Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ugonjwa usio wa kawaida wamuacha mwanamke mmoja na maumivu makali kwa miezi 16
Ugonjwa usio wa kawaida umemfanya mwanamke mmoja kupitia machungu mno kwa miezi 16 kabla ya kufanyiwa operesheni ya dharura iliyonusuru maisha yake.
Rebecca Bostock alianza kuona tumbo lake linavimba na kufikia Januari 2020, alikuwa anatapika kila anachokula 2020.
Kilichokuwa kinampa tabu ni tatizo la umeng'enyaji chakula tumboni ambalo hutokea sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo inapokandamizwa kati ya mishipa miwili ambapo njia ya kupitisha chakula hufunga ama kidogo au kabisa.
"Sitaki mwingine yeyote apitie nilichopitia," amesema.
Bi. Bostock, 32, alifanyiwa upasuaji wa dharura katika hospitali ambayo imesema ndani ya kipindi cha miaka 27 tangu ilipoanza kutoa huduma yeye alikuwa wa tatu kupata na ugonjwa huo huku wanaopatikana na tatizo hilo ikiwa ni chini ya asilimia 1.
Na kwamba ikiwa hangekimbizwa hospitali siku ile huenda angepoteza maisha.
"Tumbo langu lilikuwa limefura kiasi kwamba sikuweza kupumua, nilikuwa naumwa na siwezi kunywa dawa yoyote," alisema.
"Walichoniambia ni kwamba nahitaji kufanyiwa upasuaji haraka sana kwasababu huenda nisiwe hai saa kadhaa zijazo," amesema.
Kabla ya operesheni, Bi. Bostock alisema amekuwa akipitia maumivu ya ajabu kwa miezi 16, tumbo lake linafura, anapata homa mara kwa mara, anahisi kuumwa tu, ana harisha nakuhisi kisunzi. Pia uzito wake ulipungua kweli.
"Baada ya kumuona daktari mara ya kwanza nilitakiwa kubadilisha mlo wangu hatua ambayo ilionekana kunipa afueni, lakini hali yangu ikazidi kuzorota zaidi kiasi cha kushindwa hata kutembea na nikawa napata tabu kupumua."
Operesheni hiyo inahusisha kufungua njia za kumeng'enya chakula kulingana na maelezo ya Bi. Bostock aliyopewa na daktari.
Unaweza pia kusoma:
Bado hawezi kula vyakula vigumu lakini anaimani kuwa hivi karibuni ataruhusiwa kula chakula kama mwanadamu mwingine yoyote na sasa anataka kuelewesha wengine juu ya ugonjwa huo ili waweze kujua dalili zake mapema.
"Nataka kuelimisha wengine kwasababu najihisi mbarikiwa na mwenye faraja," amesema.
"Nashukuru madaktari na wauguzi walionusuru maisha yangu. Sina cha kuwalipa.
"Ugonjwa huo ni nadra kiasi kwamba hata madaktari hawaujui, kwahiyo kusaidia watu kujua dalili za ugonjwa huo litakuwa jambo la msingi", Bostock.