Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Howard Stringer: Daktari anayekimbia akiwa utupu nchini Uingereza ili kuchangisha fedha za wasiojiweza
Daktari mmoja nchini Uingereza amekuwa akikimbia kilomita tano kila siku akiwa utupu baada ya kuwaahidi marafiki zake kwamba atafanya hivyo iwapo hatua yake ya kuchangisha fedha itaanza.
Howard Stringer ,27, alianza kukimbia katka eneo la Liverpool akiwa amevalia nguo ya mwanamiereka wa Japan au Sumo ili kuchangisha fedha za hisani lakini akabadilisha nguo hizo na kukimbia utupu alipofikisha £500.
Dkt Stringer: Watu hunipongeza, kucheka na kutabasamu huku wakipiga picha.
Daktari huyo anasema kwamba aliona haya kwa mara ya kwanza alipokua akikimbia na nguo ya ndani lakini kila mtu amefurahia na amepata usaidizi wa hali ya juu.
Alichagua nguo ya ndani nyekundu ili kutofautisha na nguo ya ndani ya buluu zinazovaliwa na Mick Cullen , kwa jina maarufu Speedo Mick ambaye ametembea umbali wa taifa la Uingereza akivalia sare za kuogelea na kuchangisha £300,000 kusaidia watu wasiojiweza.
Dkt Stringer, anayefanya kazi katika hospitali ya Aintree, alisema kwamba afya ya ubongo imeangaziwa kwa kiwango cha juu kutokana na mlipuko wa virusi vya corona hivyobasi alikuwa anachangisha fedha za kampeni ya kuishi hali mbaya(CALM).
Amechangisha zaidi ya £1,500 kufikia sasa.
''Watu wanatambua kwamba hatuna furaha zaidi ya ilivyohitajika wakati huu hivyobasi kukimbia kwa kuvalia sare ya wanamiereka wa Japan ama nguo ya ndani huvutia tabasamu kutoka kwa raia lakini pia inatoa hamasisho'', alisema.