Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
BBC 'yapokea malalamiko 100,000 ' kuhusu taarifa zinazomuhusu Mwanmfalme Philip
BBC imepokea malalamiko 100,000 kutoka kwa umma juu ya namna inavyoangazia taarifa za kifo cha Mtawala wa Edinburgh Mwanamfalme Philip, kwa mujibu wa gazeti la Sun nchini Uingereza
Shirika hilo lilipangua utaratibu wake wa vipindi wakati Mwanamfalme Philip alipofariki siku ya Ijumaa , akiwa na umri wa miaka 99.
Vipindi maarufu nchini Uingereza vya EastEnders na kipindi cha fainali ya mashindano ya upishi MasterChe, vilisitishwa na badala yake vikawekwa vipindi vya habari, huku matangazo ya kituo kingine cha BBC - BBC Four yakizimwa kabisa.
BBC ilisema : "Tunajivunia taarifa na mchango wetu wakati wa matukio yenye umuhimu kwa taifa ."
Hatahivyo, ilikataa kuthibitisha idaidi iliyopokea ya malalamiko ya watu.
Unaweza pia kusoma:
Idadi inatarajiwa kujumuishwa katika matangazo yajayo kuhusu malalamiko hayo siku ya Alhamisi.
Idadi ya hiyo ya malalamiko 100,000 itaifanya taarifa ya kifo cha Mwanamfalme Philip kuwa taarifa ya kipindi maalumu iliyowahi kulalamikiwa zaidi katika historia ya vipindi vya BBC.
Vipindi vingine ambavyo vilipata malalamiiko ya hali ya juu ni pamoja na matangazo ya Jerry Springer: The Opera, yaliyopata malalamiko 63,000 mwaka 2005; na wito wa Russell Brand kwa muigizaji Andrew Sachs, ambao uliibua malalamiko 42,000 mbamo mwaka 2008.
BBC halikuwa shirika pekee lililobadili ratiba ya matangazo yake ili kuangazia kifo cha Mwanamfalme Philip, Televisheni za ITV na,Channel 4 zote pia zilirefusha muda wakie wa taarifa kufuatia kifo hicho.
Hatahivyo, watazamaji wengi waliamua kuacha kutazama televisheni hizo kufikia mwisho wa siku, huku idadi ya watazamaji wa ITV ikishuka kwa 60% ikilinganishwa na wiki iliyotangulia , kulingana na takwimu zilizotangazwa usiku huo.
Watazamani wa kituo cha televisheni cha BBC cha BBC One, walipungua kwa asilimia sita, huku BBC Two ikipoteza theluthi mbili ya watazamaji wake, ambapo watu 340,000 pekee ndio waliofungua televisheni hizo kati ya saa moja na saa tano usiku.
Kipindi kilichotazamwa zaidi katika channel moja Ijumaa usiku kilikuwa ni kipindi cha Channel 4 cha Gogglebox, ambacho kilikuwa na watazamaji milioni 4.2 .
Jumamosi, BBC iliweka fomu kwenye wavuti wake kuwawezesha watazamaji kulalamika kuhusu matangazo ya televisheni, ili kutambua ukubwa wa malalamiko.
Fomu hiyo iliondolewa Jumapili, baada ya idadi ya malalamiko kuanza kupungua, lilisema shirika hilo