Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu tatizo la kutohesabu wafu Afrika
Ni mataifa manane pekee barani Afrika kati ya zaidi ya 50 yalio na mifumo mwafaka ya kuhesabu idadi ya wafu , uchunguzi wa BBC umebaini.
Hii sio tu kufeli kwa serikali kutambua majanga yanayowakumba watu binafsi lakini ina athari kubwa katika utengenezaji wa sera za serikali.
Mataifa yote isipokuwa mawili barani Ulaya - Albania na Monaco yana mifumo ya kusajili watu waliokufa duniani na barani Asia ni juu ya nusu ya tathmini ya data hiyo ya UN ndiyo inayoonyesha.
Lakini barani Afrika ni mataifa ya Misri, Afrika kusini, Tunisia na Algeria ,Cape Verde, São Tomé Príncipe, Seychelles na Mauritius ambayo yana kile kinachotajwa kuwa mifumo inayofanya kazi ya usajili wa iadi ya raia inayojulikana kama CRVS - inayorekodi vifo vya watu.
Mataifa yote yaliochunguzwa na BBC ikishirikiana na watafiti kutoka kwa tume ya kiuchumi ya Umoja wa Mataifa UNECA, yana mifumo ya kusajili vifo.
Lakini mara nyingi huwa imenakiliwa katika daftari tu, unapochunguza hawana mifumo hiyo iliohifadhiwa kidijitali.
Habari hiyo inaweza kutumika katika maeneo ya makaazi lakini hayawezi kusajili mwenenedo wa vifo katika viwango vya kitaifa
Wakati wa mlipuko wa virusi vya ebola na hivi sasa corona , kuwa na picha ilio sawa kuhusu ni nani anayefariki kutokana na nini na eneo gani ni muhimu katika kubaini ni wapi usambaza raslimali na ufadhili unapaswa kufanyika.
Hili pia lina athari kwa kufuatilia vifo vya akina mama na watoto kwa kuwa kuna idadi kubwa ya watoto ambao huzaliwa kwao na hata vifo vyao hukosa kurekodiwa.
Hatua hii sio tu hukosesha haki ya utambulizi , kupitia maneno ya William Muhwava , mkuu wa Demographia katika UNECA ilio na makao yake Addis Ababa - lakini pia ina maanisha kwamba watu hupata mafunzo.
''Ili kusaidia wanaoishi , tunahitaji kuwahesabau wanaokufa'', alisema mfadhili wa demographia katika Umoja wa Mataifa Romesh Silva akizungumza na BBC.
''Wale wanaokosa kurekodiwa katika sajili huwa masikini na kutengwa na jamii'' , aliongezea, na ukosefu wa habari kuhusu vifo hunamaanisha kwamba hatua za kukabiliana na vyanzo ama sababu za vifo hivyo hazichukuliwi.
Licha ya uwekezaji, mifumo ya CRVS haifanyi kazi na kulazimu serikali kutegemea tafiti ambazo inapofikiwa wakati wa kuzichapisha huwa zimepitwa na wakati, kulingana na Irina Dincu, kutoka kwa kituo cha mifumo ya CRVS.
Linapojiri suala la virusi vya corona kuna wasiwasi kwamba uwepo wake katika baadhi ya mataifa haueleweki.
Imeripotiwa sana kwamba idadi ya watu wanaofariki kutokana na Covid 19 barani Afrika ipo chini ikilinganishwa na maeneo mengine duniani.
Wataalamu wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko, hatua zilizochukuliwa katika baadhi ya mataifa, watu wenye umri mdogo na kinga iliotokana na virusi vingine vya corona huenda ndio sababu kuu.
lakini wanasayansi wa data wanasema kwamba hesabu ya kubaini iwapo idadi ya wanaofariki ni ndogo barani - haiwezi kufanyika katika mataifa mengi kutokana na ukosefu wa mifumo ya CRVS.
Hesabu ya watu waliofariki na Covid-19
Vifo vya kupitia kiasi ni kipimo kinacholinganisha vifo kamili wakati fulani huku idadi hiyo ikitarajiwa wakati kama huo mwaka uliopita.
Lakini pia hutegemea usajili kamili wa vifo. Ukitazama idadi ya vifo vya kupitia kiasi vinakupatia fikra kuhusu kupotea kwa maisha kunakosababishwa na Covid - 19.Pia inaonyesha vifo vilivyosababishwa kwa njia isio moja kwa moja na mlipuko huo kutokana na sababu kama vile ukosefu wa matibabu, hofu ya kwenda hospitalini na kushuka kwa uchumi.
Utafiti wa jarida la sayansi la Lancet katika mataifa 118 yalio na uchumi wa kadri, unakadiria kwamba muendelezo wa uharibifu wa mifumo ya afya kutokana na covid 19 unaweza kusababisha vifo zaidi vya watoto 1,157,000 na vile vya akina mama 56,700.
Afrika Kusini na Misri ni miongoni mwa mataifa manane ambayo yana sajili adimu za vifo, hivyobasi kuhesabu idadi ya vifo katika mataifa hayo ni suala la kawaida.