Ugonjwa usio wa kawaida wamuacha mwanamke mmoja na maumivu makali kwa miezi 16

Rebecca Bostock, hospital

Chanzo cha picha, Rebecca Bostock

Maelezo ya picha, Rebecca Bostock, kutoka Winchcombe katika Gloucestershire, anasema alikuwa na maumivu kwa miezi 16
Iliyochapishwa

Ugonjwa usio wa kawaida umemfanya mwanamke mmoja kupitia machungu mno kwa miezi 16 kabla ya kufanyiwa operesheni ya dharura iliyonusuru maisha yake.

Rebecca Bostock alianza kuona tumbo lake linavimba na kufikia Januari 2020, alikuwa anatapika kila anachokula 2020.

Kilichokuwa kinampa tabu ni tatizo la umeng'enyaji chakula tumboni ambalo hutokea sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo inapokandamizwa kati ya mishipa miwili ambapo njia ya kupitisha chakula hufunga ama kidogo au kabisa.

"Sitaki mwingine yeyote apitie nilichopitia," amesema.

Rebecca Bostock, hospital

Chanzo cha picha, Rebecca Bostock

Maelezo ya picha, Rebecca mwenye umri wa miaka 32, alifanyiwa upasuaji wa dharura baada ya tumbo lake kuvimba sana na kumfanya ahangaike kupumua

Bi. Bostock, 32, alifanyiwa upasuaji wa dharura katika hospitali ambayo imesema ndani ya kipindi cha miaka 27 tangu ilipoanza kutoa huduma yeye alikuwa wa tatu kupata na ugonjwa huo huku wanaopatikana na tatizo hilo ikiwa ni chini ya asilimia 1.

Na kwamba ikiwa hangekimbizwa hospitali siku ile huenda angepoteza maisha.

"Tumbo langu lilikuwa limefura kiasi kwamba sikuweza kupumua, nilikuwa naumwa na siwezi kunywa dawa yoyote," alisema.

"Walichoniambia ni kwamba nahitaji kufanyiwa upasuaji haraka sana kwasababu huenda nisiwe hai saa kadhaa zijazo," amesema.

Rebecca Bostock weight loss

Chanzo cha picha, Rebecca Bostock

Maelezo ya picha, Uzito wa mwili wa Rebecca ulishukwa kwa kiwango kisicho cha kawaida

Kabla ya operesheni, Bi. Bostock alisema amekuwa akipitia maumivu ya ajabu kwa miezi 16, tumbo lake linafura, anapata homa mara kwa mara, anahisi kuumwa tu, ana harisha nakuhisi kisunzi. Pia uzito wake ulipungua kweli.

"Baada ya kumuona daktari mara ya kwanza nilitakiwa kubadilisha mlo wangu hatua ambayo ilionekana kunipa afueni, lakini hali yangu ikazidi kuzorota zaidi kiasi cha kushindwa hata kutembea na nikawa napata tabu kupumua."

Rebecca Bostock, Chris Turton

Chanzo cha picha, Rebecca Bostock

Maelezo ya picha, Bi Bostock alipelekwa hospitalini na mchumba wake Chris Turton katika siku ya Ijumaa Kuuwakati hali yake ilipokuwa mbaya sana

Operesheni hiyo inahusisha kufungua njia za kumeng'enya chakula kulingana na maelezo ya Bi. Bostock aliyopewa na daktari.

Unaweza pia kusoma:

Bado hawezi kula vyakula vigumu lakini anaimani kuwa hivi karibuni ataruhusiwa kula chakula kama mwanadamu mwingine yoyote na sasa anataka kuelewesha wengine juu ya ugonjwa huo ili waweze kujua dalili zake mapema.

Rebecca Bostock at home

Chanzo cha picha, Rebecca Bostock

Maelezo ya picha, Rebecca anatumai kutumia uzoefu wake wa kuumia kutokana na hali yake kuzuia wengine kupitia masaibu aliyoyapitia

"Nataka kuelimisha wengine kwasababu najihisi mbarikiwa na mwenye faraja," amesema.

"Nashukuru madaktari na wauguzi walionusuru maisha yangu. Sina cha kuwalipa.

"Ugonjwa huo ni nadra kiasi kwamba hata madaktari hawaujui, kwahiyo kusaidia watu kujua dalili za ugonjwa huo litakuwa jambo la msingi", Bostock.