Prince Philip: Jamii za Vanuatu zinazoomboleza kifo cha 'mungu' wao

Iliyochapishwa

Uingereza inapoomboleza kifo cha Mwanamfalme Philip, inajumuika na kabila moja kwenye kisiwa kimoja cha Pasific mbali sana na Uingereza.

Kwa miongo kadhaa, vijiji viwili kwenye kisiwa cha Wavanuatu cha Tanna vimemheshimu Mtawala wa Edinburgh kama mtu wa kiroho kama mungu.

Kipindi rasmi cha maombolezo sasa kinaendelea, na watu wengi wa kabila wanakusanyika Jumatatu katika sherehe ya kumkumbuka Prince Philip.

"Uhusiano kati ya watu wa kisiwa cha Tanna na watu wa Uingereza una nguvu sana ... Tunatuma ujumbe wa pole kwa familia ya kifalme na watu wa Uingereza," Amesema kiongozi wa kabila hilo Chief Yapa, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Kwa wiki chache zijazo, wanakijiji watakutana mara kwa mara kufanya ibada na matambiko kwa Mtawala huyo ambaye anaonekana kama "kizazi kilichotumiwa tena cha roho mwenye nguvu sana au mungu anayeishi kwenye moja ya milima yao", anasema mtaalam wa jamii Kirk Huffman ambaye amesoma makabila hayo tangu miaka ya 1970.

Labda watafanya densi ya kitamaduni na kuonyesha kumbukumbu za Prince Philip, wakati wanaume watakunywa kava, kinywaji cha sherehe kilichotengenezwa kutoka mizizi ya mmea wa kava.

Hii itafikia kilele na "mkutano muhimu" kama kitendo cha mwisho cha maombolezo. "Kutakuwa na utajiri mwingi kwenye maonyesho" ambayo inamaanisha mimea ya viazi vikuu na kava, anasema mwandishi wa habari aliyeko Vanuatu, Dan McGarry.

"Na pia nguruwe, kwa sababu wao ni chanzo cha msingi cha protini. Ningetarajia nguruwe wengi watauawa kwa hafla ya sherehe."

"Safari ya shujaa"

Kwa nusu karne, Harakati ya Prince Philip ilistawi katika vijiji vya Yakel na Yaohnanen - na kwa kilele chake ilikuwa na wafuasi elfu kadhaa, ingawa idadi inadhaniwa imepungua hadi watu mia chache.

Wanakijiji wanaishi maisha ya kawaida sana katika misitu ya Tanna, kama vile mababu zao walivyofanya. Kuvaa mavazi ya kitamaduni bado ni jambo la kawaida, wakati pesa na teknolojia ya kisasa kama simu za rununu hutumiwa mara chache ndani ya jamii yao.

Ingawa wanaishi kilomita kadhaa tu kutoka uwanja wa ndege ulio karibu, "walifanya tu chaguo la kutofautisha ulimwengu wa kisasa. Sio umbali halisi, ni umbali wa kimafumbo. Wako miaka 3,000 tu," anasema Bw McGarry, ambaye alikutana mara kwa mara na wanakijiji.

Utamaduni wa wanakijiji na njia ya maisha, huichukulia Tanna kama asili ya ulimwengu na inalenga kukuza amani - na hapa ndipo Prince Philip amechukua jukumu kuu.

Baada ya muda, wanakijiji wameamini kuwa yeye ni mmoja wao - utimilifu wa unabii wa kabila ambaye "ameondoka kisiwa hicho, katika hali yake ya kiroho ya asili, kupata mke mwenye nguvu nje ya nchi," anasema Bw Huffman.

"Akitawala Uingereza kwa msaada wa Malkia, alikuwa akijaribu kuleta amani na heshima kwa mila kwa Uingereza na sehemu zingine za ulimwengu.

Ikiwa angefanikiwa, basi angeweza kurudi Tanna - ingawa jambo moja lililomzuia lilikuwa, kama walivyoona, upumbavu wa wazungu, wivu, uchoyo na mapigano ya kila mara.

Na "dhamira yake ya kupanda mbegu ya utamaduni wa Tanna katikati ya Jumuiya ya Madola na Dola nzima ", Prince Philip alionekana kama mfano halisi wa tamaduni yao, anasema Bwana McGarry.

"Ni safari ya shujaa, mtu anayeanza harakati na anashinda binti wa mfalme na ufalme."

Hakuna mtu anayejua hasa jinsi au kwa nini harakati hiyo ilianza, ingawa kuna nadharia anuwai.

Wazo moja, kulingana na Bwana Huffman, ni kwamba wanakijiji wanaweza kuwa waliona picha yake na ile ya Malkia kwenye kuta za vituo vya wakoloni wa Briteni wakati Vanuatu ilikuwa bado inajulikana kama New Hebrides, koloni iliyosimamiwa kwa pamoja na Uingereza na Ufaransa.

