Uhusiano wa China na Marekani : Marekani yaituhumu China kwa kuchukua hatuazaidi za uchokozi

Chanzo cha picha, Reuters
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameishutumu China kwa kuchukua hatua za uchokozi zaidi nje ya nchi na ndani ya nchi.
Amesema katika mahojiano na kituo cha habari cha CBS News , kwamba Marekani haikutaka kuiweka uchina katika kiwango cha chini, lakini haitairuhusu kudhoofisha sheria zenye misingi ya agizo la kimataifa.
Alisema kuwa makabiliano ya kijeshi ni kinyume cha maslahi ya nchi zote mbili.
Hali ya uhasama imeongezeka hici karibui juu ya biashara, ujasusi na janga.
Uhusiano wa Uchina na Marekani ni muhimu kwa pande zote mbili na dunia kwa ujumla, huku Beijing ikiutolea wito wa mara kwa mara utawala wa Washington kuboresha uhusiano ambao uliharibika chini ya mtangulizi wa Joe Biden, Donald Trump.

Bw Blinken alikiambia kipindi cha CBS cha 60 Minutes kwamba Bw Biden na kiongozi wa Uchina Xi Jinping waliongea kuhusu mada mbalimbali katika mazungumzo yao ya kwanza kwa njia ya simu, yaliyodumu kwa muda wa saa mbili, mwezi Februari.
"Rais Biden alikuwa wazi kwamba katika maeneo mbalimbali tuna wasiwasi mkubwa juu ya hatua ambazo Uchina imezichukua, pamoja eneo la Uchumi, ambayo inajumuisha wizi wa akilimiliki ," alisema.
Nusura aiite Uchina adui licha ya kwamba Marekani imeishutumu Beijing kwa kuiba mamia ya mabilioni ya dola katika biashara za siri na akilimiliki.
"Hatuna muda wa kupoteza wa kutokabiliana na China," alisema. "Kuna magumu kusema kweli katika uhusiano, iwe ni kwa upande wa upinzani, upande wa ushindani, iwe ni kwa upande wa ushirika wake."
Lakini alisema, ingawa Uchina inafanya kama "mtu ambaye anajaribu kushindana kwa haki na kwa kuongeza njia za upinzani ... sisi tuna ufanisi na uthabiti zaidi wakati tunapokusanya nchi kusema na Beijing: 'Hii haiwezi kuvumilika, na haiwezi '."

Chanzo cha picha, Reuters/EPA
Bw Blinken anafanya ziara mjini London kwa ajili ya kufanya mkutano wa ana kwa ana wa mawaziri wa nchi zilizostawi zaidi kiviwanda duniani G7 mbao unafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuibuka kwa janga la corona miaka miwili iliyopita.
Rais Joe Biden, katika hotuba yake kwa baraza la Congress wiki iliyopita, alisema kuwa hatafuti mzozo na Uchina na alisema kuwa alimwambia Rais in Xi katika mazungumzo naye kwa njia ya simu kwamba "tunakaribisha ushindani " yatawale nguvu ya dunia.












