati wa janga la corona.
Louis Vuitton ni chapa ya nguo za kifahari huku Hennessy ni moja ya pombe ghali.

Chanzo cha picha, Reuters
Hisa za LVMH, ambayo pia inamiliki chapa nyengine za kifahari za fasheni kama vile Fendi, Christian Dior na Givenchy, ilipanda kwa asilimia 0.4 wakati wa saa za mwanzo za siku ya Jumatatu, na kuliweka soko lake la hisa katika thamani ya dola bilioni 320 na kupandisha mapato ya binafsi ya Bw Arnault kwa zaidi ya dola milioni 600.
LVMH na Arnault wanawakilisha kupanda kwa kiwango kikubwa kwa kampuni za bidhaa za anasa na mitindo Ulaya wakati wa kipindi cha Lockdown.
Kwa miaka mingi, orodha ya matajiri zaidi wa dunia ya Forbes imekuwa kwa kiasi kikubwa ikitawaliwa na Wamarekani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nafasi ya kwanza imekuwa ikichukuliwa na raia wa Marekani Bezos, Elon Musk, Gates na Buffett kwa miongo miwili iliyopita, huku Mmexico mmoja pekee Carlos Slim akijitokeza kwenye orodha hiyo baada ya muda fulani.
Kwa miaka kadhaa katika mwanzo wa karne, matajiri wakuu wa Ulaya walikuwa Muasisi wa kampuni ya Aldi Theo ana Karl Albrecht wa supermarket fame. Walifika miongoni mwa watu 10 tajiri zaidi duniani lakini hawakuwahi kushikilia nafasi ya kwanza.
Bernard Arnault alikuwa miongoni mwa watu 10 tajiri zaidi duniani katikati ya mwaka 2005, akiwa na utajiri wa dola bilioni 13 . Arnault amekuwa miongoni mwa matajiri 5 wakuu duniani tangu mwaka 2018 na alikuwa nambari 11 mwaka uliopita. Alikuwa mtu wa tatu tajiri zaidi mwaka 2019, akiwa na utajiri wa dola bilioni 76.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hii ni mara ya pili kwa tajiri huyo ata kumpiku kwa muda mfupi Bezos na kuwa mtu tajiri zaidi duniani. Alifanya hivyo kwa mara ya kwanza usiku wa Disemba 16, 2019.
Tangu mwanzo wa janga, thamani ya utajiri wa watu tajiri zaidi dunaini imeyumba kwa kiasi kikubwa, huku wengi wakiongeza utajiri wao kwa mabilioni ya pesa.
Elon Musk alikuwa mtu tajiri zaidi duniani kwa muda mfupi Januari 2021, wakati thamani ya utajiri wake ilipogonga dola bilioni 189.7. Hicho kilikuwa ni kiwango cha kushangaza cha faida ya dola bilioni 165 tangu Machi 2020, ambapo alikuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 24.6
Matajiri watano wakubwa zaidi
- Jeff Bezos $188.2 bilioni
- Bernard Arnault 187.5 bilioni
- Elon Musk $152.5 bilioni
- Bill Gates $126.0 bilioni
- Mark Zuckerberg $117.7 bilioni