Tafsiri nyingine ni kwamba iliibuka kama "athari kwa uwepo wa wakoloni, njia ya kuweka tena na kuchukua tena nguvu za kikoloni kwa kujihusisha na mtu anayeketi mkono wa kulia wa mtawala wa Jumuiya ya Madola," anasema Bw McGarry, akiashiria historia ya ukoloni wakati mwingine ya Wavanuatu.

Lakini wataalam wana hakika kwamba kufikia miaka ya 1970, Harakati ya Prince Philip tayari ilikuwepo, iliyotiwa nguvu na ziara ya wanandoa wa kifalme mnamo 1974 huko New Hebrides ambapo Duke angeshiriki katika tamaduni za kunywa kava.

Je Prince Philip alichukuliaje jambo hilo kwa ujumla?

Hadharani, alionekana kukubali heshima yao, akiwatumia barua kadhaa na picha zake mwenyewe kwa watu wa kabila, ambao nao walimrundukia zawadi za kitamaduni kwa miaka iliyopita.

Moja ya zawadi zao za kwanza ilikuwa rungu ya sherehe inayoitwa nal-nal, iliyotolewa wakati wa mkutano wa 1978 ulioitishwa na wanakijiji kuuliza habari zaidi juu ya Prince Philip, ambao Bwana Huffman alihudhuria.

"Kwa hivyo kamishina wa makazi wa Briteni alishuka, akawasilisha picha za Prince Philip. Mamia ya watu hawa walikuwa wakingoja tu karibu, wameketi au wamesimama chini ya vichaka. Kulikuwa kimya sana, ungeweza kusikia pini ikianguka anasema Bw Huffman .

Mmoja wa machifu kisha akampa rungu ile ili ampatie Prince Philip, na alitaka uthibitisho kwamba ameipokea. "

Ilitumwa hadi Uingereza, ambapo picha za Duke aliyeshikilia rungu zilichukuliwa na kurudishwa kwa wanakijiji. Picha hizo, kati ya kumbukumbu zingine, bado zinathaminiwa na wanakijiji hadi leo.

Mnamo 2007, watu kadhaa wa kabila walikutana na Duke kibinafsi. Wakisafirishwa kwenda Uingereza kwa kipindi cha Runinga cha Channel 4 kiitwach Meet the Ntaives na viongozi watano wa kabila walifanya mkutano wa pembeni na Mtawala huyo katika Kasri la Windsor ambapo walitoa zawadi na kuuliza atarudi lini Tanna.

Jibu lake, kama ilivyoripotiwa na watu wa kabila baadaye, lilikuwa la kuficha - "patakapokuwa na hali ya joto , nitatuma ujumbe" - lakini ilionekana alikuwa akiwafurahisha

Ingawa Prince Philip alikuwa anajulikana kwa ukweli wake na amekosolewa zamani kwa kutokuwa na hisia za kitamaduni, juu ya Tanna "anaonekana kuwa mwenye kuunga mkono sana na na mfahamu wa undani wa masuala yao ," anasema Bw Huffman.

Uhusiano wake na makabila umeendelea kupitia Prince Charles, ambaye alitembelea Vanuatu mnamo 2018 na kunywa kava ile ile ambayo baba yake alifanya miongo kadhaa iliyopita. Alipokea pia fimbo ya kutembea kwa niaba ya Duke kutoka kwa kabila la Yaohnanen.

Mwana anaendeleza na majukumu ya babake?

Kifo cha Duke sasa kimefungua swali gumu la nani atachukua nafasi yake katika ulimwengu wa kiroho wa makabila.

Majadiliano tayari yanaendelea, na inaweza kuchukua muda kabla ya kuamua juu ya mrithi wake.

Lakini kwa watazamaji wanaoijua Vanuatu, ambapo kawaida ya kikabila huamuru kwamba jina la chifu limerithiwa na kizazi cha kiume, jibu ni dhahiri. "Wanaweza kusema, amemwachia Charles aendelee na misheni yake," anasema Bw Huffman.

Hata kama Prince Charles atakuwa mwili wa hivi karibuni wa mungu wao, Prince Philip hatasahaulika wakati wowote hivi karibuni. Bwana Huffman anasema kuwa harakati hiyo inaweza kutunza jina lake, na mtu mmoja wa kabila amemwambia wanafikiria hata kuanzisha chama cha kisiasa.

Lakini la muhimu zaidi, "kumekuwa na wazo kwamba Prince Philip atarudi siku moja, iwe mwenyewe au kwa hali ya kiroho," anasema Bwana Huffman, ambaye anaongeza kuwa wengine wanaweza kufikiria kifo chake mwishowe kitasababisha hali hii.

Na kwa hivyo, wakati Duke wa Edinburgh amelala katika kasri ya Windsor kuna imani kwamba roho yake inafanya safari yake ya mwisho kuvuka mawimbi ya Bahari ya Pasifiki kwenda nyumbani kwake kiroho, kisiwa cha Tanna - kukaa na wale ambao aliwapenda na kumheshimu kutoka mbali miaka yote hii.